Kazi Sina, Nazidi Kuchelewa Kuoa...

Kazi Sina, Nazidi Kuchelewa Kuoa...

Mkuu pole sana, Mungu atakujalia utapata kazi na utaoa tuu, ila unahitaji changamoto zaidi ili akili yako iweze kufanya kazi vizuri, nna mshkaji wangu alikuwa kama wewe ajira hapati na kujishughulisha na shughuli ndogo ndogo akawa hataki kampa mwanamke mimba baada ya hapo akili ilikaa sawa now ni mfanyabiashara hataki hata ajira tena...challenges zinasaidia sana ku boost akili na hasa ukiwa bado unakula na kulala kwa baba
 
Tangu mwaka 2011 mpaka today, job sina, umri unaenda, kuoa nashindwa, nimegraduate, nimefanya interview kibaao, but no job, jaman?

Pole sana kiongozi...naimani mwaka huu mungu atajibu maombi yako...mungu ni mwema usichoke kutafuta kazi na kumshirikisha mungu katika kila jambo ulitendalo...pole ndugu daima mapambano na siku zote ukiona matatizo yamekuandama kwa kasi ujue neema/mafanikio yapo karubu..
 
dah, pole sana bana, nakushauri uangalie plan b, huku ukiendelea kutafuta kazi taratibu.
 
Dah mkuu tafta mzigo mdogo mdogo upate mtaji, kuna watu eti unauliza hivi unataka kazi ili uoe? kwan jibu halijulikani? starehe ya dunia mwanamke mtulivu wewe siku hz kuajiliwa mmmmmh utachoka kama waenda kwa wale maali hadi milion kadhaa umejtakia hiyo ni hela ya wa biashara
Tangu mwaka 2011 mpaka today, job sina, umri unaenda, kuoa nashindwa, nimegraduate, nimefanya interview kibaao, but no job, jaman?
 
Kuna wenzio wana kazi na wana maisha mazuri kuoa kwao mtihanii
Kumbe kuwa na kazi siyo kuoa eee,kwa hiyo unamaanisha jamaa kama ana mpango wa kuoa aoe tu watakula hata godoro
 
...dah, jamaa kaongea kwa masikitiko sana mpaka kanihudhunisha, amini yote yanawezekana mkuu.
 
Mmmh hiyo kali a graduate houseboy utamlipa shilingi ngapi? kumbuka mwenzio akipata kazi anaoa so inabidi mshahara uwe reasonable

Atakama namlipa kiduchu its better than kukaa home
 
Nime maliza chuo 2012. Nikiwa na mategemeo makubwa sana,lakini baada ya mwezi sikuona chochote.
Nilikua nime panga so kodi ya nyumba ilikua ina hitajika.

Niliomba internship sehem flani,nikaahidiwa kulipwa laki 2,nikasema potelea mbali.
Nimefanya mwezi mzima,lakini sikupewa hata thumni. Nika sepa,nikaona bora kulala tu geto.

Ilitokea kibarua sehem flani (****),nikaambiwa mshahara laki8 ( :israel::israel🙂 , YES laki8.
Ni kazi ambayo iko nyuzi 180 tofauti na bachelor degree yangu.

Niliomba na nikapewa,kazi unapiga juani mda wote,jua kali balaa,jasho jingi,nguvu nyingi,nimesoma comp science nikijua kazi yangu ni viyoyozi tu ndani,lakini najikuta kwenye jua kaliiii la Dar,ndani ya ma-overall ya ma-engineer...... Kwanini Mungu wangu tabu hii?????

Haikua tabu,toka wakati huo hadi leo niko kwenye hiyo kazi (Potential yangu ilionekana though). Na mpaka sasa nimejenga na usafili mashallah.......

Point yangu ni kwamba sijui situation yako,lakini ACHA KUDEKA,USIDHANI DEGREE YAKO HAMNA MWENYE NAYO MTAANI. PIGA KAZI YOYOTE,HATA KAMA NI KUBEBA ZEGE BORA HUTEGEMEI WAZAZI. YOUR POTENTIAL WILL BE SEEN,YOU WILL BE DISTINGUISHED, ACHA KUKAA KIZEMBE,KAMA UNAWEZA INGIA JF BASI UNAWEZA KUFANYA KAZI YOYOTE,USILIE.


(Ops,by the way hata sihitaji kazi ya profesheni yangu)...

Speaker,Mvuja jasho.
 
Shule nyingi za private zinahitaji walimu sana, jaribu kuomba kufundisha kile ulichosomea kwa kuanzia badala ya kupoteza resource uliyonaya maana wewe tayari ni resourceful. Baada ya hapo unaweza kuanza mipango ya kuoa, tafuta mchumba kama bado lkn kama yupo tayari basi hongera. lkn pia kama tayari unaye mchumba ambaye tayari ana kazi mnaweza kukubaliana kuoana hata kabla wewe hujapata kazi kwani unapoingia kwenye ndoa wakati mwingine ndio mwanzo wa maendeleo yenu kwa sababu mnapokuwa wawili si sawa na unapokuwa peke yako. Ukichunguza sana utaweza kugundua kuwa wanaume wengi wameanza kuwa na maendeleo kimaisha mara tu wanapoingia kwenye ndoa. Usiogope, muombe Mungu atakusaidia.

Amwache kabisa! Kuna mahusiano mengine ni mikosi, hufanikiwi, kila unachogusa/fanya huoni matokeo yake.

Na kwa kuwa kakiri ame attend interview nyingi, nahisi kilichomfunga hajakitambua bado!
 
Tangu mwaka 2011 mpaka today, job sina, umri unaenda, kuoa nashindwa, nimegraduate, nimefanya interview kibaao, but no job, jaman?


Wewe ni --------.
Tena wadau msishangae kwanini nimesema hivi.
Nendeni jukwaa hili hili kuna post moja, jamaa mmoja ameiweka inasema "Baada ya udom kufanyisha watu interview...yatangaza tena nafazi za kazi". Huyu mpuuzi anajitapa kuwa ameajiri watu 7(kama sikosei) tena kajichanganya, mara asema ana GPA ya 2.5 mara 2.7.
Mjinga kabisa huyu.
cc: Invisible
 
Wewe ni --------.
Tena wadau msishangae kwanini nimesema hivi.
Nendeni jukwaa hili hili kuna post moja, jamaa mmoja ameiweka inasema "Baada ya udom kufanyisha watu interview...yatangaza tena nafazi za kazi". Huyu mpuuzi anajitapa kuwa ameajiri watu 7(kama sikosei) tena kajichanganya, mara asema ana GPA ya 2.5 mara 2.7.
Mjinga kabisa huyu.
cc: Invisible

njia ya muongo fupi asante kwa taarifa mkuu
 
Back
Top Bottom