Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
Kinachonishangaza mimi majenerali wetu ambao ni wakosoaji wakubwa wa vyombo vya habari vya nyumbani hawaoneshi mfano wa nini media nyumbani iwe. Basi angalau waandike ripoti moja ya uchunguzi, waifanyie utafiti wa kina halafu waichape kwenye gazeti lolote lile na tuone ubora wa habari hiyo ili na sisi wengine tufuate mfano. Tatizo hawatofanya hivyo bali wataketi kwenye viti vyao vya Ujenerali na tepe zao ziking'ara mabegani wakieleza kwa vifimbo vyao vyeusi vilivyonyoka jinsi gani hakuna vyombo vya habari Tanzania!
Wananikumbusha wale mabwanyeye ambao walikuwa wanasimama na vifimbo vyao pembeni ya shamba huku wanakunywa wanzuki wakicheka kicheko cha dharau, na meno yao wakikenua kwa kejeli; wakiwaelekeza wakulima kulima huku wao wenyewe wamesimama mahali penye magugu! Basi angalau wangeng'oa magugu wanayosimama juu yake ili iwe mfano kwa wanaojifunza kulima!
Mabwanyeye hao wanasema hawako tayari kufanya hivyo kwani watachafuka na hawakuja shamba na nguo za kubadilisha!
Hivi ndivyo walivyo wakosoaji wetu wanaotoa kauli za jumla dhidi ya waandishi wa habari na sekta ya habari nchini! "Tanzania hakuna media" wanatamka kiuvivu! Huku wakicheua vile walivyokula katika viti vyao vya uvivu wanawatangazia wengine pasipo aibu kuwa "Hakuna waandishi wa habari Tanzania!".
Tunapoomba basi watuoneshe mfano sisi wengine ambao fani ya uandishi hatuijui na hatuifanyi inavyostahili (kwa maoni yao) watatoa kila aina ya udhuru kwanini wao wasifanye!
Hawa ndio majenerali wetu wakosoaji wa media nchini ambao wamekaa pembeni na suruali zao vimepanda hadi kitovuni wakicheka cheka kwa kejeli wakiamini katika mawazo yao kuwa kwa vile wao wanasema hakuna media Tanzania basi ulimwengu mzima ukubali hivyo! Na hawa tutaendelea kuwapinga!