Uchaguzi 2020 Katika Uchaguzi wa Oktoba 28, mpinzani mkubwa wa CCM sio Vyama vya Upinzani

sopinta

Member
May 28, 2020
46
93
Katika uchaguzi wa oktoba 28, mpinzani mkubwa wa CCM sio vyama vya upinzania , yani hii ipo wazi kabisa , hawa wapinzani mfano wakina Lissu sio Membe , sijui Zitto hawa wote sio wapinzani wa CCM , ni vyema ikafhamika tu kuwa mpinzani mkubwa wa CCM ni mtanzania kwa maana ya mwananchi , kiutamaduni watanzania ni mabingwa wa unafiki yaani mtanzania anaweza kuwa anacheka na wewe , anakupepea , anakubeba , anakusifia kuwa umeboresha mambo mengi lakini jitahidi sana uipasue akili yake na mawazo yake laiti mtu ukaweza kuingia katika ubongo wa mtanzania unaweza kufa au zimia kabla ya siku

Watanzania wanatabia halisi ya kitanzania ambayo viongozi wa dini wanajaribu kuikemea sana nayo ni kulipiza kisasi , watanzania kuanzia mwaka 2015 wengi sana wameumia kwa kila mmoja na staili yake , wapo waliovunjiwa nyumba kwa kusema tunatanua barabara , wapo waliofanya kazi zaidi ya miaka 30 baadae wakaambiwa kuwa wanavyeti feki hata pensheni zao zikachukuliwa na tukumbuke hawa wote wana watu wanaowafuata na wengine walikuwa wanawategemea sasa tengeneza picha hapo pia wapo wafanya biashara walifungiwa na kubambikiwa kesi na msururu wa kodi mpaka biasha zikafa , wapo watanzania ambao ndugu zao wapo Keko kwa kubambikiwa kesi , kuna watu hawa wanaitwa watanzania ambao ni watumishi wa umma yaani hawa ukiwaona kama vile hawana mpango na siasa ila akilini mwao mungu ndio anajua hasira walizonazo sijui ni za wapi

Yani niseme tu utafiti mdogo tu niliofanya mpinzania wa CCM kwa siasa za uchaguzi huu wa 2020 kuanzia ngazi chini mpaka juu sio vyama vya upinzania ni watanzania wenyewe. Sina maslahi na chama chochote cha kisiasa ila uhalisia unaonekana ni tofauti na mioyo ya watu.
 
Uchaguzi huru na wa haki ukifanyika ccm haiwezi kubaki madarakani, na wanalijua jambo hili vizuri na ndio maana unaona figisu figisu zinazoendelea.
 
Wapo walioumia kwa hayo uliyosema na pia wapo waliofaidika na hawajayasema tathimini ya ya haya yote ni tareh 28 October
 
Hapo watawala huwa wana kosea sana.Wanaona wapinzani kwa majina ya vyama vyao badala yashida zao wanazoona zinasababishwa na watawala.Hata miongoni mwa wenye nguo za kijani kuna wapinzani wabaya kuliko wenye nguo za blue na zambarau. Advantage ya kutumia dola haiwezi kuwa forever kwa kuwahata kuko kwa watumishi wadolawapinzani wako piait is a matter of time tu. Kwene hili somo kubwa this timelinaweza kutoka Zanzibar.
 
Back
Top Bottom