Katika Picha: Maandamano ya wanahabari Leo

Status
Not open for further replies.
2790.png

Khaa! Khaa! Khaa! haaa!!!
 
Hapa kuna vitu viwili vinakinzana.

Kuna watu wenye standards za Tanzania, ambapo waandishi wanaweza kusema "hatuwezi kumuandika Mkuchika by any means" halafu kesho yake wakamuandika.

Halafu kuna watu wanaotaka umakini na kila mtu kuheshimu maneno yake na ahadi zake.

Ukichagua lile la kwanza halafu kesho ukaanza kupiga kelele ufisadi unachekesha, ufisadi unaanza kidogo hivi hivi, mara umeona mikamera ukataka kuleta dramatics bila kupima maneno, ukatoa mitamko iliyokuzidi kimo ambayo kesho huwezi kuiheshimu.Kesho utapewa ofisi kwa sababu ya maneno yako ya kupinga rushwa "by any means" halafu utayasahau kama ulivyosahau kwamba "by any means" hatutam cover Mkuchika.

Halafu kuna watu humu wanaleta mambo ya "Us versus them", kwamba if you are against Mkuchika you must be with the journalist, and if you criticize the journalist you must be with Mkuchika, sorta like George Bush in his doctrine of "If you are not with us you are with the terrorist" .Yaani upumbavu huu hauamini mtu assertive anaweza kukaa na kuona makosa pande zote mbili. Kwamba kwa kuwa ni waandishi wa habari na wanaandika kuhusu ufisadi wasisemwe ni ujuha wa hali ya juu, kama wanachemka wanasemwa vizuri tu.

safi na kweli tupu!! ndio maana mara nyingine ni vyema kukaa pembeni na kuwa mtazamaji tu, maana ukitoa maoni yako, basi inakuwa kama unanunua malumbano/majigomvi yaso na msingi!!

hao wahariri mdebwedo, wame-declare kitu ambacho wameshindwa kukitekeleza....matusi na kashfa pembeni, lakini ukweli ndio huo!!
 
Yaani upumbavu huu hauamini mtu assertive anaweza kukaa na kuona makosa pande zote mbili.

Kwamba kwa kuwa ni waandishi wa habari na wanaandika kuhusu ufisadi wasisemwe ni ujuha wa hali ya juu, kama wanachemka wanasemwa vizuri tu.

Mkuu Max Melo, leo nitakuwa mstaarabu kidogo hii lugha inakubalika ili tujibu inavyotakiwa, maana siku zote tunatakiwa kuongea na ushahidi, dataz au facts, ushahidi wangu ni huu hapa chini kwamba nimetukanwa (tusi) au Bwa! ha! ha! ha!?:-

Maxence Melo :JF Founder Join Date: Fri Oct 2006
Location: Dar es Salaam

Angalizo muhimu...

--------------------------------------------------------------------------------

Wakuu heshima zenu,

Kumradhi kwamba sijakuwepo hapa muda mrefu, nilikuwa na mzunguko mrefu nchini na nawashukuru wote niliokutana nao Morogoro, Dar, Tanga, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Songea, Mbeya, Kagera, Musoma, Zanzibar, Singida, Kibaha, Dodoma na Karatu kwa namna mlivyonipokea. Nimejifunza mengi kwa jinsi tulivyoongea na nasikitika pia kwa muda mchache nilokuwa nao kupata kubadilishana nanyi mawazo. Yote tuliyoongelea yanafanyiwa kazi na matunda yake yataonekana soon. Nawashukuru wote walionipa ushirikiano wa namna moja ama nyingine wakati wa maandalizi hadi kufanikisha harusi yangu, ahsanteni sana.

Kutokana na kuwa mbali na jukwaa hili kuna mengi nayaona humu, kuna mambo hayaridhishi na ndiyo ningependa tuhadharishane ama kuelekezana.

