Kauli ya Julius Malema kuhusu kifo cha Malkia Elizabeth inasikitisha na kuhuzunisha

Ungejua madhira ambayo wazungu wametupa na Sasa Hawa vibaraka wao anyway ni neema ya Mungu kwamba Afrika bado inahimili vishindo
 
Wadau hamjamboni nyote?

Alichoandika Malema muda mfupi uliopita kinahuzunisha sana hususani wakati huu wa msiba mzito wa Mkuu wa Taifa la Uingereza na Jumuiya ya Madola

Hebu someni wenyewe alichoandika:

"We do not mourn the death of Elizabeth, because to us her death is a reminder of a very tragic period in this country and Africa's history.... If there is really life and justice after death, may Elizabeth and her ancestors get what they deserve."

Binafsi sijafurahishwa na kauli yake ambayo kimsingi inatakiwa kulaaniwa dunia nzima.

Namuombea kwa Mungu apumzike kwa amani kiongozi wetu wa Jumuiya ya Madola.

Vita amevipiga na mwendo ameumaliza.

View attachment 2350759
Namsifu Malema kwa kusema ukweli,na wengi wenu ukweli hua hampendi kuusikia
 
Nimesema Julius Malema amezaliwa 1981 ila anavyojinadi km kazaliwa 1502

Anatia hasira **** yule
Kumbuka pia SA imepata Uhuru 1994 . Pia malema kuzaliwa 1981 hakumfanyia yeye kutokujua mateso ya Babu na Bibi zake walio fanyiwa na Dictators Royal family ya UK
 
Matatizo ya waafrika yanatokana na waafrika wenyewe kwa kuendekeza unafiki, ubinafsi uliopitiliza, kujikomba, uchawa, uzandiki, uzembe, kutowajibika, tamaa, poor reasoning, poor innovation, na mambo ya hovyo hovyo kama ulozi, kucheza mangoma na kushinda kwenye vilabu vya pombe za kienyeji. Mzungu anafanya ambacho anaona ni sahihi kwake kwa ajili ya maslahi yake na kizazi chake.........poor Malema!​
Umeelewa alichosema malema?
 
Malema yupo sahihi kwa waafrika wenye mtizamo wa kimapinduzi na Waafrika wanafiki wenye kupenda umagharibi au undumilakuwili nao wapo sahihi pia kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth!
 
Mawazo ya sampuli yake ni sawa mtu kuwa nayo, lakini kuyaleta wakati huu ni kutafuta umaarufu usiokuwa na maana, kwangu siku zote kuipiga teke maiti ni upungufu wa akili kwa yule anayeipiga.
Malema anatafuta umaarufu au tayari ni Maarufu 🤣🤣
 

Attachments

  • 20220909_091920.jpg
    20220909_091920.jpg
    157.8 KB · Views: 4
Sawa mkuu je Mr.Malema alitoa tamko kama hilo baada ya King wa wazulu kufariki dunia?,maana naye hakua clean kwenye maisha yake, alitoa kauli iliyosababisha wageni wa kiafrika kuuawa,afriphobia yenye mchanganyiko wa xenophobic, King wa wazulu amehodhi almost ardhi yote ya Ile province but malema amefyata mkia wake, reason wazulu sio target rahisi ila queens!,malema haishi manzese au tandale au kinondoni shamba, anapiga kelele na mwisho wa siku anakimbilia kwenye makazi ya wazungu yaliyo chini ya opposition party, DA maana kuko smart na safe, why assisting kule seshogo, alex?
Hakuna mwanasiasa msafi kama pamba, ila angalau watu 'vocal' wa aina hiyo ni muhimu sana. Hapa amezungumzia madhila waliyoyapata chini ya uangalizi wa Malkia na si habari ya Wazulu. Halafu mkuu unataka Kiongozi aishi 'Manzese' ya South Afrika! ili aonekane anawajali Watu. Lakini kuhusu wageni kushambuliwa Malema alitoa statement ya kulaani hilo tena waziwazi

Malema is well-known for his controversial politics; however, the EFF commander preached a simple message of love and unity when it came to this difficult topic. The EFF politician affectionately known as ‘Juju’ drove one particular point home when it came to xenophobia in SA: “Africa is for all of us…”
 
Wakoloni walikuwa wabaya, lakini tawala nyingi za Afrika, ni afadhali ya wakoloni.

Leo hii, kimbilio la Waafrika wanaodhulumiwa na watawala, imekuwa kwa wakoloni. Tukitaka kujenga barabara, madarasa, vituo vya afya, kwa kwenda kuomba ni kwa wakoloni. Kule Seychelles, kuna kisiwa, wananchi wake wamegoma kuwa taifa huru, wameamua kuwa sehemu ya Ufaransa.

Afrika Kusini iliyokaliwa na makaburu kwa miaka mingi ndiyo nchi yenye uchumi mzuri kuliko mataifa karibia yote ya Afrika.

Kumlaani marehemu, ambaye mpaka kifo chake, serikali imeendelea kuyasaidia makoloni yake, siyo uungwana. Kama tusingekuwa wanafiki, tulistahili kuwalaani watawala wetu, waafrika wenzetu, ambao wanajiona ni bora zaidi kuliko wananchi wenzao, hasa wale wenye fikra tofauti na zao.

Queen Elizabeth, na marehemu wengine wote, Mungu mwenye huruma, kwa yale mazuri waliyoyafanya kwaajili ya hinadamu wenzao, awajalie pumziko jema na furaha ya milele. Sote tu mavumbi, mavumbini tutarudi.
Ni hao hao wazungu unao wasifia ndio walio walea viongozi wetu unao waponda,tunayo ita misaada ni zao la raslimali zetu walizo ingia mikataba na viongozi walio wasimika. Hao hao wazungu ndio wanatufitinisha na neno lao "demokrasia"... Ni wanafiki kwa maslahi yao.
Kama tunajiamini na kuchagua mema kutoka kwa wazungu, basi,tujichagulie viongozi wetu kwa mfumo wa asili yetu,inawezekana kabisa matokeo yasipite kwenye wizi.
 
Hakuna mwanasiasa msafi kama pamba, ila angalau watu 'vocal' wa aina hiyo ni muhimu sana. Hapa amezungumzia madhila waliyoyapata chini ya uangalizi wa Malkia na si habari ya Wazulu. Halafu mkuu unataka Kiongozi aishi 'Manzese' ya South Afrika! ili aonekane anawajali Watu. Lakini kuhusu wageni kushambuliwa Malema alitoa statement ya kulaani hilo tena waziwazi

Malema is well-known for his controversial politics; however, the EFF commander preached a simple message of love and unity when it came to this difficult topic. The EFF politician affectionately known as ‘Juju’ drove one particular point home when it came to xenophobia in SA: “Africa is for all of us…”
Kwangu ni mnafiki na hana tofauti kabisa na politicians wengi wa hapa Africa, anajifanya yupo very vocal kumbe ni kwa ajili ya maslahi yake binafsi, anazungumzia demokrasi wakati ndani ya chama chake anakiongoza kwa iron rule, kuna baadhi ya municipalities alishinda why ameogopa kuziongoza?kulalama on the side ni tofauti kabisa na kuwa in the mix, EFF hawana respect na angalia walivyoligeuza bunge la SA kuwa kama kijiwe cha kahawa, EFF hawana uwezo wa ku uphold rule of laws, hata mimi kama unaingia kwangu kwa kuruka dirishani wakati mlango upo definitely Nita deal na wewe maana ur undermine me,mfano wa malema kuishi na watu anaowapigania nimeutoa ili ujue unafiki wake, bankrollers wake ni crocodiles 🐊, mchana anajifanya anawachana giza likings anaingia kwa kunyenyekea kwenye security estates zao
 
Back
Top Bottom