Kauli Cheshi za KAKOBE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli Cheshi za KAKOBE

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiranja Mkuu, Mar 9, 2010.

 1. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  • Umeme wa |TANESCO HAUTAWAKA.
  • Mrema atakuwa Raisi wa Tanzania.
  Haya sisi yetu masikio.
  Mwaka huu tutasikia mengi.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,112
  Likes Received: 2,412
  Trophy Points: 280
  Maaskofu kama hawa wanautia aibu ukristo!
   
 3. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Huu ni ushirikina!
   
 4. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,849
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Huyu naye sio wa kumsikiliza. Amewalaza sana waumini pale nje bila malipo
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Watu wamekesha kwa miezi miwili mizima na mwisho wa siku umeme unapita.
  Angekuwa na macho ya kiroho, angeona kuwa kamwe huwezi kushindana na serikali.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  tehe tehe tehe.
  ngoja waje wenyewe watatetea kwamba umeme hautawaka kweli.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,012
  Likes Received: 37,313
  Trophy Points: 280
  Kafananisha makaburi ya lringa na kanisa lake.
  Jamani swali langu ni hili:
  hivi Kakobe anamwamini Yesu au mizimu ya lringa?
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,771
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  Mkuu hivi huyu kweli ni ASKOFU katika mantiki ya kiaskofu? nadhani tuanzie hapo kabla hata hatujafika hilo suala la kutia aibu ukristo..

  mi wala sikumshangaa alivodai eti ni njama za baadhi ya watu ambao hawampendi yeye na kanisa lake! alishindwa nini kuzima njama hizo kama anatenda miujiza pale?
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,012
  Likes Received: 37,313
  Trophy Points: 280
  Nasikia jamaa alikuwa myuzisheni hapo longtime.
  Kisha baada ya hapo akaenda Nigeria kusomea elimu dunia,
  Hajawahi kusomea Theolojia.
  Leo ndio amekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,012
  Likes Received: 37,313
  Trophy Points: 280
  SIKU moja baada ya serikali kuamua kupitisha waya za umeme wa kilovoti 132 karibu na Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zachary Kakobe, amesema anaamini umeme hautawaka kwa nguvu ya Mungu kwa vile hakuna nguvu zitakazopita hapo.
  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Askofu Kakobe alisema ameshangazwa na kauli ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuutangazia umma kuwa ameridhia umeme huo kupitishwa kwenye kanisa hilo.
  “Nakwambia hata wakipitisha umeme huu hapa… hautawaka kwa vile nguvu ya Mungu itashinda nguvu ya umeme lakini kibaya nimesikitishwa na Waziri Ngeleja kuutangazia umma eti nimekubali umeme upitishwe hapa, nasema siyo kweli jamani,” alisema Askofu Kakobe.
  Alisema yeye mwenyewe hana uwezo wa kukataa maamuzi yaliyofikiwa na serikali ndiyo maana hadi jana hakukuwa na muumini hata mmoja ambaye alikuwa akililinda eneo hilo.
  “Huu ni uonevu wa hali ya juu, sijakubaliana na maamuzi hayo kwa kuwa vipimo vyote vilivyotolewa havikuwa vya kweli na kama ningekuwa nimeafiki basi ile siku Waziri Ngeleja alivyotoa taarifa yake ningeshiriki katika hicho kikao,” alisema Askofu Kakobe.
  Alisema hivi sasa amegundua hawatakiwi kupinga upitishaji wa umeme huo kimwili kama walivyokuwa wamefanya huko siku za nyuma bali ni kutakiwa kukaa katika maombi.
  Alisema ni hatari kukatalia utawala ambao hauna hofu ya Mungu kwa kuwa hauwezi kudumu na mara nyingi unakosa kutenda haki, hivyo jamii nzima inatakiwa kuondoa tofauti zao na kuwa na sauti moja ili kukemea unyanyasaji unaofanywa na utawala.
  Alisema hivi sasa amepata taarifa za uhakika kuwa baadhi ya watu wamepewa taarifa kuwa wanatakiwa kuhama katika eneo hilo kupisha upitishaji wa nguvu hiyo ya umeme kitendo ambacho kinampa ishara kuwa kuna mpango wa kanisa lake kuvunjwa.
  “Kwa sasa jamii haiwezi kunielewa, lakini ukweli ni kuwa serikali hii imedhamiria kuvunja maeneo hayo kwa kuwa hakuna mradi kama huu unaofanyika ukaruhusu jirani kuwa na vizuizi kama majengo” alisema Askofu Kakobe.
  Alisema amesikitishwa na Waziri Ngeleja kutoa maelezo kuwa hata kituo cha televisheni ambacho anatarajia kuanzisha hakitaweza kukidhi vigezo.
  “Unawezaje kusema eti hatuwezi kukidhi vigezo vya kuomba usajili, inawezekana labda wameshafikia hatua ya kutaka kutunyima kibali maana wanatoa kauli hizo ambazo zinaweza kuwa ni dalili njema,” alisema Askofu Kakobe.
  Askofu Kakobe alipingana na madai yaliyotolewa na Mshauri Mtaalam wa Kampuni ya BICO, kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linatakiwa kuepukana na kona kali kwenye waya na kutounganisha sehemu yoyote kati ya nguzo namba 18 na 19.
  Akitolea mfano, alisema kuna maeneo mbambali yaliyopitishiwa umeme kama huo, ingawa unatofautiana kwa ukubwa wake, ambao umewekwa kona ikiwemo maeneo ya Mwenge na katika kijiji cha Tanangozi kilichoko Iringa karibu na makaburi ya Kiyeyeu.
  “Huu ni uwongo! Wanafikiri hatuna uelewa wa masuala hayo ya umeme? Si kweli kuwa kunaweza kutokea madhara iwapo kutawekwa kona kama wangepitisha upande wa pili; mbona karibu na kaburi la Kiyeyeu kule Iringa nguzo zimevushwa upande wa pili?” alihoji Askofu Kakobe.
  Juzi Waziri Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari kuwa mgogoro uliodumu kwa siku 77 kati ya serikali na Askofu Kakobe umemaliza kwa askofu huyu kukubali umeme huo kupitishwa eneo la kanisa lake.  SORCE Tanzania Daima.
   
 11. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #11
  Mar 9, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu wanaJF. Kakobe ni Mtumishi wa Mungu na ukweli. Imani yake inamshawishi kuamini kuwa Umeme hautawaka.
  Mfano Mdogo.
  Katika kitabu Cha Daniel kwa wale wanaosoma bibilia.(Dan 3:16-18)
  16The three men replied, " Your Majesty, we don't need to defend ourselves. 17The God we worship can save us from you and your flaming furnace. 18But even if he doesn't, we still won't worship your gods and the gold statue you have set up."

  Tunaona mtumishi wa Mungu daniel Anaamini kuwa Hata wakitupwa kwenye Tanuru la moto Mungu wanaye Mwabudu atawaokoa. Na hatakama hatawaokoa hawawezi kuabudu Miungu wengine

  Ninachoomba. Just dont Talk negative on this guy. he had a point to prove! na ndio maana alikua anakataa umeme upite.
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Zahoro bana, an'chekesha kweikwei.
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  baada ya miezi mitatu ya mgomo..............!
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  My friend, Kakobe and his follower just did worship the so called gods..........Daniel said, and I qoute "Your Majesty, we don't need to defend ourselves. 17The God we worship can save us from you and your flaming furnace"

  Kakobe defended himself, he used his followers to fight Tanesco guys from erecting the poles.

  Got that?!!! Tofautisheni kati ya matendo ya kiuanaharakati na will of God.
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Mkuu ule haukuwa mgomo, nafikiri yale yalikuwa maonyesho ya utamaduni wa ufinyu wa fikra.
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,771
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280

  hapa hatuongei negative, tunaongea facts

  mwanzoni, alisema kuwa vipimo vimekosea, kwamba tanesco wanadanganya umbali, lakini ikaonekana baadaye kuwa yeye ndo alikuwa anasema uongo!

  sasa Daniel and co hawakusema uongo mbele ya mfalme Nebukadreza! wale walikuwa waadilifu wa kweli!

  Niambie Kakobe je anafananishwaje na wale vijana watatu? tuache ushabiki jamani
   
 17. d

  damn JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Let me be neutral, ningependa kujua ni kwa nini umeme wa 132kv unaotoka mtera na kidatu umetengewa njia yake na karibu yake hairuhusiwi kujengwa makazi ya watu, lakini huu wa 132kv kutoka ubungo (kama kweli ni 132kv) unapitishwa karibu na makazi ya watu? au si 132kv? na kama ni 132kv hamwoni kuwa serikali inawatendea vibaya wakazi wote katika barabara hiyo na wala si kakobe na waumini wake ambao kwanza hawaishi eneo hilo?
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,771
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  Yaani pamoja na kusababisha public unrest, kujaribu kuwajeruhi wale wachina sijui wajapani, etc

  wale walitakiwa wakamatwe mara moja washitakiwe kwa uzururaji bana lol
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,565
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nilitoa angalizo watu waache Kujadili maneno ya Kakobe wala Tanesco,

  Nikauliza Swali kwa Mashabiki wa Kakobe na Mashabiki wa Tanesco kwamba nani alikuwa sahihi Kakobe Kukataa Umeme au Tanesco kupitisha Umeme, nikatoa na Simple Reasono kwamba Umeme wa Tanesco ambao ni 50Hz hauwezi kuingilia TV ambazo ziko katika 170-240MHz lakini Mashabiki hawakuelewa! Wakaendelea kushabikia zaidi kuliko kuangalia Facts kwamba kunazia Ubungo mpaka Mwenge kuna Nyumba za Waislam, wakristo, Wapagan nk sasa iweje Wakristo Pekee ndiyo tukaangwe kwa Mujibu wa Kakobe?

  Jambo la Msingi ninalomshauri Askofu ni Kwamba akae Chini, atafakari ni nini Wajibu wake kama Mchunga Kondoo wa Bwana, yeye ni mchungaji, hawezi kuwa yeye ndiyo Mtaalamu, yeye ndiyo Mwanasiasa! Hata Yesu alisema Ya Kaisar Mwacheni Kaisar, Ya Mungu mepeni Mungu!

  Aachane na Waandishi wa Habari, afanye kazi ambayo Mungu amemuitia, Achunge Kondoo wa Bwana na Wanasiasa awaache wafanye kazi zao

  Asiwe Mbinafsi, kama anaamua kupambana na Wanasiasa isiwe tu katika Jambo linalomhusu yeye peke yake bali hata yale yanayowahusu Watanzania Wote!

  Huo ni ushauri wangu tu
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,565
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Unafahamu unachozungumza?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...