gwamaka aswile
Senior Member
- Mar 26, 2015
- 186
- 106
Ndugu Mhariri, nikiwa mzalendo wa nchi napenda kuwapongeza Watanzania jinsi wanavyoshiriki kwa utulivu kwenye mikutano ya kampeni kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu nchi nzima.Nawapongeza sana kwani wameonesha ukomavu wa kisiasa naamini hata uchaguzi mkuu utafanyika kwa amani na kuwakubali viongozi watakaochaguliwa kihalali katika ngazi ya udiwani, ubunge na rais.
Hata hivyo, napenda kuipinga kauli ya mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wanachi (UKAWA), Edward Lowassa aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni huko Arumeru Mashariki ambapo aliwataka wanachama wao kuhakikisha wanakesha kwenye vituo vya kupigia kura wakizilinda ili zisiibwe.Kauli hiyo ya Lowassa ambayo amekuwa akiitoa mara kwa mara inakwenda kinyume na maagizo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo inawataka watu wote wakishapiga kura warudi majumbani kusubiri matokeo kutangazwa na mamlaka husika ambayo ni tume hiyo.
Binafsi nawashauri wananchi kutosikiliza kauli za mgombea huyo ambaye nina wasiwasi anazitoa kutokana na hofu ya kushindwa katika uchaguzi huo badala yake wafuate maelekezo ya tume kwani kubaki kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kuzilinda ni mwanzo wa kuleta vurugu ambazo
Watanzania hatuzihitaji.