Elections 2010 kAULI YA MWENYEKITI WA TUME IFANYIWE KAZI HARAKA.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Inasitikisha kuona kwamba michango karibu yote iliyotolewa kwenye blog hii mpaka sasa haisemi ni nini kifanyike ili kuweza kuepukana na janga hili linalonyemelea nchi yetu. Kwa maoni yangu tuwatake chadema wawasilishe kwenye tume leo hii hizo takwimu walizodai wanazo zinazothihilisha kwamba idadi ya kura za urais inayotangazwa na tume hiyo inahitilafiana na iliyoko majimboni. Naamini hatua hiyo inaweza ikatusogeza mbele, kwakuwa jana wakati jaji Makame anazungumza na wahandishi wa habari alisema tume yake ikishapokea takwimu hizo itazishughulikia mara moja. Hiyo ni kauli ya mtu mwenye dhamana kubwa kwa mustakabali wa nchi yetu, kwa hali hiyo hatuna sababu ya kuitilia shaka yeyote. Isipokuwa ushauri wangu kwa mheshimiwa Makame, ni kwamba maadam kuna baadhi ya watu wanaoitilia shaka tume yake, ili kumaliza tatizo ili, wahusika wote na baadhi ya wana harakati washirikishwe kwenye hilo zoezi la kuhakiki takwimu hizo. Bila shaka wewe kama mwana haki unajua fika kuwa haitoshi kutenda haki bali ni muimu pia ionekane kwa kila mtu ya kuwa haki imetendeka.
 
Mkuuu umenena, tafadhali Chadema wahini angalao hata na sample ya malalamiko ili kuzuia kutangaza matokeo.
 
Nafikiri kina Marando na Lissu wamekusikia, najua mwanaharakati Lissu ameshaingia Dar baada ya kazi ngumu aliyoifanya jimboni hatapuuza ushauri huu, nasikia wanataka kutangaza haraka haraka kama walivyofanya Kenya na kumwapisha Kikwete haraka haraka.
 
Ni vizuri wafanye formal complaint badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari tu. Pamoja na kuwa tume watafuata maelekezo ya serikali iliyopo lakini ni afadhali wa lodge hiyo formal complaint ili ipuuzwe kama wafanyavyo kila wakati!!!!!
 
Mkuuu umenena, tafadhali Chadema wahini angalao hata na sample ya malalamiko ili kuzuia kutangaza matokeo.
Kupeleka sample pia kutathibitisha umakini wa chama. But waangalie pia na sheria ya uchaguzi inasemaje
 
Hapa ni kurudia tu uchaguzi kwani ndivyo itakuwa suluhu. Ikiwa waliopiga kura mara mbili wamefungwa miaka. Hawa waliochakachua je? UCHAGUZI urudiwe na upande uliochakachua ukoseshwe nafasi ya kushiriki tena uchaguzi mwingine (CCM) kwa kuwa utakuwa umehukumiwa kwa kosa maana yake disqualified. SLAA atachukua kiulaini sana. Haya ni mawazo yangu anyhow.
 
Jamani,tusifikiri kuwakilisha ushahidi huu ni jambo la kukurupuka.the evidence must be objective and strong.najua chadema wana vichwa na ndio maana hujaona kama wamekurupuka.ushahidi upo ila unahitaji maandalizi ya kuanika ushahidi huo kwa kuonyesha na kuthibitisha mapungufu ambayo ni ya kweli na mtu hawezi kubisha hata kama akiwa jambazi.ukweli ni kwamba subirini ila uhakika ni kuwa chadema wana ushahidi wa kutosha,kinachofanyika sasa hivi ni uandaaji wa makabrasha(paper works) kwa ajili ya ushahidi.
 
GEITA................ 505 ...17,792.. 3,789 ..1,042 ........51 ........18 ...........49......... 791...... 24,037

NYANG'HWALE. 505 ...17,792.. 3,789 ..1,042 ........51 ........18 ...........49......... 791...... 24,037

haya majimbo yamefanana kila kitu .muulize huyo kila imekuwaje mi niko mbali huku usalule sitaweza kufika
 
Natamani Mkuu wetu ajipange nina uhakika Kuna majimbo zaidi ya matano yatarudia kupiga kura this taimu
 
Copy and paste Jamani wanatuchezea akili au wametuloga wa-tz wote kaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Kwa kweli hata ushahidi ukiwasilishwa hautabadili kitu. ila as a matter of formality ni bora uwasilishwe ili wasiseme ushahidi haukuletwa, kwani kesi ya nyani huwezi mpelekea nyani.Then ukikataliwa na tume ambayo ni obvious, CHADEMA wasonge mbele mahakamani kwa matokeo ya ubunge na ya rais kwenye vyombo vya Kimataifa na ikishindikana hapo sasa itakuwa shughuli pevu! Lakini pia pamoja na kuuwasilisha mahakamani CHADEMA wahakikishe coverage ya huo ushahidi iwe kubwa.

CHADEMA wahakikishe wanaoutangaza huu ushahidi na wanatufafanulia vizuri na coverage kubwa, yake iwafikie Watanzania wote haswa wa vijijini ili ukweli na madhambi ya CCM yajulikane! Kila siku wautangaze kwenye vyombo vya habari hata kama itachukua mwaka.

CHADEMA tupeni evidences tupate mzuka! Haki yenu haiwezi dhulumiwa, haki is very expensive! Tutadai kwa njia yoyote ile kama Nyerere alivyodai uhuru wetu, alivyodai ukombozi wa nchi nyingine za Afrika na pia alivyomtandika nduli Iddi Amini! Hakukubali haki idhulumiwe by any means. Watanzania tusikubali na wala tusiwe ma-coward. Tusitishane kila kitu in the name of AMANI ITAVUNJIKA! Ingekuwa hivyo Nyerere asingefanya yote aliyofanya.

Busara itumike (kama CCM wameiba wakiri !) ikishindikana lazima haki ipatikane! CCM watake wasitake haki is a must kama kweli wamefanyauchakachuaji!

CHADEMA kimbilio la wanyonge tupeni mzuka ili tukasake haki yetu!
 
Chadema has nothing to loose by raising this evidence. Watanzania tumeibiwa na tunaomba wasomi wa chadema wafanye kazi ya ziada kuzuia matokeo kutangwazwa. Huyu idd amini kiwete atatumwaga damu.
 
GEITA................ 505 ...17,792.. 3,789 ..1,042 ........51 ........18 ...........49......... 791...... 24,037

NYANG'HWALE. 505 ...17,792.. 3,789 ..1,042 ........51 ........18 ...........49......... 791...... 24,037

haya majimbo yamefanana kila kitu .muulize huyo kila imekuwaje mi niko mbali huku usalule sitaweza kufika

Mzee tuwekee source ya hizo data basi!!!
 
Iyo ndo elimu waliyopata watz copy and paste,walibahatika kusoma komputa wana drag tu! Majimbo yanafanana kila kitu isipokuwa jina tu ! Aibu. Alaf jaman mtu analala polisi kwa kubambwa na kura feki alaf anatangazwa mshindi!
 
Back
Top Bottom