Kauli ya upendeleo ya rais Kikwete clouds fm

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.
 
Upendeleo wa kauli kutoka kwa yeyote haufifishi ubora wa radio nyingine wa kweli kama.upo!!!!!!

Acha wasifiwe kama.wanastahili ila THE TRUTH WILL ALWAYS STAND AND PREVAIL
 
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.
Huo ndio ukweli clouds fm inasikilizwa na wengi kuliko kituo kingine chochote hapa TZ.
 
Ila ni kweli, utafiti wa synovate 2012 redio bora ya kibiashara na inayosikilizwa na watu wengi ni cloudsfm.

Acha chuki.

How do we check on the validity and reliability ya mchakato wa kutangaza hivyo na njia zilizotumika!!!!!!?????
Kulikuwa na external moderator wa study yao???!!!
 
kweli hapo ameteleza.Nadhani bado anafikiri Clouds hii ya sasa bado ina influence kwa vijana kama enzi za akina ML Chriss,Bobby,seven,Dj Boggie Master,Amina Chifupa n.k
Clouds sio radio ya burudani tena bali imejaa siasa na kufanya kazi za TBC.
 
Hayo ni maoni yake binafsi kama ambavyo kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake ambayo si lazima yashabihiane na ya mwingine.
 
kweli hapo ameteleza.Nadhani bado anafikiri Clouds hii ya sasa bado ina influence kwa vijana kama enzi za akina ML Chriss,Bobby,seven,Dj Boggie Master,Amina Chifupa n.k
Clouds sio radio ya burudani tena bali imejaa siasa na kufanya kazi za TBC.

Haya watatangaza migomo na maandamano yenu tu na kuhamia marasta katika chama chenu ili mukipende!

Lol! Mumekaa kama wajawazito Wallah
 
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.
CLOUDS FM ni mbadala wa radio UHURU CCM
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom