Kazi ya kulea si mchezo, mbarikiwe wanawake

Kazi ya kulea si mchezo, mbarikiwe wanawake

Ni ngumu kweli lakini wewe umeiyongezea ugumu mara 3 yake.
Kwanza wewe sio mzoefu, pili ugeni wa watoto hawakukuzoea ndio maana ulipata changamoto kubwa. Hongera akina mama wote.
Uzoefu ninao ila sio sana maana nilishirikiana na partner wangu kipindi mwanangu yupo mdogo.
Ila hata baba yao anakiri huwa wanamsumbua mno,mama yao ndo anawawezea.
 
Aisee hii kazi ya kulea kwa wanaume hapana, wacha niwapongeze tu wanawake.

Hii kazi ni ngumu. Mnaodai mnazalisha kisha mnalea naanza kuamini ni chai ya tangawizi kabisa! Labda kama unamchukua mtoto kwa mama yake ana miaka mitano kwenda juu. Tofauti na hapo utateseka na kukonda rafiki.

Juzi nimeachiwa watoto mapacha masaa matatu tu ila naona kama nimeachiwa mwaka mzima!

Ipo hivi: Majuzi mke wa kaka yangu, shem, kaugua kidogo. Hivyo wakampeleka hospitali. So mimi baadaye nikaenda kucheki hali ipoje pale home. Nikasalimia fresh. Sasa bro akaniambia dogo baki tu hapa utaondoka kesho shemeji yako akija. Nikakubali.

Sasa usiku sasa house girl na kaka wakatoka kufuata chakula sijui. Akaniambia ndugu tunakuja muda si mrefu, kuna watoto pia wamelala hapo (mapacha). Nikasema sawa. Dk 5 akaanza kulia mmoja.

Nikamchukua huyo anayelia. Akanyamaza sema aliponicheki usoni akaanza kulia zaidi (hanijui). Bembeleza wee wapi. Ni ka kike kana sauti kali kakamuamsha nduguye. Kazi ikawa ngumu zaidi.

Tumia mbinu zote zikafeli. Sipendagi ujinga wa hivi. Cha kufanya nikawabeba wote nikawapeleka chumbani kwenye kitanda kikubwa. Nikawaweka mwisho kabisa ili hata wakigaragara hapo kitandani wasianguke.Nikaendelea na mambo yangu.Wakalia hadi walipoona wametosheka.

Wale walivyorudi wakauliza vipi watoto hawajasumbua? Nikawahadithia wakafurahi wenyewe.

Mimi ukiniambia unazalisha tu halafu unalea nakusikitikia.

Ila kumbe mama zetu wanapotusikitikia huwa wanasikia uchungu sana.

Wakuu hii kazi ni ngumu. Mbarikiwe sana wanawake.
Kwan kaka yako haez kufuata chakula adi aende na house girl? Kuna jambo hapo[emoji19]
 
Hakuna kama mama mkuu. Na hapo sasa bado hukubadilisha nepi na kuvilisha. Na bado havijaumwa usiku kucha vinalia homa imepanda. Unaweza kutamani ardhi ipasuke. Wanawake wamejaliwa moyo wa upendo na uvumilivu wa hali ya juu sana.

Mungu awabariki mama zetu na kuwapa maisha marefu; na waliotangulia kwake Awape pumziko jema. Nasi tukiwa na kauwezo japo kidogo tusiwasahau. Waliteseka na kutuhangaikia sana [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
😍😍
Ameen
 
Wife Alisafiri Kwa Wiki Moja Kwenda Arusha Kumsalimia Dada Ake Mgonjwa,Nikabaki Na Mtoto Wetu Wa Mwenye Mwaka na mieizi 8,,picha likaanza mchana namsikia mtoto yupo jikoni vitu vimeanguka,naenda kufika nakuta katia ndoo ya unga maji namuliza vipi ananiambia anasonga ugali[emoji3]nikaishiwa pozi,,,nikimwambia usiguse hichi yeye ndo anagusa,,usiku kwake ndo mchana anacheza hata hadi saa sita na hataki nilale anataka tucheki katuni mara yupo juu ya meza,mara katoa viatu vya mama ake anavaa,,kina mama wana karama kubwa,,mama ake akiwepo mtoto saa tatu anakuwa ameshalala ila mimi hadi saa sita,,mama ake akiwepo japo ni mtundu ila haharibu vitu ila mimi hata nikimtishia atapanda juu ya meza atachama vituu baada ya siku mbili ikabidi nimpigie mama ake nimwambie aseh kazini kuna dharura ruhusa niloomba imesitishwa fanya urudii ila ukweli ni kwmaba niliona nimeachiwa mtoto nikae nae zaidi ya miaka miwili,,,siku mama ake amerudi nilishukuru kwakweli nikaona nimetua mzigo mzitoo
 
Hizo kazi ndio sipendi, mtoto atakuwa wangu akishashiba na kuogeshwa ili nipate kumlaza tu kifuani.
Akinya nakupa wewe, akilia nakupa wewe 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Unasemaaa!!!...muone unavyopenda Raha..malezi kusaidiana mtoto kanya mnawishe..akilia mbembeleze ili utengeneze chemistry nzuri na mtoto..we m'baba wewe..
 
Unasemaaa!!!...muone unavyopenda Raha..malezi kusaidiana mtoto kanya mnawishe..akilia mbembeleze ili utengeneze chemistry nzuri na mtoto..we m'baba wewe..
Sema mtoto wangu atakuwa sio kilizi sana 🤣🤣🤣🤣🤣!!!

Chemistry sindo nambembeleza alale akishiba. Nashukuru sana ujio wa pampers, maana nilipokuwa chalii niliwazaga lile zoezi ya kufua nepi ni noma.
 
Back
Top Bottom