Kama muasisi wa JF, ningependa kuwakumbusha kuwa hapa hoja inajibiwa na hoja. Haipendezi kabisa hoja kujibiwa kwa viroja!

Kuna namna flani ya uwakilishaji hoja ambayo nimeiona humu ikionekana wazi ni dhamira mbaya kabisa ya kuweza kuwakatisha tamaa wanachama flani kwa kujadili watu badala ya hoja.

Haijalishi mwanachama ni mzoefu wa muda gani hapa JF, wengine wamechelewa kupafahamu hapa na kama wamejiunga nasi basi tuwapokee kwa busara ili watambue kuwa wenyeji wao tu wakarimu. Tuwaelekeze kiungwana tunapoona wanaenda nje ya mstari na kuwasahihisha ili twende nao sawa. Wanaweza kuja na mawazo ambayo inaonesha wazi kuwa hawajui tulikotoka, vema tuwape links (kwakuwa zipo tu) ili badala ya kuchanganya mambo wasome kwanza kabla ya sisi kuwanukuu huku tukiwambia "Una vijipost viwili halafu una pointless au wewe ni ***** au mpumbavu wewe".

Ni heri asiyejua akakosea na kuelekezwa kuliko anayejua akakosea makusudi. Tuwaheshimu wenzetu ili kupitia sisi wajifunze zaidi na zaidi.

Kuna mengi nimeyaona humu lakini nikasema hapana, ni heri kuwakumbusha kuwa hoja hujibiwa na hoja. Kutaniana kupo lakini nako kukizidi inashusha hadhi ya mchangiaji. Nimeombwa na moderation crew kuwa nitie neno nami nikaona nisisite kufanya hivyo.

Nawashukuru Admins, moderators na baadhi ya wanachama kwa ushirikiano mnaonekana kuutoa katika kuhakikisha tunahabarika na kuburudika kupitia JF.

Mengine tutaendelea kushirikishana kadiri muda utakavyopatikana na nawatakia kila la kheri katika uchangiaji wa hoja mbalimbali.

Mac

Si ajabu iko siku polisi nao watakapoandamana kudai haki zao na kutamka wazi kutokurudi nyuma mpaka madai yao yashughilikiwe. Siku hiyo wataeleza walivyochoshwa na tabia ya kutumiwa wao kulinda wahujumu uchumi badala ya kuwakamata. Watatoa masikitiko yao ya kulazimishwa kuwatwanga marungu na kuwarushia mabomu ya machozi wananchi wenzao wasio na hatia kwa kosa tu la kudai haki zao. Wataeleza wanavyoamriwa kufanya kazi zao kwa upendeleo na kwa maslahi ya CCM na si ya taifa wanalolipenda. Na mwisho wataeleza jinsi baada ya kushinda juani kutwa zima, hurudi kwenye nyumba zao za mbavu za mbwa na kukabiliwa na watoto wao wanaolia njaa, njaa. Wanahabari wameanza na sasa ni zamu ya wauguzi, madereva, makarani, waalimu, wahandisi n.k. Haki lazima idaiwe.
 
I still don't understand kwanini Pundit katika kuonesha hoja za mtu mwingine kuwa ni dhaifu umelazimika kutumia maneno ya "upumbavu, na ujuha" kumdescribe mtu unayetofautiana naye au positions zake?

hivi hoja haiwezi kupingwa na hoja za mtu kukataliwa bila kuitana majina kwani nyume ya hicho ni madai ya kuwa bora zaidi "I'm smart, I'm more intelligent, n.k". Nadhani kwa jinsi hoja unavyozipangua ndivyo watu wanaweza kuona jinsi gani hoja zako zina nguvu.

Hii tabia ipo sana siyo kwako tu ndugu yangu bali nimeiona kwa mzee mwenzangu FMES, bwana mdogo YNIM, na wengine wengi. I reallyl don't get it.

Ila kama ni kweli mtu anaamini kuwa fulani ni mjinga, juha, mpumbavu n.k then its a fair game. Naamini ujuha, upumbavu au sifa nyingine yeyote ya mtu inaoneshwa kwa kuchambua hoja zake na kuziweka tupu mbele ya hadhara.
 
Hii tabia ipo sana siyo kwako tu ndugu yangu bali nimeiona kwa mzee mwenzangu FMES, bwana mdogo YNIM, na wengine wengi. I reallyl don't get it.

Mkulu Wangu MMJ,

Hapo hukunitendea haki, umelisema hili neno mara nyingi sana na nimekujibu mara nyingi sana kua sijawahi kumchokoza member yoyote hapa na hilo neno,

lakini Yes nimelijibu mara nyingi sana baada ya kurushiwa kwanza, kama nilivyorushiwa hapa, kama kuna mwenye ushahidi kuwa nimewahi kumrushia kwanza, ajitokeze hapa na ushahidi! Nitabeba msalaba wangu!

Otherwise, hujanitendea haki hapa kwa sababu sijawahi kukurupuka, especially na hizo lines za (matusi).

Na kwa nyongeza tu ni kwamba hawa waandishi wengi walioandamana, ninafanya nao kazi kwa karibu sana, sasa ukiwaita vilaza, bila ya kosa ni lazima nijibu ipasavyo na kama nilivyojibu, unless neno vilaza ni matusi, au?
 
Mkulu Wangu MMJ,

Hapo hukunitendea haki, umelisema hili neno mara nyingi sana na nimekujibu mara nyingi sana kua sijawahi kumchokoza member yoyote hapa na hilo neno,

lakini Yes nimelijibu mara nyingi sana baada ya kurushiwa kwanza, kama nilivyorushiwa hapa, kama kuna mwenye ushahidi kuwa nimewahi kumrushia kwanza, ajitokeze hapa na ushahidi! Nitabeba msalaba wangu!

Otherwise, hujanitendea haki hapa.

mzee sijasema mtu aliyetumia kwanza ndio maana nimesema na wengine wengi. Ninaamini kabisa kuwa mtu akiniita mimi "mpumbavu" na mimi nikigeuka na kumuita "mpumbavu" siyo kuwa ninalipiza kisasi bali ninakuwa nimeshuka katika level yake.

Mfano mzuri tumeiuona juzi wa Chiligati alipokuwa anamsema Mbowe kuwa anamdhalilisha Rais na kuhoji "mbowe ni nani" n.k Wakati anampinga Mbowe kutumia maneno makali kumuelezea Rais Kikwete yeye mwenyewe akawa anatumia maneno ya aina hiyo hiyo na hivyo kuhukumu kitu ambacho yeye mwenyewe anakifanya.

Naamini kati ya watu wenye hoja zinazoweza kusimama zenyewe na ushahidi uliodhahiri wewe ni kinara hapa. Huwa hata hivyo natatizika sana ninapoona mzee mwenzangu unaporushiana madongo na watoto wadogo. Inakuwa mzee mzima mimi watoto wanirushie mayai viza basi niende kununua na kuanza kuwarushia watoto mayai viza vile vile kwa kuwa tu "wao ndio walioanza".

Mzee tuwaache watoto wadogo wachezee mayai viza na matope, hawa watu wazima wenzetu tutawajibu hoja kwa hoja hata kama itabidi turudie zaidi ya mara moja. Na ukiona mtoto anafanya mambo ya namna hiyo ni kumpinga na kumkatalia na kumpa elimu ukishuka na kuwa kama wao hujitofautishi nao na watu watakuona kama wazee wa mitaani ambao hawajakubali kuwa wao sasa ndiyo visima vya hekima.

Natumaini umenielewa mkulu.
 
Mwanakijiji,
Pengine mimi sikusoma vizuri huko yaliko anzia lakini kwa maneno hayo hapo juu sioni kama hoja ya Upumbavu ama Ujuha inamlennga mtu fulani humu isipokuwa habari ambazo zinaaminika..

Mkuu Field Marshall Es,

Hizo habari ilizonukuu hapo juu mbona haziendani na kukutukana au! mfano ..Yaani upumbavu huu hauamini mtu assertive anaweza kukaa na kuona makosa pande zote mbili.
Upumbavu sio mtu ila maelezo fulani, kisha hapa mwisho kamalizia na kusema mtu assertive anaweza kukaa na kuona makosa pande zote mbili..

Kisha ukitazama yaliyofuata..Kwamba kwa kuwa ni waandishi wa habari na wanaandika kuhusu ufisadi wasisemwe ni ujuha wa hali ya juu, kama wanachemka wanasemwa vizuri tu..

Binafsi naamini kabisa huu ujumbe ni kwa wote wenye imani kuwa waandishi wa habari wasisimwe kitu kwa sababu tu wanaandika habari za Mafisadi...
Sasa hapa kama sababu ya kuwakingia kifua waandishi wa habari ni sababu hiyo then huo ni ujuha wa hali ya juu kwa mtu yeyote yule iwe wewe au mimi..Naamini kabisa hakuna mtu anawakingia kifua waandishi ati kwa sababu tu wameandika habari za Ufisadi...Au nimekosea!

Mkuu navyofahamu mimi kuna wakati sisi kama binadamu tunafanya makosa ambayo yanaweza kuingia ktk Upumbavu, ujuha ushamba, Ulimbukeni lakini haina maana kabisa kuwa sisi ni ktk fungu la watu hao...
Kuna wakati mimi mwenyewe husema ninmefanya jambo la kijinga sana! hii haina maana mimi mjinga isipokuwa kwa kosa moja ambalo mwenyewe nakubali ni ujinga kufanya hivyo.
Utanisamehe kama nimekosea ama nime quote vibaya maelezo ya Pundit ambayo yalikuwa deep kuliko nilivyoelezea..
 
Mzee Mkandara, unaweza uko sawa, point yangu ni kubwa zaidi ya mjadala uliopo. Ndio maana nimesema mwishoni kuwa kama mtu unaamini kilichofanywa ni upumbavu, ujuha au ujinga au whatever unaweza kukionesha kitu hicho au hoja hiyo. Lakini nimeona mara kadhaa ambapo mtu (siyo lazima Pundit) anajaribu kutumia visifa hivyo ili kulazimisha hoja yake.

Kama watu wanaamini kuwa wanachokifafanua au kukipambanua ni ujuha, upumbavu au ujingga basi waoneshe hivyo lakini siamini jinsi inavyofanywa ni katika lengo la kuonesha hilo bali la kumfany mtu duni, kumfedhehesha na kumdhalilisha ili aidha aogope kutoa michango, kupinga au kwa namna yoyote ile kutoa mawazo tofauti.

Yawezekana wengine wanaamini katika hilo (na ni haki yao) mimi simo nilikuwa natoa mawazo yangu tu, mtu mwingine anaweza kuona nilichoandika nacho ni ujinga, upumbavu au ujuha na atakuwa akinifikiria na mimi niko hivyo lakini atakaponitaja hivyo ina maana yeye ndiyo yuko smart, anayejua, au ana presume anajua nilipoandika nilikuwa nafikiria nini.
 
I still don't understand kwanini Pundit katika kuonesha hoja za mtu mwingine kuwa ni dhaifu umelazimika kutumia maneno ya "upumbavu, na ujuha" kumdescribe mtu unayetofautiana naye au positions zake?

hivi hoja haiwezi kupingwa na hoja za mtu kukataliwa bila kuitana majina kwani nyume ya hicho ni madai ya kuwa bora zaidi "I'm smart, I'm more intelligent, n.k". Nadhani kwa jinsi hoja unavyozipangua ndivyo watu wanaweza kuona jinsi gani hoja zako zina nguvu.

Hii tabia ipo sana siyo kwako tu ndugu yangu bali nimeiona kwa mzee mwenzangu FMES, bwana mdogo YNIM, na wengine wengi. I reallyl don't get it.

Ila kama ni kweli mtu anaamini kuwa fulani ni mjinga, juha, mpumbavu n.k then its a fair game. Naamini ujuha, upumbavu au sifa nyingine yeyote ya mtu inaoneshwa kwa kuchambua hoja zake na kuziweka tupu mbele ya hadhara.

Mwanakijiji,

Naamini hapa tunaongea hoja. Ukiwa sensitive kwa sababu hoja yako imeitwa "upumbavu" nitashangaa.Mimi mtu akiiita hoja yangu "upumbavu" nitaelewa kuwa hajanitukana, na anaeleza weakness ya hoja yangu.

Kwa hiyo "upumbavu" si tusi, ni description tu ya kitu na kama mtu anatoa hoja za kipumbavu kama hizi za "if you are not with the journalists you are with Mkuchika" then inafaa kuonyesha upumbavu wa hoja hii.

Sioni tabu kusema hivyo pale panapostahili kwa sababu nafikiri mbiu yetu ni kuwa tunaongea kwa uwazi.Sijamtusi mtu, nimeonyesha udhaifu wa hoja tu.

Si ajabu kwa mtu smart akaingia mkenge na kushabikia hoja ya kipumbavu, kwa hiyo tukimkanya kwamba asishabikie hoja ya kipumbavu si kweli kwamba yeye amekuwa mpumbavu, ila anashabikia hoja ya kipumbavu.

Nasema tena, kuamini kwamba waandishi wa habari wasisemwe hata wanapokosea, kwa sababu tu wanaandika habari za ufisadi, ni ujuha wa hali ya juu.
 
1.
mzee sijasema mtu aliyetumia kwanza ndio maana nimesema na wengine wengi. Ninaamini kabisa kuwa mtu akiniita mimi "mpumbavu" na mimi nikigeuka na kumuita "mpumbavu" siyo kuwa ninalipiza kisasi bali ninakuwa nimeshuka katika level yake.

Okay wewe unaamini hivyo, lakini sio lazima na mimi niamini hivyo, maana level za busara zinazidiana, I mean no question kwamba kufikia level ya maturity uliyonayo sasa uliwahi kupitia huku, ambako mimi bado nipo yaani kwenye jino kwa jino, kwako wewe ni kushuka kwangu mimi ni ku-get even na it is about respect.

Kwenye maisha tunaenda stage by stage, ukiruka stage unaishia kua kama Michael Jackson, mtu mzima miaka 50 unalala kitandani na watoto wa miaka 13 na unafikiri ni sawa sawa, kwa sababu wakati wa ule umri uliruka hii stage,

Sasa hapa mnanichanganya nikiyatumia hayo maneno ya upumbavu na ujuha, yanakua matusi lakini akitumia huyu bwana tena ni yule yule, yanakua maneno mengi ya busara, nilisema toka mwanzo aliposema Mkulu Max, kwamba mimi sijawahi kumchokoza mtu hapa, huwa ninachokozwa na huu hapo juu ni ushaidi wangu tosha, kwa kawaida huwa sina sura mbili, maana can you imagine ningekua nazo sura mbili ingekuwaje kwa wale wote ninaoshirikiana nao kwa karibu, na hasa hapa JF?

Sasa uamuzi ni wenu, kama haya maneno ya Pundit sio matusi, basi kila mtu aruhusiwe kuyatumia mimi sikujua kuwa ni matusi mpaka Max aliposema, kuwa ni matusi. Uamuzi ni wenu wakuu mimi simo ila nilitaka kuweka point yangu kuwa huwa siku zote ninachokozwa, that is all!

Nimemaliza na I am out of this!

1.

Okay wewe unaamini hivyo, lakini sio lazima na mimi niamini hivyo, maana level za busara zinazidiana, I mean no question kwamba kufikia level ya maturity uliyonayo sasa uliwahi kupitia huku, ambako mimi bado nipo yaani kwenye jino kwa jino, kwako wewe ni kushuka kwangu mimi ni ku-get even na it is about respect.

Nimekupata mzee carry on...
 
Mwanakijiji,
Mkuu nimekuelewa lakini moja tu naposema uloandika ni upumbavu mtupu haina maana wewe mpumbavu...isipokuwa hukuweza kuona upumbavu wake, na kwa sababu wewe sio Mpumbavu anatumaini utaweza kuona makosa yako wapi...
Kweli kabisa mwandishi ni lazima akuonyeshe Upumbavu wenyewe uko wapi katika mandishi yako..
majuzi tu mkuu wangu fedha yetu ilipokuwa juu ya US nilijiona mpumbavu kutobadilisha fedha zangu wakati leo fedha yetu dhaifu kishenzi, yaani ningevuta bila jasho, na jana tu nilitaka kununua hisa zangu ktk shirika moja ambalo hisa zake zilikuwa chini sana nikasita.. Leo najiona mpumbavu kwa kutochukua hatua hiyo.. sasa sielewi kama mimi ni mpumbavu ama kitendo cha kufanya hivyo ndicho kilichonipa hisia za kujiona Mpumbavu, yet pamoja na kutofanya hivyo, uwezo wangu kufikiria tu makosa hayo kunaniondoa mimi ktk fungu la Upumbavu, kesho nitakuwa makini zaidi.
Huu pia ni mfano mwingine ktk upumbavu..
 
I still don't understand kwanini Pundit katika kuonesha hoja za mtu mwingine kuwa ni dhaifu umelazimika kutumia maneno ya "upumbavu, na ujuha" kumdescribe mtu unayetofautiana naye au positions zake?

hivi hoja haiwezi kupingwa na hoja za mtu kukataliwa bila kuitana majina kwani nyume ya hicho ni madai ya kuwa bora zaidi "I'm smart, I'm more intelligent, n.k". Nadhani kwa jinsi hoja unavyozipangua ndivyo watu wanaweza kuona jinsi gani hoja zako zina nguvu.

Hii tabia ipo sana siyo kwako tu ndugu yangu bali nimeiona kwa mzee mwenzangu FMES, bwana mdogo YNIM, na wengine wengi. I reallyl don't get it.

Ila kama ni kweli mtu anaamini kuwa fulani ni mjinga, juha, mpumbavu n.k then its a fair game. Naamini ujuha, upumbavu au sifa nyingine yeyote ya mtu inaoneshwa kwa kuchambua hoja zake na kuziweka tupu mbele ya hadhara.

...acha kisirani braza, ni wazi una lako jambo!! haukuwa na ulazima wa kufanya ulivyofanya, kwa taarifa tu, attitude yangu juu ya mijadala hapa imebadilika...pay attn!!
 
Quote: Mwanakijiji

I still don't understand kwanini Pundit katika kuonesha hoja za mtu mwingine kuwa ni dhaifu umelazimika kutumia maneno ya "upumbavu, na ujuha" kumdescribe mtu unayetofautiana naye au positions zake?

hivi hoja haiwezi kupingwa na hoja za mtu kukataliwa bila kuitana majina kwani nyume ya hicho ni madai ya kuwa bora zaidi "I'm smart, I'm more intelligent, n.k". Nadhani kwa jinsi hoja unavyozipangua ndivyo watu wanaweza kuona jinsi gani hoja zako zina nguvu.

Quote: Pundit

"1. Naamini hapa tunaongea hoja. Ukiwa sensitive kwa sababu hoja yako imeitwa "upumbavu" nitashangaa.

2. Mimi mtu akiiita hoja yangu "upumbavu" nitaelewa kuwa hajanitukana, na anaeleza weakness ya hoja yangu.

3. Kwa hiyo "upumbavu" si tusi, ni description tu ya kitu na kama mtu anatoa hoja za kipumbavu kama hizi za "if you are not with the journalists you are with Mkuchika" then inafaa kuonyesha upumbavu wa hoja hii.

