KAULI ya CHADEMA juu ya watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM


Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Points
1,500
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 1,500
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Kwa niaba ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) natoa mwito kwa watumishi wa umma kote nchini kupuuza maagizo yaliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ya kuwalazimisha kuhudhuria mikutano ya CCM na kutoa taarifa za kiserikali kama yalivyotolewa katika baadhi redio na televisheni tarehe 2 Disemba 2012 na kunukuliwa na magazeti mbalimbali tarehe 3 Disemba 2012.

Pia namshauri Rais Jakaya Kikwete kwa mamlaka yake ya mkuu wa nchi na kiongozi wa Serikali ambaye ndiye mwajiri wa watumishi wa umma wenye kulipwa mishahara kwa kodi za wananchi wasio na vyama na ambao ni wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa kukemea kauli kama hizo zilizo kinyume na haki za kikatiba, misingi ya utawala bora, sheria na waraka wa utumishi wa umma.

Aidha, CCM kutaka kujitwalia mamlaka ya Serikali kutoa maagizo kwa watumishi wa umma badala ya vyombo vya usimamizi kwa niaba ya wananchi kama bunge, baraza la mawaziri, mabaraza ya madiwani, kamati za ushauri za wilaya, kamati za ushauri za mikoa, bodi za mashirika mbalimbali na mamlaka nyingine ambapo wapo viongozi waliotokana na chama hicho ni ishara ya udhaifu na uzembe wa viongozi wanaotokana na chama hicho katika mikutano ya vyombo hivyo.

Maagizo hayo ya CCM yanazidi kuongeza sababu za wananchi kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuunga mkono CHADEMA ikiwa ndicho chama mbadala chenye kuweza kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya taifa.

Maagizo haya ya CCM yanaashiria ‘ulegelege’ wa chama hicho na kuzidiwa na vuguvugu la mabadiliko linaloongozwa na CHADEMA na madai ya uwajibikaji toka kwa umma kwa kiwango cha kutaka kuirejesha nchi katika maagizo yamfumo wa siasa wa chama kimoja ambapo kundi lote la watumishi wa serikali na vyombo vyake walikuwa wakilazimishwa kushiriki katika shughuli za CCM wakati ambapo kwa sasa watumishi hao wengine ni wanachama wa CHADEMA na wapo ambao sio wanachama wa chama chochote cha siasa.

Rais Kikwete aikumbushe CCM kuwa mapendekezo ya Tume ya Nyalali ya mwaka 1991 na marekebisho ya Katiba ya mwaka 1992 kuingia katika mfumo wa vyama vingi na marekebisho ya sheria yaliyofuata yameweka uhuru wa watumishi wa umma katika kujiunga na vyama vya siasa (isipokuwa watumishi wa kada maalum) na mipaka ya mahusiano kati ya kazi zao za kiserikali na shughuli za vyama vya siasa kikiwemo chama kinachotawala.

Naitaka CCM izingatie kuwa utumishi wa umma katika nchi yetu unaongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na marekebisho yake. Kifungu cha 4(1) cha Sheria hiyo kinampa mamlaka Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi kutoa waraka kuhusu taratibu mbalimbali za utumishi wa umma.

Chini ya Mamlaka hayo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Martem Y.C. Lumbanga tarehe 26 Juni, 2000 alitoa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma na. 1 wa mwaka 2000 wenye kumb. Na. SHC/C.180/2/113 uliohusu maadili ya Watumishi wa Umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Waraka huo unawataka watumishi wa umma kutekeleza wajibu wao wa utumishi bila kufanya upendeleo wala ubaguzi wa chama chochote cha siasa. Waraka huo unawakataza watumishi wa umma kuzungumza na kutoa taarifa kwenye mikutano ya vyama vya siasa na haujatoa ruhusa kwa watumishi hao kuzungumza katika mikutano ya CCM pekee; hivyo maagizo yaliyotolewa na chama hicho ni kinyume maagizo ya Serikali inayoongozwa na chama hicho hicho.

Ikiwa Rais Kikwete atahalalisha maagizo hayo haramu ya CCM, watumishi wa umma watawajibika pia kuitwa na kutoa taarifa kwenye mikutano ya CHADEMA na vyama vingine vya upinzani nchini.


Imetolewa na:

John Mnyika (Mb)

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

04/12/2012

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Ps

Sheria ya 1989 ilifutwa na Sheria ya 2002 na marekebisho yake ya mwaka 2007. Na kanuni za mwaka 1994 zilifutwa na kanuni za mwaka 2009. Hata hivyo hoja ya Waraka wa Watumishi wa Umma katika mfumo wa vyama vingi inabakia pale pale.
 
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Messages
3,582
Points
2,000
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2012
3,582 2,000
Nashukuru kuliona hili
 
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
8,181
Points
2,000
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
8,181 2,000
Imetulia hii.. Naunga mkono...
 
D

diwan

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
309
Points
195
D

diwan

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
309 195
Well don, your in my shoes.
 
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
3,519
Points
2,000
Age
38
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
3,519 2,000
Kanuni za kudumu za utumishi wa 1994 zilifutwa na kanuni mpya za utumishi wa umma toleo la 3 la mwaka 2009.
 
RealMan

RealMan

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
2,367
Points
1,250
RealMan

RealMan

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
2,367 1,250
Siku Kikwete anahutubia sijui atamwita nani atoe maelezo kwa wananchi kwa nini wauza unga hawajakamatwa na orodha serikalini ipo!!!

Yaani CCM ni full komedi.....
 
UKI

UKI

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Messages
697
Points
0
UKI

UKI

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2012
697 0
kweli ccm inapigwa kote kote waje na hoja za msingi kwa kujibu hizo shutuma wasije na hoja za kidhaifu kuwa eti viongozi wa chadema wanataka sifa, wajibu hizo hoja kwa msingi wa maelezo ya mnyika, big up chadema,
 
Nduka

Nduka

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2008
Messages
8,521
Points
2,000
Nduka

Nduka

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2008
8,521 2,000
Njia rahisi ni kwa CDM nao kuita mateja walioshiriki kwenye maandamano kuwaelezea wananchi utendaji wa kazi za chama katika kuvuruga amani nchini.
 
commited

commited

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,617
Points
1,195
Age
28
commited

commited

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,617 1,195
98% ya viongozi wa juu kabisa wa sisiemu ni wagonjwa wa akili, roho na mwili, wakiongozwa na jk.... Muwasamehe bure tu. Hawajui wanayoongea, wapo pale kwa jeuri ya dola tu na kunufaisha matumbo yao, wala si kuwapigania watanzania, furaha yao ni watanzania tuzidi kuwa na dhiki na umaskini.

chini ya sisiemu maendeleo, uadilifu na uwajibikaji tusahau.
 
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
15,280
Points
2,000
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2012
15,280 2,000


Asante sana Kamanda!!!!
 
Ntale Wi Isumbi

Ntale Wi Isumbi

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
479
Points
170
Ntale Wi Isumbi

Ntale Wi Isumbi

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
479 170
Naunga mkono hoja.
 
Ntale Wi Isumbi

Ntale Wi Isumbi

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
479
Points
170
Ntale Wi Isumbi

Ntale Wi Isumbi

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
479 170
Njia rahisi ni kwa CDM nao kuita mateja walioshiriki kwenye maandamano kuwaelezea wananchi utendaji wa kazi za chama katika kuvuruga amani nchini.
Kazi ya kichwa sio kufugia nywele tu, naomba kifanye kazi ya kufikiri!!!!
 
Tukundane

Tukundane

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Messages
9,699
Points
2,000
Age
53
Tukundane

Tukundane

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2012
9,699 2,000
Hii ni dalili ya ccm kushindwa kuhimili vishindo vya wapinzani.wameshindwa kurudisha mfumo wa chama kimoja.sasa wanataka kuurudisha kwa kuzunguka.
 
E

eddgabby

New Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
2
Points
0
E

eddgabby

New Member
Joined Oct 24, 2012
2 0
wagonjwa hutawajua tu kwa kusoma coments zao.
Njia rahisi ni kwa CDM nao kuita mateja walioshiriki kwenye maandamano kuwaelezea wananchi utendaji wa kazi za chama katika kuvuruga amani nchini.
 
yegella

yegella

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
3,115
Points
1,250
yegella

yegella

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
3,115 1,250
Njia rahisi ni kwa CDM nao kuita mateja walioshiriki kwenye maandamano kuwaelezea wananchi utendaji wa kazi za chama katika kuvuruga amani nchini.
kodi yetu ndiyo inayokupa kiburu mpaka kuwatolea watanzania maneno ya kejeri namna hii..
 
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Points
2,000
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 2,000
Safi sana Mnyika.Huyu ndiye mfano wa vijana wanaojua wanafanya nini.Umempa somo la kutosha Nape.
 

Forum statistics

Threads 1,285,560
Members 494,675
Posts 30,866,841
Top