Kauli ya shemeji kuhusu kugawana mali imemponza

Amoxlin

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,784
4,089
Habari wandugu.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nna kaka yangu hapa jijini Dar es salaam anaejishuhulisha na shuhuli za ujasiriamali na kwa ujumla zinamuingizia kipato kikubwa tu.

Miaka kama mitatu iliyopita alibahatika kupata mchumba ambae alienda mpaka kwao na kufanya taratibu za kimila na hatimae sasa wana mtoto na wanaishi pamoja ila tatizo ni huyu shemeji yetu ni mfujaji wa fedha yani ana matumizi mabaya ya fedha kiasi kwamba hata ukimwachia laki 3 kwa mwezi huku mahitaji makubwa umeshanunua bado atalalamika haitoshi.

Kila wikendi yeye ni kukaribisha marafiki na ndg nyumbani na kutumia pesa atakavyo yani kwa siku moja laki inaisha kwa kualika marafiki na kila kitu kipya kikinunuliwa anawaalika ili waone. Hali hii bro hakuipenda kwani aliamini akioa ndio atapata mtu wa kupanga nae mambo ya maendeleo kumbe ikawa kinyume.

Hali hii ilipelekea misuguano ya muda mrefu mpaka kupelekana kwa wazee na cha kushangaza shemeji alilia kwa uchungu na kudai "nnachojua mimi ni mke wako halali na hata tukiachana tunagawana mali". Kauli hii ilimshtua broo japo hakuonesha kushtuka na alichoamua kufanya ni kwenda nyumbani akachukua tv yake kubwa (hizi model mpya) na kumletea flat ya kawaida 35" kisha akamlipia kodi ya nyumba nzima miezi sita na kumuachia mali zote ndani maana ndicho alichoona cha msingi kwake(hakuchukua chochote zaidi ya kumbadilishia tv).

Brother akaamua kuondoka na kwenda kuweka kambi mahala pengine mbali anapojenga mjengo wake wa kuishi kwakua usafiri wa kwendea kazini anao. Mpaka sasa huwa anaenda tu kusalimia wikend hasa kwa ajili ya kumuona mtoto na kuondoka.

Shemeji amebaki na mali zote, nyumba nzima imefungwa CCTV camera sijui hata kama ana raha na hizo mali alizoachiwa.

Hii iwe funzo kwa wanawake wanaowaza mali kwanza kuliko familia.
1481201726892.jpg
 
Anapata bahati anaichezea akija kustuka amechelewa.
Amwache akae akili ikimrudi huyo mwanamke atakuta na mwanaume keshapiga hatua na wala hatomtaka tena
 
Bora amani ya moyo kuliko mali inayokuletea maumiv daily.
Ila ww kaka yako ana moyo.. unamuachia mwanamke nyumba hiv hiv... hell no... atakuwa na tatizo
Alifikiria sana akaona mwanamke anaewaza mali kwenye kesi za kijinga mwisho wake si mzuri akaamua kumpisha na hakutaka kugawana.
 
ogopa sana mwanamke mnaekwazana nae kidogo anagusia mgawane mali alihali ni mama wa nyumbani yaani huyo yuo tayari kukuua ili abaki na mali hawa wanawake si wakawaida.
Usishangae kumkuta shemeji yako kaleta bwana kwenye nyumba ya kk yako wakati kaka yako alitoa jasho kuzipata hizo mali yy anaishia kupanga wakati nyumba anayo.
 
Mwanamke mpumbavu huvunja ndoa kwa mikono yake mwenyewe,bora hyo amekunjua makucha yake mapema la sivyo ingemkost hyo bro,ndo maana wanaume wengi huficha mali zao ili wake zao wasijue,

kuishi na Hawa viumbe yahitaji akili na uvumilivu wa hali ya juu .
 
Kuingiza mwanaume itamsumbua sana maana camera zipo kila kona labda asubiri luku iishe asinunue ndo ataweza kufanya huu ushenzi maana camera zitakua off.
 
Ukiacha ajali na maradhi hawa ndio tulioweka roho zetu rehani kwao, akiamua tu muda wowote anakupoteza.
 
Kuingiza mwanaume itamsumbua sana maana camera zipo kila kona labda asubiri luku iishe asinunue ndo ataweza kufanya huu ushenzi maana camera zitakua off.
mkuu kwa kwani akizima main switch jamaa akaingia na ukawa mtindo wake nauhakika hakuna camera chumbani kwa kaka ako.
 
Wanawazaga kugawana mali tu yaani wanawake bwana
Sio wanawake wote wanawaza hivyo.. Km mwanamke alikupendea mali zako lzm atakua hivyo lkn km alikupenda ww km ulivyo hatojali mali maana furaha yake ni mme wake...
Tatizo linalokua naolew na flani kawasbb ana nyumba utafika kwny nyumba lkn huna mapenzi...
Tujifunze kuwapenda watu km walivyo na si mali zao khaaa.
 
Hii inanikumbusha professor mmoja pale mlimani, miaka hiyo alitofautiana na mke wake, mke aliweka ngumu ukiniacha ninaondoka na kila kitu, baba alimwambia isiwe shida, aliondoka na vyeti vyake tu, na huko alipata kazi maisha yakaendelea. Mama ilibidi ahame nyumba za chuo, na furniture zake.
 
Sio wanawake wote wanawaza hivyo.. Km mwanamke alikupendea mali zako lzm atakua hivyo lkn km alikupenda ww km ulivyo hatojali mali maana furaha yake ni mme wake...
Tatizo linalokua naolew na flani kawasbb ana nyumba utafika kwny nyumba lkn huna mapenzi...
Tujifunze kuwapenda watu km walivyo na si mali zao khaaa.
tumechuma wote tugawane
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom