Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.
Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.
Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.
Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.
Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.