Angalia kauli kama hii iliyotolewa na Mheshimiwa Nape jana (22.08.2013):
"Taasisi zilitakiwa ziandae mabaraza ya katiba ambayo yatatumika kukusanya maoni. Hivyo sijui ni ushamba wa CHADEMA au kutokujua sheria wanafanya mikutano ya hadhara, maoni ya helikopta hayapokelewi kama alivyosema mzee warioba"
Hapa sijui ni nani mshamba kati ya Chadema Na yeye Nape. Kama viongozi wa CCM hawaendi kukusanya maoni-kwa wanachama wake kwa nini Nape atake Chadema nayo isikusanye maoni kwa wanachama?
Na kwa nini yeye Nape aisemee tume? Au yeye ndiye mwenyekiti mwenza wa tume ya kukusanya maoni ya rasimu ya katiba!
Mheshimiwa Nape anaogopa nini Chadema kufanya mikutano yake ya kukusanya maoni kutoka kwa wanachama na wapenzi wake?
Njia ya mikutano ya hadharani ya wanachama na wapenzi ni njia mojawapo tu ambayo chama kimeona inafaa ili kuwashirikisha wanachama na wananchi wengi na ni njia ya kidemokrasia iliyokomaa. Njia nyingine zinazotumika -ni kushirikisha wananchi katika mitandao na Simu kama matangazo mbalimbali yanavyosomeka. Njia hizi ni za uwazi na zinashirikisha watu wengi zaidi bila ubaguzi.
Inaelekea -nguvu ya Chadema ambayo ni nguvu ya wananchi imekuwa tishio kubwa sana kwa Nape na ndio maana uoga unampata anapoona wanachama wengi na wapenzi wanavyojitokeza mikutano ya maoni. Anapata kitu kinaitwa 'Chademaphobia'
Pia Nape anaeleza;
"... taasisi zilitakiwa ziandae mabaraza ya katiba ambayo yatatumika kukusanya maoni..."
Sasa sijui hapa haya mabaraza yatakutanaje bila kuhusisha wananchi!
Hapa swala la kujiuliza -hawa wanachama na wapenzi wa CCM wamekaa lini hadi kupata maoni ya kujadili vikao vya juu vya chama?
Mbona sisi huku mitaani hatujaona vikao! Na kama kulikuwa na vikao labda kwa viongozi wa chama na si kwa wanachama wote.
Hii inaonyesha uongozi wa CCM kutumia ubabe na kudharau wanachama wa ngazi za chini.
Bwana Nape anaendelea; "...Pia wiki hii CCM mbali na vikao vya sekretarieti ya chama,tutakuwa na kamati kuu ya chama itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii baada ya mwenyekiti kurejea kutoka kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais Mugabe.
Baada ya Kamati kuu kutakuwa na vikao vya NEC"-
Hapa Inavyoelekea CCM taifa imekwishaandaa maoni yake bila kushirikisha wananchi.
Sasa kinachofanyika ni uchakachuaji na -kuhalalisha kwa vikao vya juu. Kitu ambacho ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasia ndani ya chama cha mapinduzi.