Mshana ulichoandika umeandika kitu muhimu sana ingawa naona wachangiaji wengi wanakushambulia wewe na HAWA. wakati ukweli hilo halikuwa lengo lako. Lengo lako ni kwa diamond kutumia maudhui ya wimbo wa NITAREJEA kumsaidia HAWA.Tena umetaja mambo mawili yanayompa shida kwa sasa diamond ukamtaja video vixen Hamisa mobetto na wimbo wao wa Salome.
Wachangiaji hata hawamgusi mobetto kwa sababu hawaoni km anafanana na HAWA. Lkn hawajui mateso aliyonayo diamond kwa mobetto,wasichojua ni kwamba Hamisa mobetto anaweza kuchangia kumshusha kabisaa diamond na mobetto akaendelea kung'aa! Na pengine mshana ulipaswa kuweka pia Jambo la tatu kwa diamond ni kuhusu Baba yake. Hili nalo ni tatizo kubwa sana kwa diamond..!
Diamond hata km biashara ya muziki alimalizana na Hawa,bado sioni km kuna ukuta wowote wa kumzuia asimsaidie. Hebu tugeuze haya matokeo ya Hawa awe ndo diamond na diamond awe ndo Hawa. Hivi kweli watoto wa kike walivyo na huruma ataacha kumsaidia!?? Diamond bila kumung'unya maneno arejee amsaidie huyu Binti. Lkn Jambo la muhimu sana kwa diamond kwa sasa,aangalie sana,diamond sioni km ataendelea kuwa nyota kwa miaka 5 ijayo. Na diamond siku ambayo tu mziki wake utaachwa na wapenzi wake,ndo siku ambayo ataanza kuporomoka na watu hawataamini. Diamond anaishi maisha ya anasa,so akiyumba mwaka mmoja tu hata Mr.Nice au mwisho mwampamba watakuwa nafuu...!!!