Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Inasitikisha kuona kwamba michango karibu yote iliyotolewa kwenye blog hii mpaka sasa haisemi ni nini kifanyike ili kuweza kuepukana na janga hili linalonyemelea nchi yetu. Kwa maoni yangu tuwatake chadema wawasilishe kwenye tume leo hii hizo takwimu walizodai wanazo zinazothihilisha kwamba idadi ya kura za urais inayotangazwa na tume hiyo inahitilafiana na iliyoko majimboni. Naamini hatua hiyo inaweza ikatusogeza mbele, kwakuwa jana wakati jaji Makame anazungumza na wahandishi wa habari alisema tume yake ikishapokea takwimu hizo itazishughulikia mara moja. Hiyo ni kauli ya mtu mwenye dhamana kubwa kwa mustakabali wa nchi yetu, kwa hali hiyo hatuna sababu ya kuitilia shaka yeyote. Isipokuwa ushauri wangu kwa mheshimiwa Makame, ni kwamba maadam kuna baadhi ya watu wanaoitilia shaka tume yake, ili kumaliza tatizo ili, wahusika wote na baadhi ya wana harakati washirikishwe kwenye hilo zoezi la kuhakiki takwimu hizo. Bila shaka wewe kama mwana haki unajua fika kuwa haitoshi kutenda haki bali ni muimu pia ionekane kwa kila mtu ya kuwa haki imetendeka.