Naona hoja zimejaa ushabiki, vijembe, kuna wanaotukana nadhani hapa haitatusaidia kwa lolote kwanza nijadili maada hii kama ninavyoona inafaa; at leats we can discuss issue in other directions, siyo swala la Volt, watt, ampere!!
This is the fact!
TANESCO
Tanesco hawataweza kutolaumiwa katika saga loote hili la huu mradi;
1. Tanesco walitakiwa wafanye EIA ambayo ina comprise technical and social risk, katika hiyo EIA walitakiwa wafanye na risk analysis ya mradi kuanzia kuanza mpaka kuisha.However risk assessment unaweza ukaifanya kama separate study
Ninaposema risk assessment inayo-comprise social interest ni kuwashirisha raia wa hayo maeneo kuhusiana na mradi huo, ninachoandika hapa ni standard, na Tanesco wanalijua hilo na ndicho kilichopelekea wawe wapole muda wote huu.
Kilichotakiwakufanyika ni simple wakubwa; iteni watu aelezeni kuna mradi kwa ajili ya manufaa yao na taifa na yao, ndio ulikuwa muda mzuri wa kujadili issue zote hizi zilizotokea sasa. mkikubaliana wawakilishi wanaandika majina yao na kupiga sign ku-endorse mradi.
Mimi kama project manager ninapokuwa ninapanga schedule yangu ya kazi, naangalia time, qality ya kazi na gharama. kwa sababu nimeshafanya risk assessment nina hakika project yangu itaisha kama nilivyopanga kwa bajeti niliyopanga. This is taught everywhere in project management!
Risk assessment inamwokoa professional kukutana na watu kama Kakobe ambaye yuko wrong, haelewi na njia pekee ni kukutana nao mapema. kuna mtu atasema mbona kuna miradi haikufanyika bila EIA, that was old time!
Inakuwa kichekesho kutetea ujinga huu wa Tanesco ambao umetugharimu sisi wooote shilingi millioni 25!!! still mtu anapiga kelele kumtukana Kakobe, where is our thinking, nimemwajiri mtu ameniletea hasara ya milioni 25 ambayo angeikwepa kama angefuata utaratibu unaotakiwa unamlaumu mtu wa mbali kabisa??
ushiriki wa raia
Ushiriki wa raia ni lazima kwa standard za sasa za WB, IMF na first world, imegundulika kuna miradi mingine haiisaidii jamii bali wahusika fulani, haya yametokea sana UK , kwenye nuclear waste, migodi, food waste, toxic waste n.k, Tanzania tuna mradi wa mabati ya asbestos ambao ulifungwa kwa sababu raia wa hayo maeneo walipata na wanaendelea kupata cancer hata leo hii. Project in now a days lazima ufanye risk analysis ' tuache fikra za kizamani za zidumu fikra sahihi za serikali'' wangefanya the same approach kwa Asbestos watu wasingepata makansa. Leo hii tuna minara ya simu imezagaa kila kona nani alifanya EIA? nchi za asia hivi sasa hawataki kuona mnara karibu na shule za watoto n.k . why??
Kauna ushahidi approach hii ya serikali/Tanesco kutoshirkisha raia ndio iliyofanya watu wafukiwe migodini na miradi ya migodi kuanzishwa pasipo ushiriki wa raia. Hii imetokea sehemu nyingi duniani
KAKOBE
Nilipopata taarifa kwa mara ya kwanza nilikusifia sana kwa sababu umeonyesha njia ya wataalamu, kufanya kazi zao kitaalamu kadiri procedures na standard zinavyosema. Nilifurahi sana siyo kukutetea wewe bali at least watendaji wa serikali watajua nini kinatakiwa kifanyikekwenye project zingine.
I think by your capacity and status serikali ilikaa chini na kukusikiliza, hilo pekee lina -i-credit serikali kuwa inasikiliza watu kama wewe. Serikali wakati inaongea na wewe ilijishusha na kukusikiliza, hata kupelekea kufanya vikao mpaka jumamosi.
Mkutano wako wa Jumamosi ulipokataa tena maoni ya wataalamu wa BICO, wakiongozwa na Kyaruzi professor wa umeme nilikushangaa sana. Nilidhani kwako wewe ungekuwa wakati mzuri wa kuandikishiana mkataba na Taneco kuwa if anything happen Tanesco watakuwa liable. Siyo kubisha tu kama mtu ambaye hana sense sawa sawa au hawezi kufikia kuelewana.
Hatua hii ya ubishi siyo tu kuwa ime-kudevalue lakini pia imenipa picha na kunikumbusha mengi sana kuhusu wewe na kanisa kwa ujumla. Ubishi, ujuaji, kutokuamini siyo tabia za upendo kama ambayo wakorintho wa 1 sura ya 13 inavyosema. It was good time and only chance to show and rise up again and show the public you did that for good reasons. However now it will be difficult to suggest that, askofu kama wewe aispofikia hatu ya kusema nimekubali, je waumini wako?/ wanaiga nini??
Ubishi wako kutokana na kutokujua haukuwa na matatizo kamwe, ila ubishi wako baada ya kujua ndiyo umeleta maswali mengi na jina la Yesu kuchafuliwa.