4. Sioni tabu kusema hivyo pale panapostahili kwa sababu nafikiri mbiu yetu ni kuwa tunaongea kwa uwazi.Sijamtusi mtu, nimeonyesha udhaifu wa hoja tu.

5. Si ajabu kwa mtu smart akaingia mkenge na kushabikia hoja ya kipumbavu, kwa hiyo tukimkanya kwamba asishabikie hoja ya kipumbavu si kweli kwamba yeye amekuwa mpumbavu, ila anashabikia hoja ya kipumbavu.

Mkuu Pundit,

Heshima mbele kaka, hapa ninamuachia Mkulu Max.
 
Mwanakijiji,

Naamini hapa tunaongea hoja. Ukiwa sensitive kwa sababu hoja yako imeitwa "upumbavu" nitashangaa.Mimi mtu akiiita hoja yangu "upumbavu" nitaelewa kuwa hajanitukana, na anaeleza weakness ya hoja yangu.

Kwa hiyo "upumbavu" si tusi, ni description tu ya kitu na kama mtu anatoa hoja za kipumbavu kama hizi za "if you are not with the journalists you are with Mkuchika" then inafaa kuonyesha upumbavu wa hoja hii.

Sioni tabu kusema hivyo pale panapostahili kwa sababu nafikiri mbiu yetu ni kuwa tunaongea kwa uwazi.Sijamtusi mtu, nimeonyesha udhaifu wa hoja tu.

Si ajabu kwa mtu smart akaingia mkenge na kushabikia hoja ya kipumbavu, kwa hiyo tukimkanya kwamba asishabikie hoja ya kipumbavu si kweli kwamba yeye amekuwa mpumbavu, ila anashabikia hoja ya kipumbavu.

Nasema tena, kuamini kwamba waandishi wa habari wasisemwe hata wanapokosea, kwa sababu tu wanaandika habari za ufisadi, ni ujuha wa hali ya juu.

tatizo ni kuwa premise yako is wrong; kwanini unafikiri watu "wanaamini waandishi wa habari wasisemwe"? Waandishi wa habari ni sehemu ya jamii na wao wanastahili kipimo kile kile wanachowapimia wengine. Sasa ili iwe "Ujuha wa hali ya juu" huna budi kuonesha ni wapi mtu kasema au kaashiria kuwa "waandishi wasisemwe".
 
Quote:
Originally Posted by Majita
Wangekuwa vilaza usingekuwa na huo mshawasho wa kuona wataandika nini.Kilaza ni wewe unayesubiri kuona vilaza wataandika nini.Assume wasipoandika huyo mkuchika tutakuitaje????

Quote: Mchukia Ufisadi

Tutamuita Kilaza. Na hadi sasa inaelekea hakuandikwa kwa magazeti mawili niliyoona. Ngoja tusubiri.

Wakuu tupo ukurasa mmoja hapo.
 
Quote: Masatu

Mie nasubiri magazeti ya kesho kuona kama wataandika habari za maandamano ya Mkuchika. Hawa jamaa ni vilaza tu hawajui walifanyalo ni wa kusamehewa....

tatizo ni kuwa premise yako is wrong; kwanini unafikiri watu "wanaamini waandishi wa habari wasisemwe"? Waandishi wa habari ni sehemu ya jamii na wao wanastahili kipimo kile kile wanachowapimia wengine. Sasa ili iwe "Ujuha wa hali ya juu" huna budi kuonesha ni wapi mtu kasema au kaashiria kuwa "waandishi wasisemwe".

I mean waandishi walioandamana wameitwa vilaza, kwa sababu kesho wataandika na kumtaja Mkuchika, sasa so far magazeti mawili yametoka hakutajwa sasa tunawaitaje hawa watabiri wetu na hii hoja?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom