Kauli za Kikwete na Sirro zinaashiria kuna tatizo kwenye kifo cha Dkt. Reginald Mengi..

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba wa mzee wetu. Mungu aendelee kumpumzisha kwa amani Dkt. Reginald Mengi. Amen!

Tangu zitangazwe taarifa za ghafla za kifo chake, kumetokea taarifa tata zinazodai kifo chake kina mkono wa mtu. Taarifa hizi zinaongozwa na mwanaharakati Mange Kimambi ambaye amefika mbali zaidi kwa kumtaja mke wa marehemu, Jacky na kijana Hussein wa Element kuhusika.

Awali zilionekana kama taarifa za umbea tu na uzushi lakini kwa kadri zinavyoanza kuzungumzwa na watu nyeti, jumlisha na kucheleweshwa kwa mwili wa marehemu, lipo jambo!

IGP Sirro amesema mwili ukishazikwa, Jeshi la Polisi litaanza kufuatilia ukweli wa kinachozungumzwa mitandaoni.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete nae amesema tusubiri ndugu wa marehemu waliopo Dubai waje wafafanue. Kwamba, ukweli utajulikana wakishawasili nchini. Maana yake, lipo la kuzungumzwa!

Hizi sio kauli nyepesi. Kama wao hawakupuuza, basi kuna mtiti unaendelea huko ambao unaonekana kufichwa fichwa!

Huenda wengi wetu tulishaamua kupuuza vijimaneno vilivyojitokeza na kumuombea mzee apumzike kwa amani, lakini hizi kauli zilizotolewa leo na zinazoendelea kutolewa zinatengeneza shauku ya kujua kuna nini cha ziada?

Nadiriki kusema JK na IGP wanafahamu kitu.. Ngoja tuone!
 
Ingefaa zaidi huyo anayejiita mke wa marehemu Reginald Mengi na huyo basha wake Hussein wawekwe chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa "usalama wao"....watanzania tusikubali kuufumbuia macho huu upumbavu unaodaiwa kufanya na huyo mwanamke.
Unaweza kuthibitisha ili polisi wafanyie kazi?

Mengi ana ndugu, wana akili na wanaijua sheria. Kama kuna tatizo, wao ndio watakaokwenda kwenye vyombo vya dola ili hatua zichukuliwe.

Watanzania tuna mambo mengi asee, muda wa kuingillia maswala ya familia za watu unatoka wapi?
 
Sasa wale waliokuwa wanampinga Dada wa taifa sijui watasemaje kama wakubwa hawa wanatia shaka inawezekana kuna ukweli ndani yake
Ukweli ni kuwa mazingira ya kifo chake,na yaliyokuwa yanasemwa kabla kuhusu ndoa hiyo ni lazima speculations hizo ziwepo.Maana kila mtu alisema binti wa watu kafuata hela.So yanayozungumzwa ni sawa ila ukweli post mortem itaeleza kila kitu.But 77 yrs anything(sudden death) can happen.So ni bora kutokuhukumu na kusubiri matokeo ya uchunguzi.
 
Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba wa mzee wetu. Mungu aendelee kumpumzisha kwa amani Dkt. Reginald Mengi. Amen!

Tangu zitangazwe taarifa za ghafla za kifo chake, kumetokea taarifa tata zinazodai kifo chake kina mkono wa mtu. Taarifa hizi zinaongozwa na mwanaharakati Mange Kimambi ambaye amefika mbali zaidi kwa kumtaja mke wa marehemu, Jacky na kijana Hussein wa Element kuhusika.

Awali zilionekana kama taarifa za umbea tu na uzushi lakini kwa kadri zinavyoanza kuzungumzwa na watu nyeti, jumlisha na kucheleweshwa kwa mwili wa marehemu, lipo jambo!

IGP Sirro amesema mwili ukishazikwa, Jeshi la Polisi litaanza kufuatilia ukweli wa kinachozungumzwa mitandaoni.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete nae amesema tusubiri ndugu wa marehemu waliopo Dubai waje wafafanue. Kwamba, ukweli utajulikana wakishawasili nchini. Maana yake, lipo la kuzungumzwa!

Hizi sio kauli nyepesi. Kama wao hawakupuuza, basi kuna mtiti unaendelea huko ambao unaonekana kufichwa fichwa!

Huenda wengi wetu tulishaamua kupuuza vijimaneno vilivyojitokeza na kumuombea mzee apumzike kwa amani, lakini hizi kauli zilizotolewa leo na zinazoendelea kutolewa zinatengeneza shauku ya kujua kuna nini cha ziada?

Nadiriki kusema JK na IGP wanafahamu kitu.. Ngoja tuone!

Hata mimi nimeona inaonekana na kuna suala zito ambalo sisi hatulifahamu lakini nahisi wakubwa wameshajua kilichotokea.
 
Back
Top Bottom