Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,121
- 14,032
Aisee hii kazi ya kulea kwa wanaume hapana, wacha niwapongeze tu wanawake.
Hii kazi ni ngumu. Mnaodai mnazalisha kisha mnalea naanza kuamini ni chai ya tangawizi kabisa! Labda kama unamchukua mtoto kwa mama yake ana miaka mitano kwenda juu. Tofauti na hapo utateseka na kukonda rafiki.
Juzi nimeachiwa watoto mapacha masaa matatu tu ila naona kama nimeachiwa mwaka mzima!
Ipo hivi: Majuzi mke wa kaka yangu, shem, kaugua kidogo. Hivyo wakampeleka hospitali. So mimi baadaye nikaenda kucheki hali ipoje pale home. Nikasalimia fresh. Sasa bro akaniambia dogo baki tu hapa utaondoka kesho shemeji yako akija. Nikakubali.
Sasa usiku sasa house girl na kaka wakatoka kufuata chakula sijui. Akaniambia ndugu tunakuja muda si mrefu, kuna watoto pia wamelala hapo (mapacha). Nikasema sawa. Dk 5 akaanza kulia mmoja.
Nikamchukua huyo anayelia. Akanyamaza sema aliponicheki usoni akaanza kulia zaidi (hanijui). Bembeleza wee wapi. Ni ka kike kana sauti kali kakamuamsha nduguye. Kazi ikawa ngumu zaidi.
Tumia mbinu zote zikafeli. Sipendagi ujinga wa hivi. Cha kufanya nikawabeba wote nikawapeleka chumbani kwenye kitanda kikubwa. Nikawaweka mwisho kabisa ili hata wakigaragara hapo kitandani wasianguke.Nikaendelea na mambo yangu.Wakalia hadi walipoona wametosheka.
Wale walivyorudi wakauliza vipi watoto hawajasumbua? Nikawahadithia wakafurahi wenyewe.
Mimi ukiniambia unazalisha tu halafu unalea nakusikitikia.
Ila kumbe mama zetu wanapotusikitikia huwa wanasikia uchungu sana.
Wakuu hii kazi ni ngumu. Mbarikiwe sana wanawake.