Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 3,129
- 4,285
Kuna wengi sana hawafanyi Biashara kwa sababu wanadhani kwamba tatizo lao ni kwamba hawana MTAJI. Utamsikia mtu anasema nikipata Mil 10, Au nikipata Mil 100 au nikipata laki 5 nitabadilisha maisha yangu oabisa. Huko ni kutokujua.
Hakuna kitu kama hicho. Hatuhitaji MTAJI mkubwa Bali UNAHITAJI mambo mawili yaani ufahamu kidogo na utayari.
Ifahamu kiasi kidogo unachotaka kufanya.
Pili, uwe na moyo wenye utayari wa kuanza na usiokata tamaa haraka.
kila kitu lazima kianze chini. Mtu anaanza kama mtotot, mti unaanza chini, mnyama hata tembo alikuwa mtoto.
Mbuyu ulikuwa mbegu kwanza.
Kwenye Biashara UNAHITAJI moyo ulio tayari na MTAJI WA 10,000. Wataalam wanasema kama huwezi kubadilisha 10,000 kuwa 100,000 maana yake huwezi kubadilisha milioni mia Moja kuwa kuwa milioni mia mbili.
Kwenye vitabu vitakatifu Kuna mfalme Sulemani aliandika kwenye Mithali 13. 11 kwamba Mali iliyopatikana haraka haraka hupungua, Bali Mali iliyopatikana kidogo kidogo huongezeka. Hii ina maanisha kwamba Kila mtu anatakiwa kuanza chini na siyo juu tena kidogo kidogo.
Uingereza walifanya utafiti wa watu waliopata Bingo ya mabilioni miaka ya nyuma na utafiti ukathibitisha Andiko la Sulemani la kwenye Mithali 13.11.
Ule utafiti uliwafuatilia watu waliopata au kushinda bahati na sibu au Bingo. Baada ya kufanya utafiti walipata matokeo haya 96+3+1=100.
YAANI kati ya watu 100 waliopata fedha za bahati nasibu au Bingo, watu 96 walirudia kwenye umaskini wao baada ya miaka mitatu hadi mitano. Watu watatu wakawa matajiri wa kawaida na Moja akawa tajiri mkubwa sana.
Huu utafiti unathibitisha kwamba Andiko La Sulemani kwenye Mithali 13. 11 na unathibitisha kwamba Changamoto yako siyo MTAJI Bali ufahamu mdogo na Utayari au moyo usiokata tamaa. Lazima uwe na moyo wenye utayari wa kuanza na kuanguka na kuanza na kuanguka na kuanza na kuanguka mpaka ufanikiwe. Haijalishi kama utachukua miezi sita au miaka mitatu.
Wachache sana wako tayari kuingia kwenye hiyo gharama ya kujifunza kidogo na kuwa na moyo usiokata tamaa ndo maana maana matajiri ni wachache. Wengine wanatafuta Hela nyingi bila kujua kwamba Hela nyingi ukipewa Leo ni sawa na kumpeleka mwanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi, akajiunge Chuo kikuu. Ni sawa na kumimina maji ya ndo ya Lita 20 kwenye kikombe Cha chai. Mengi yatamwagika chini. Wakati unaanza chini ufahamu wako pia unaongezeka taratibu kadiri fedha inavyoongezeka. Hiyo ndo siri. Ndo maana Elimu ya darasani siyo kigezo Cha kuwa tajiri.
Leo hii Watanzania wote wakipewa MTAJI wa mil 10, nchi hii itabadilika kwa miaka mitatu tu. Baada ya hapo 96% watarudia kwenye Hali yao. Na Tanzania itarudia kwenye umaskini wake. Yaani huwezi kutangaza mimba Leo na mtoto akazaliwa Leo. UNAHITAJI utayari, ufahamu kidogo na moyo wenye uvumilivu na siyo MTAJI WA Milioni Moja. Hilo halina mjadala.
Hitimisho. Huhitaji MTAJI WA mabilioni Bali UNAHITAJI ufahamu kidogo na moyo wenye utayari na unaovumilia mimba ifikishe miezi 9 au unaovumilia kipindi Cha mpoto ambacho kinaweza kuwa miaka wakati mwingine.
Nakutakia mafanikio mema
Mikael Aweda
0719386100