Kauli ya Waziri Mkuu imebeba ujumbe mzito si ya kubeza. Jaribu kufikiri kwa upana

This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,903
4,979
Waziri Mkuu ametilia shaka barakoa kutoka nje kuwa tujishonee wenyewe. Kuna watu wanabeza hii kauli, Kuna wanaodhihaki hata kutoa kauli chafu, kuna wanaotetea hii kauli kwasababu tu imetolewa na mwenzetu ktk serikali au chama. Kuna wanaoongea kwa hofu kwanini PM atoe kauli hii.

Kuna wanaofikiri nje box ambao Ni wachache na mimi ni mmoja wao.

Mosi, Watu wanahoji TBS kazi yao Ni nini km Waziri Mkuu anatoa kauli ya mashaka kama hii. Waziri mkuu anajua uwezo wa TBS katika kupima na kujiridhisha ubora wa bidhaa km hii. Hapa kuna mambo mawili ambayo mashaka ya Waziri Mkuu hayajagusia:
a. Je, Ni barakoa SALAMA lakini tatizo tu hazina ubora kwa maana hazina uwezo wa kuzuia kirusi kupenya.
b. Ni barakoa zenye UBORA lakini tayari zina maambukizi na si salama kwa matumizi.
Haya ndiyo ambayo unaweza kuyafikiria na kujiuliza Je, TBS wana uwezo wa kudhibiti yote mawili? Ubora na Usalama.

Pili, simsemei Waziri Mkuu, lakini fikra zangu zinanielekeza kuona kwamba hii ni kauli ya tahadhari kwasababu msimamo wa serikali yetu kimataifa unaeleweka juu ya suala la korona. Ni msimamo ambao si kuwafurahisha. Korona ni suala lenye malengo ya kiuchumi ndani yake, lengo ambalo Tanzania tunalikwamisha. Kwahiyo wanaweza kutumia njia ya kuingiza barakoa zisizo salama ili maambukizo yawe juu, vifo viwe vingi ili kuonyesha dunia kuwa tumefeli, na hivyo kwenda kusujudu kwao na kupokea chanjo ambayo pengine nayo si Salama.

Wametengeneza tatizo na wao ndiyo wanaokuja na suluhisho. Suluhisho Ni chanjo ambayo itawaingizia matrilioni ya shilingi, na pengine chanjo yenyewe si salama., Tukajikuta tunanunua mauti yetu kwa pesa zetu.

Tatu, Waziri Mkuu Ni mtu nwenye access ya habari nyeti za ndani na nje ya nchi, hivyo yuko informed vya kutosha kuhusu kinachoendelea hata kwa nchi majirani. Si nchi zote jirani zinakubaliana na msimamo wa serikali yetu. Wanaweza kutumika pia.

Chakula ulichopika mwenyewe nyumbani Ni salama kuliko cha hotelini au mghahawani.

Wakati mwingine kuna kauli zinatolewa na serikali Ni kwasababu ya tahadhari na nia njema. Kwa hali km hii Ni vyema tukadoubt kila kitu juu ya korona na tukachukua tahadhari.

Ushauri: Serikali inapaswa kutoka hadharani na kutangaza hadharani korona ipo na inauwa.Inatamkwa tu kuchukua tahadhari bila kukiri uwepo wake.

Kuna mwananchi kila kitu lazima asikie serikali inasema ndiyo anaona ni jambo siriazi.

Serikali ina plani gani baada pengine hii ya kujifukiza na tiba asili kufeli. Imejipanga kiasi gani?

Watanzania tuchukue tahadhari, tuache mzaha, si lazima kila kitu uambiwe na serikali.
 
Kirusi cha corona kina kaa kwenye nguo kwa mda wa siku ngap na barakoa zinasafirishwa n kutufikia kwa siku ngap vitu vingine tujiulize maelezo mengii kma ni vita ya uchumi ni kwetu tu au Tanzania kuna nn cha pekee mpka tupigwe vita ya kiuchumi kenya tu hatuwawez kiuchumi ndio tuje tuwe n vita n wazungu akili yang imegoma kulishwa ujinga
 
Nimezungumzia vita ya uchumi kwa maana ya mauzo ya chanjo ya korona. Umesahau kuwa uchumi wetu Ni rasilimali zetu,unafikiri mzungu hawazihitaji.KWANINI TUNA GESI ASILIA LAKINI LEO HII HATUYAONI MANUFAA YAKE.Kama umesoma kwa makini.

Kuhusu uhai wa kirusi, sayansi, teknolojia imekua sana hakuna linaloshindikana. Mbona Ni jambo jepesi tu.
 
Usalama wa barakoa kutoka nje sio suala jipya kuhojiwa. Akili za kawaida zingetegemea kungetokea juhudi za kiuchunguzi na kampeni za kupita maduka ya dawa na sokoni kama ambavyo mamlaka zimekuwa zikifanya Kwa vipodozi.

Unless haya yamefanyika kimya kimya, kuna wa kuwajibika Kwa sio tu kupuuza kauli ya Rais, Bali kuhatarisha maisha. Kumbuka barakoa tunazonunua madukani (hasa ya dawa) ndio zinazotumika na watoa huduma za afya Kwa sehemu kubwa.

Sijui kama nao wanashauriwa washone za vitambaa Kwa matumizi ya kitabibu. Kuna swala pia la nini tumefanya toka mlipuko ufike nchini kwetu karibu mwaka mmoja sasa, kuhakikisha upatikanaji na ubora wa barakoa zetu wenyewe. Pengine hatuna muda wala rasilimali za kujenga uwezo wa ndani kwa kuanzia au kutumia viwanda vilivyopo.

Lakini hatuwezi kwepa jukumu la kuweka viwango ili kama tunajitengenezea wenyewe au kununua kwa mafundi cherehani, tujiridhishe tunatumia kinga stahiki. Wave ya Kwanza kulikuwa na muongozo wa jinsi ya kutengeneza barakoa (idadi ya layer, Aina ya kitambaa n.k). Naamini huu ulikuwa informed na maelekezo yenye merit ya kisayansi. Binafsi sijaona juhudi za wazi za kuenforce ubora huu kwenye barakoa zetu.

Kumuachia kila mjasiriamali atengeneze na kuuza barakoa bila viwango na usimamizi halafu tukajiaminisha tunapambana ni kujidanganya.
 
Tabia za viongozi wa kiafrika wakishindwa kuwajibika kwa raia wao wanawaangushia lawama wazungu.bidhaa ngapi zinatoka ulaya watumie barakoa tu,zuieni zote.
Mitaani Kuna sidiria hata chupi za mitumba,mataulo toka USA na EU.msitutie urofa wakati mnajua uongo.
Kuna watu sasa hivi Tanzania na Afrika na dunia wanakufa kwa KUSHINDWA kupumua kwa kuvaa sidiria na chupi za mtumba .

Korona Ni mpango maalumu kwa malengo maalumu na wakati maalumu.

Fikiria tena.
 
Serikali inapigia Debe tununue barakoa zao hizi style zao za kusingizia barakoa za kutoka nje zina madhara ni uongo Tu huyu Mzee yupo Tayari kupiga marufuku barakoa za nje ilimradi apate hela
 
Kuna watu sasa hivi Tanzania na Afrika na dunia wanakufa kwa KUSHINDWA kupumua kwa kuvaa sidiria na chupi za mtumba .

Korona Ni mpango maalumu kwa malengo maalumu na wakati maalumu.

Fikiria tena.
Laumu rafiki zetu wachina ndio chanzo,mpaka Sasa wagomea WHO kuchunguza source halisi kule wuhan.kwa hili waacheni wazungu
 
Ukivaa barakoa huna imani
Wanakubeza
Unapuuzwa
Kama mh alivyowapa makavu live masister waliovaa barakoa zao UCHWARA
Screenshot_20210221-132656_1613903265359.jpg
 
Kiongozi mkuu wa serikali kama ulivyosema na access na taarifa nyeti halafu anaenda kwenye majukwa kutoa tahadhari kwa dhana? acha utani mkuu.. Serilaki ina uwezo wa kupiga marufuku hakuna kuingiza barakoa to nje kauli moja tu, wewe unaingiza katika soko unachukuwa tax halafu unawaambia watu hii kitu hatari. hebu tuwe serious kidogo.

Hatuna best intelligence kuna yule Kigogo tu mwaka sijui wangapi wameshindwa kumjuwa nani waje na taarifa hizi bila kuchukuwa hatua. Taarifa anazo lakini action zero anatizama tu raia wake wanavaa mask kuwauwa. Mimi nimevaa hizo mask na Mungu kanijalia sijapata hiyo corona sasa walete ushahidi hadharani.
 
Waziri Mkuu ametilia shaka barakoa kutoka nje kuwa tujishonee wenyewe. Kuna watu wanabeza hii kauli, Kuna wanaodhihaki hata kutoa kauli chafu, kuna wanaotetea hii kauli kwasababu tu imetolewa na mwenzetu ktk serikali au chama. Kuna wanaoongea kwa hofu kwanini PM atoe kauli hii.
Nimeona uzi wenye ujumbe kama huu kutoka kwa ndugu Erythrocyte ambae nae amesema:
Nchi yenye wasomi wengi kama Tanzania haiwezi kunyamazia kauli ya Mh Majaliwa ya ku ignore barakoa zilizotumiwa na madaktari wetu miaka nenda rudi kuwalinda na maambukizi ya magonjwa wanapowahudumia watanzania kwenye hospitali za umma na nyinginezo .
Sina lengo la kumtetea PM lakini ningependa kuwakumbusha tu kwamba mambo ya hovyo YOTE yanayotamkwa na kufanywa na viongozi wa chama na serikali wao wanaendelea kufuata yale yale ya yaliyowahi kutamkwa na Mheshimiwa Rais, si mara moja wala mara mbili! Suala la barakoa kuitwa matambara lilianzishwa na Rais June mwaka jana.

Kuanzia dakika ya 5, Mheshimiwa Rais anasema
Na nimeshatoa wito kwa wizara ya afya,na viongozi wangu mikoani na wilayani. Ukiona mtu anagawa barako kwa wananchi, ashikwe na akaulizwe zimekuwa verified wapi. Tutaumia kwa kukosa maarifa. Ukitaka kuvaa barakoa, kashone yako. Mbona ni rahisi tu. Barakoa mbona imekaa kama titi moja la mtu mmoja hivi, limekatwa upande.
Hoja yangu ni kwamba, tutapiga kelele kuhusu akina PM, akina Mama Gwajima na wapuuzi wengine wengi tu lakini kiini cha haya yote ni rais!!! Ni Mheshimiwa rais ndie alianza kuzi-discredit barakoa. Na hata katika kauli yake ya kwamba kashone yako ni katika kupoza poza tu lakini furaha yake ni kusema "watu wasivae barakoa" lakini kwavile anajua hata watoto wadogo watamshangaa ndo hapo anapoza kwa kusema "kashone yako" ili wanaomuunga mkono waendelee kusema kama wanavyosema kwamba "rais hajakataza kuvaa barakoa" ingawaje yeyote mwenye akili timamu anafahamu Rais amekuwa aki-discredit jitihada za kupambana na hilo gonjwa since Day One.

Na kama alivyosema Erythrocyte kwenye uzi wake, hizi barakoa zimekuwa zikivaliwa kwa miaka na dahali, kwanini Rais aanze kuzitia kasoro hivi sasa?! Tukumbushane pia kwamba ni rais huyu huyu baada ya kuzitia kasoro barakoa, akageukia kwenye vifaa vya kupimia ugonjwa wenyewe. Waswahili wanasema ukitaka kuua nyoka mkate kichwa, hawa akina Majaliwa ni mkia tu wakati kichwa chenyewe ndo kile ambacho kikiona mambo magumu, anakimbilia Chato na anapokuwa huko bado huwa haachi kuwakejeli wanaojikinga.
 
Waziri Mkuu ametilia shaka barakoa kutoka nje kuwa tujishonee wenyewe. Kuna watu wanabeza hii kauli, Kuna wanaodhihaki hata kutoa kauli chafu, kuna wanaotetea hii kauli kwasababu tu imetolewa na mwenzetu ktk serikali au chama. Kuna wanaoongea kwa hofu kwanini PM atoe kauli hii.
Ameshakamata containers ngapi za barakoa fake na kuzichoma? Amechukua hatua gani until now baada ya kugundua?

Wanaleta siasa tu!
 
hiyo ni version ya kuficha mapungufu yao ya kiuongozi nyuma ya vita fulani hivi tunavyopigana na mabeberu. hizi barakoa zinatengezwa na maswahiba, ma dictator wa democrasia za kisocialist wenzao wachina, lakini wao wanadai ni za mabeberu.
 
Hili neno la vita ya kiuchumi kwangu nachukulia kama ficho la udhaifu na ukosaji wa point za msingi katika kuhalalisha hoja, vita ipi ya uchumi tunayopigana sisi na dunia mpaka tujione special sana kiasi cha kusambaziwa CORONA, kila kukicha tunaomba misaada toka kwao, kila kukicha deni la Taifa linapaa kwa kuwakopa, kama wangekuwa katika vita na sisi hiyo misaada wala wasingeiotoa, nafikiri itafutwe hoja nyingine ya msingi lakini sio VITA YA KIUCHUMI.
 
Kiongozi mkuu wa serikali kama ulivyosema na access na taarifa nyeti halafu anaenda kwenye majukwa kutoa tahadhari kwa dhana? acha utani mkuu.. Serilaki ina uwezo wa kupiga marufuku hakuna kuingiza barakoa to nje kauli moja tu, wewe unaingiza katika soko unachukuwa tax halafu unawaambia watu hii kitu hatari. hebu tuwe serious kidogo. Hatuna best intelligence kuna yule Kigogo tu mwaka sijui wangapi wameshindwa kumjuwa nani waje na taarifa hizi bila kuchukuwa hatua. Taarifa anazo lakini action zero anatizama tu raia wake wanavaa mask kuwauwa. Mimi nimevaa hizo mask na Mungu kanijalia sijapata hiyo corona sasa walete ushahidi hadharani.
Labda ,Kuna kitu najiuliza Sana,pengine kuna kitu hata Rais hataki kukisema wazi.JPM ana discourage kila mtu aliyevaa barakoa kunani?

Leo akiwa kanisani amekiri korona ipo tuchukue tahadhari.Lakini hapo hapo anawabeza masister wawili waliovaa barakoa na kumsifu yule ambaye hajavaa.

Nahisi kuna jambo la ziada zaidi ya ubora, usalama na imani ambalo rais analijua. Yeye anasisitiza imani kumtegemea Mungu tu lkn mengine yote anayaignore.

Sijui km kuna mtu anawaza km mimi.
 
Kirusi cha corona kina kaa kwenye nguo kwa mda wa siku ngap na barakoa zinasafirishwa n kutufikia kwa siku ngap vitu vingine tujiulize maelezo mengii kma ni vita ya uchumi ni kwetu tu au Tanzania kuna nn cha pekee mpka tupigwe vita ya kiuchumi kenya tu hatuwawez kiuchumi ndio tuje tuwe n vita n wazungu akili yang imegoma kulishwa ujinga
Hukubahatika kusoma baolojia?
Ungelijua sifa za virusi usingeuliza swali hilo la kukaa siku ngapi, hata ingekuwa miaka million ila akipata host anakuwa hai tena.
 
Hili neno la vita ya kiuchumi kwangu nachukulia kama ficho la udhaifu na ukosaji wa point za msingi katika kuhalalisha hoja, vita ipi ya uchumi tunayopigana sisi na dunia mpaka tujione special sana kiasi cha kusambaziwa CORONA, kila kukicha tunaomba misaada toka kwao, kila kukicha deni la Taifa linapaa kwa kuwakopa, kama wangekuwa katika vita na sisi hiyo misaada wala wasingeiotoa, nafikiri itafutwe hoja nyingine ya msingi lakini sio VITA YA KIUCHUMI.
Bosi wake leo kasema nchi wanaovaa barakoa ndio wanakufa zaidi kwa corona, sasa nchi waliokufa zaidi ni boss wa mabeberu, USA, yeye sijui anatumiwa corona kwenye barakoa na nani?
 
Labda ,Kuna kitu najiuliza Sana,pengine kuna kitu hata Rais hataki kukisema wazi.JPM ana discourage kila mtu aliyevaa barakoa kunani?

Leo akiwa kanisani amekiri korona ipo tuchukue tahadhari.Lakini hapo hapo anawabeza masister wawili waliovaa barakoa na kumsifu yule ambaye hajavaa.

Nahisi kuna jambo la ziada zaidi ya ubora, usalama na imani ambalo rais analijua. Yeye anasisitiza imani kumtegemea Mungu tu lkn mengine yote anayaignore.

Sijui km kuna mtu anawaza km mimi.
Ashakuwa nyonya damu huyo, anapinga barakoa, anapendekeza kujifukiza.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom