Amoxlin
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 3,784
- 4,097
Habari wandugu.
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nna kaka yangu hapa jijini Dar es salaam anaejishuhulisha na shuhuli za ujasiriamali na kwa ujumla zinamuingizia kipato kikubwa tu.
Miaka kama mitatu iliyopita alibahatika kupata mchumba ambae alienda mpaka kwao na kufanya taratibu za kimila na hatimae sasa wana mtoto na wanaishi pamoja ila tatizo ni huyu shemeji yetu ni mfujaji wa fedha yani ana matumizi mabaya ya fedha kiasi kwamba hata ukimwachia laki 3 kwa mwezi huku mahitaji makubwa umeshanunua bado atalalamika haitoshi.
Kila wikendi yeye ni kukaribisha marafiki na ndg nyumbani na kutumia pesa atakavyo yani kwa siku moja laki inaisha kwa kualika marafiki na kila kitu kipya kikinunuliwa anawaalika ili waone. Hali hii bro hakuipenda kwani aliamini akioa ndio atapata mtu wa kupanga nae mambo ya maendeleo kumbe ikawa kinyume.
Hali hii ilipelekea misuguano ya muda mrefu mpaka kupelekana kwa wazee na cha kushangaza shemeji alilia kwa uchungu na kudai "nnachojua mimi ni mke wako halali na hata tukiachana tunagawana mali". Kauli hii ilimshtua broo japo hakuonesha kushtuka na alichoamua kufanya ni kwenda nyumbani akachukua tv yake kubwa (hizi model mpya) na kumletea flat ya kawaida 35" kisha akamlipia kodi ya nyumba nzima miezi sita na kumuachia mali zote ndani maana ndicho alichoona cha msingi kwake(hakuchukua chochote zaidi ya kumbadilishia tv).
Brother akaamua kuondoka na kwenda kuweka kambi mahala pengine mbali anapojenga mjengo wake wa kuishi kwakua usafiri wa kwendea kazini anao. Mpaka sasa huwa anaenda tu kusalimia wikend hasa kwa ajili ya kumuona mtoto na kuondoka.
Shemeji amebaki na mali zote, nyumba nzima imefungwa CCTV camera sijui hata kama ana raha na hizo mali alizoachiwa.
Hii iwe funzo kwa wanawake wanaowaza mali kwanza kuliko familia.