Kauli za Kikwete na Sirro zinaashiria kuna tatizo kwenye kifo cha Dkt. Reginald Mengi..

Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba wa mzee wetu. Mungu aendelee kumpumzisha kwa amani Dkt. Reginald Mengi. Amen!

Tangu zitangazwe taarifa za ghafla za kifo chake, kumetokea taarifa tata zinazodai kifo chake kina mkono wa mtu. Taarifa hizi zinaongozwa na mwanaharakati Mange Kimambi ambaye amefika mbali zaidi kwa kumtaja mke wa marehemu, Jacky na kijana Hussein wa Element kuhusika.

Awali zilionekana kama taarifa za umbea tu na uzushi lakini kwa kadri zinavyoanza kuzungumzwa na watu nyeti, jumlisha na kucheleweshwa kwa mwili wa marehemu, lipo jambo!

IGP Sirro amesema mwili ukishazikwa, Jeshi la Polisi litaanza kufuatilia ukweli wa kinachozungumzwa mitandaoni.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete nae amesema tusubiri ndugu wa marehemu waliopo Dubai waje wafafanue. Kwamba, ukweli utajulikana wakishawasili nchini. Maana yake, lipo la kuzungumzwa!

Hizi sio kauli nyepesi. Kama wao hawakupuuza, basi kuna mtiti unaendelea huko ambao unaonekana kufichwa fichwa!

Huenda wengi wetu tulishaamua kupuuza vijimaneno vilivyojitokeza na kumuombea mzee apumzike kwa amani, lakini hizi kauli zilizotolewa leo na zinazoendelea kutolewa zinatengeneza shauku ya kujua kuna nini cha ziada?

Nadiriki kusema JK na IGP wanafahamu kitu.. Ngoja tuone!
1. Nimeshangaa kuona Mange anadai kutumwa na familia ya Mengi
2. Familia ya Mengi ni ya kuogopwa kama Ukoma kama kweli ndio waliomtuma Mange
3. Familia ya Mengi wanataka kucheza mchezo mchafu wa kuchafua binti wa watu, ili hakose huruma kwa jamii wamdhurumu maana hawa jamaa pesa kwao ni kama Mungu , ndio maana walimpa taarifa tarumbeta mange kimambi
 
Ukweli ni kuwa mazingira ya kifo chake,na yaliyokuwa yanasemwa kabla kuhusu ndoa hiyo ni lazima speculations hizo ziwepo.Maana kila mtu alisema binti wa watu kafuata hela.So yanayozungumzwa ni sawa ila ukweli post mortem itaeleza kila kitu.But 77 yrs anything(sudden death) can happen.So ni bora kutokuhukumu na kusubiri matokeo ya uchunguzi.
Ni kweli maana hakuna sehemu ilishaandikwa kuwa mm(mengi) ntakufa kwa njia fulan, kifo hakina ahadi na tujifunze na kutambua kuwa kila aliyeumbwa na damu ya Yesu atarudi mavumbin, tunapokosoa njia ya Musaraba ni sawa na kumkufuru Mungu. Hngera muongoza njia shujaa wa busara na hekima kwa kuondoka katika shida za dunia. Amen
 
Awekwe chini ya ulinzi kwa Maneno yenu ya umbea au?..... Ww ukisikia kitu tu unaaminieeee ? Ebu pevuka aiseeh..
 
Dunia hii Ukiwa na Mtoto wa kike walau mmoja tu hata Kama ni Changudoa Mzazi jihesabu huko salama.Sisi tumezaliwa Wanaume watano wanawake Wawili lakini Bi mkubwa akiumwa sie Wanaume wagumu Sana kuchangamka tuko busy mnoo.
Nikiweka pembeni habari husika, maneno yako ni ya kweli kabisa, wanamume mara nyingi tunakuwa wazito kutokana na majukumu tulonayo, lakini pia hawa wenzetu baadhi yao wana huruma sana kwa wazazi
 
1. Nimeshangaa kuona Mange anadai kutumwa na familia ya Mengi
2. Familia ya Mengi ni ya kuogopwa kama Ukoma kama kweli ndio waliomtuma Mange
3. Familia ya Mengi wanataka kucheza mchezo mchafu wa kuchafua binti wa watu, ili hakose huruma kwa jamii wamdhurumu maana hawa jamaa pesa kwao ni kama Mungu , ndio maana walimpa taarifa tarumbeta mange kimambi
Wamdhulumu nini?!
 
Ingefaa zaidi huyo anayejiita mke wa marehemu Reginald Mengi na huyo basha wake Hussein wawekwe chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa "usalama wao"....watanzania tusikubali kuufumbuia macho huu upumbavu unaodaiwa kufanya na huyo mwanamke.

Mkuu una uhusiano gani na kipindi cha Miwani ya Maisha cha Radio One ya Bwana Mengi?

Maana naona ID na hicho kipindi the same same
 
Hiyo ndio corporate war hiyo bi dada ajiandae kisaikolojia tu, watamchafua mpaka akome, atawachwa wazi kila mmoja amuone mbaya ikiwezekana kuwanunua wote wenye midomo michafu waseme yote waliyotumwa yeye asiwe na msemaji hata mmoja ili pressure impande zaidi. Jamii yote ikimbize kama mwizi. Hapo asini tu hiyo mou mambo yaishe. Utatafutwa ushaidi kokote kule awekwe kwenye kona kama panya.

Mwanaume uwezi toka kwa mkeo unalalamika unatendewa ndivyo sivyo ukaaminika hata siku moja, ukianzisha vita na mama watoto wote wanakuwa jeshi moja na mama, hasa ukalogwe ukachukue mke mwingine yaani wewe ndio nduli kabisa. Mkeo kaanae kwa akili ni ngumu baba kushinda vita ukichukua mke mwingine jamii yote iko wired kukushambulia hasa kama kabinti kenyewe ni kasupu acha kabisa
 
Msiba wa Tajiri hasa tajiri wa Kiafrica ni nadra kupita hivi hivi
Hata angefia kwenye Ile Boeing ya Ethiopia tungeambiwa cha kuambiwa kuwa kuna Mkono wa fulani bin fulani
TX Moshi aliwahi pia kuimba


Each general rule has exception
 
Lazima kuna kitu!!
Na wanaochangia ukweli usijulikane ni jf na hao wakina mushi!!

Kivipi?

Kama elimu tunayo, tumebobea kila sekta kitaaluma, nje na ndani ya mfumo.

Kyasaka tulia. Acha kuwashwa washwa!
 
Back
Top Bottom