Katika kuusaka Urais Lowassa ajiita Ustadh Abdalah

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
524
Reaction score
271
1.lowassa by g.sengo.jpg
Ni baada ya kufanikiwa Makanisani amekuja na mpya, ameamua kuingia katika jamii ya Waislamu kwa maslai yake, katika mbio zake za kusaka Urais akiwa Jijini Mwanza aliweza 'kujisilimisha' kiaina na kujiita Ustadhi Abdalah, hii ni baada ya kuvishwa Joho maalum kwa kufanikisha upatikanaji wa Milioni 590 kwenye Harembee ya Bakwata.

Katika kumpongeza huko Waislamu hao walimpa na jina la Ustadh Abdalah Edward Lowassa.
 
Du! Hata mzee John Malecela alisilimu kabisa akapewa jina la Alhaj Saidi Malecela. Akapewa vigari flani hivi, maccm yenzake yakavipora, akaangukia jicho... Kazi kwake Ustaadh Abdallah
 
View attachment 101491
Ni baada ya kufanikiwa Makanisani amekuja na mpya, ameamua kuingia katika jamii ya Waislamu kwa maslai yake, katika mbio zake za kusaka Urais akiwa Jijini Mwanza aliweza 'kujisilimisha' kiaina na kujiita Ustadhi Abdalah, hii ni baada ya kuvishwa Joho maalum kwa kufanikisha upatikanaji wa Milioni 590 kwenye Harembee ya Bakwata.

Katika kumpongeza huko Waislamu hao walimpa na jina la Ustadh Abdalah Edward Lowassa.

Acheni kumsakama captain lowasa bila sababu za msingi. Kama huna cha kuandika, tulia kimya.
 
haya ustadh abdalah ilajua membe kakuzidi kete, akina nape na mwigulu washakutosa, we mfa maji tu.
 
Hivi nyie vichwa vya panzi hamna la kuandika. Wewe umeona wapi anapewa jina hilo? Kawashipa pabaya Pres 2015 sasa mnaweweseka kama mjuzi kabanwa na mlango. Mwache afanye kazi ya Mungu na nyie baki na majungu yenu kama majuha fulani hivi. Hivi mnashinda hapa kijiweni hamna kazi za kufanya? Wenzenu wanalamaba hela za M4Chaggani. Bakini hivo hivo. I like to know who you are, I doubt you're in bad shapes while M4C Officials are happy in the cuisine and pubs enjoying every cent you poorer contribute. Fool
 
Nachukia sana viongozi wa dini wanaokubali kutumika na wanasiasa katika kufanikisha malengo yao ya kuwania Urais. Siku hizi hakuna fedha chafu makanisani wala misikitini.
 
Acheni kumsakama captain lowasa bila sababu za msingi. Kama huna cha kuandika, tulia kimya.

Si anataka kuwa Rais wa Watanzania wacha ajadiliwe, kwani wewe hofu yako nini akijadiliwa. Ustadhi Abdalah Lowassa mwenyewe hana shaka ndiyo maana alipomaliza kuvishwa Joho akaulizwa sasa umekuwa safi ila jina yeye mwenyewe akachagua kwa kinywa chake, "Naitwa Abdalah".

Kwa vile umemuita na Captain sasa atakuwa akiitwa Ustadhi Captain Abdalah Edward Lowassa.
 
Hamna aliyeingia kwenye hiyo dini akafanikiwa
 
Si anataka kuwa Rais wa Watanzania wacha ajadiliwe, kwani wewe hofu yako nini akijadiliwa. Ustadhi Abdalah Lowassa mwenyewe hana shaka ndiyo maana alipomaliza kuvishwa Joho akaulizwa sasa umekuwa safi ila jina yeye mwenyewe akachagua kwa kinywa chake, "Naitwa Abdalah".

Kwa vile umemuita na Captain sasa atakuwa akiitwa Ustadhi Captain Abdalah Edward Lowassa.

Ha ha ha ha ha ha!!!! Ustaadhi lowasa. Hatuchagui rais kwa kuangalia dini yake.
 
big up ustaadh, huu mwezi watu watakuwa wanafutarishana ile mbaya kwa pesa za wizi
 
Si anataka kuwa Rais wa Watanzania wacha ajadiliwe, kwani wewe hofu yako nini akijadiliwa. Ustadhi Abdalah Lowassa mwenyewe hana shaka ndiyo maana alipomaliza kuvishwa Joho akaulizwa sasa umekuwa safi ila jina yeye mwenyewe akachagua kwa kinywa chake, "Naitwa Abdalah".

Kwa vile umemuita na Captain sasa atakuwa akiitwa Ustadhi Captain Abdalah Edward Lowassa.
ustadh al haj captain Dr. Abdallah Edward Ngoyayi Lowassa (MP), PM (RTD), PRESIDENT(2015)!!!
 
Akienda MEWATA ataitwa MWAJUMA NDALA NDEFU

Akitua TGNP itabidi akubali kuitwa Anti Eddo si unajua hawa pia wamewah kuadvocate mambo hayo. Sipati picha akitua Ntwara.... Njomba Nchumali
 
Hivi hili joho alivikwa ali alikuja kwenye haflka akiwa ameshalivaa mwenyewe?
 
Namkumbuka Jumanne Samwel Malecela. Huyu sasa ni Ustadh Abdallah Ngoyai Lowassa. Madaraka Bwana hayana adabu!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom