Kauli zipi zinazokuchukiza hapa duniani?

Kauli zipi zinazokuchukiza hapa duniani?

mimi siipendi hii "mtumiaji simu unaempigia hapatikani kwa sasa tafadhali jaribu tena baadaye"
 
Nachukia sana mtu anaposema.....'sina hela'......hizi kauli zinakatisha tamaa sana.......watu wajirekebishe.........hasa wanaume.......

Ohooo! Mada imeanza kubakwa bila aibu....
 
Nachukia unapomtongoza mtu kuwa unampenda afu anakumbia Asante, hia sielewi kabisa hii asante inakuwa inakuweka njia panda huwa naichukia sana.
Hahahaha......kabisa mkuu hata mimi huwaga nakerekaga sana nikijibiwa jibu la hivyo.Vipi lakini kwema?
 
Nachukizwa na watu ambao kila siku salamu uwasalimie wao ikitokea umejisahau wao hawakusalimii unasema isiwe tabu kama vipi na wewe unauchuna hakuna kumsalimia,baada ya siku kadhaa unasikia huyu jamaa huwa asalimii.
 
kauli ya ccm itashinda hata kwa goli la mkono
 
Me nachukia mtu anakupigia simu na namba ngeni then anakuuliza we nani!!!....Korrkodio....
 
1.Haya maisha tu
2. Kwa hiyo unatakaje?
Sipendi hizo kauli..basi tu.
 
Back
Top Bottom