Huyu ndiye 'Edwatalib' Ngoyai Lowassa

Huyu ndiye 'Edwatalib' Ngoyai Lowassa

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,625
Reaction score
14,589
View attachment 103590
MWAKA 1995, wakati Watanzania wakiwa kwenye mchakato wa kufanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kama kawaida yao, baadhi ya makada na wapambe wao waliokuwa kwenye mbio za kuusaka urais, walianza kupakana matope.

Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, John Samuel Malecela, ni miongoni mwa makada wa CCM walioathirika kwa kiasi kikubwa na siasa hizo za kupakana matope baada ya kudaiwa kwamba alikuwa amebadili dini yake ya Kikristo na kuingia Uislamu.

Ikavumishwa kwamba kutokana na kubadili dini yake hiyo, sasa Malecela alikuwa amepewa jina la Kiislamu la Jumanne, na kwamba kwa hatua yake hiyo, sasa angetambulika kwa jina la Jumanne Samuel Malecela.

Ikaelezwa kwamba Malecela alifikia hatua hiyo ya kubadili dini yake ili kufanikisha mpango wake wa kupatiwa msaada wa kifedha wa mabilioni ya Shilingi zitakazomwezesha kuwanunua wajumbe wa vikao vya uteuzi ndani ya CCM na hatimaye zimwezeshe kugharamia kampeni zake.

Jumanne Malecela alidaiwa kusilimishwa na Serikali ya Kiislamu ya Iran, na kwamba Serikali hiyo ndiyo ilikuwa imemuahidi mabilioni hayo ya shilingi kwa ajili ya kuusaka urais.

Nimekumbuka kisa hicho cha Jumanne Malecela, baada ya wiki iliyopita, mitandao karibu yote ya kijamii kusambazwa picha za kada wa CCM, mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Sunni al Jamaa kwa upande wa ukanda huu wa Afrika Mashariki, Sheikh Shariff Hussein al Badawi.

Edward Lowassa Picha hizo mbalimbali zilizosambazwa ndani ya mitandao hiyo ya kijamii na watu wenye malengo tofauti, zilimwonyesha Lowassa akiwa amevalia mavazi rasmi na maalumu ya Kiislamu; Joho na Hagali, huku akiwa na tabasamu babu kubwa mithili ya mtu aliyekomunika na kumpokea roho mtakatifu wa kweli.

Kwa mujibu wa mitandao hiyo, Lowassa alivishwa mavazi hayo na Sheikh Sharrif al Badawi, baada ya kufanikisha harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuanzisha Kituo cha Redio Ikra, kitakachomilikiwa na Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza.

Nimesema hapo awali kwamba picha hizo zilisambazwa mitandaoni na watu wenye malengo tofauti kutokana na mjadala mzito kutoka kwa wachangiaji wa mitandao hiyo, ambao baadhi yao walidiriki kuandika maandiko yanayopeleka ujumbe rasmi kwa jamii ya Watanzania kwamba Lowassa alikuwa amesilimu kutoka Ukristo kwenda Uislamu, na kwamba mavazi yale ya joho na hagali, alikuwa amevalishwa baada ya kukamilisha kiapo cha kushuhudia nguzo tano za Uislamu.

Kwa kadri ya ufahamu wangu, kiapo hicho na nguzo tano hizo, ambazo kila Muislamu na kila anayeingia dini ya Kiislamu lazima azishuhudie kwa unyenyekevu wa hali ya juu, huku akiwa amepiga magoti, sehemu ya makalio yake yakiwa juu ya mguu wa kulia, huku vidole vyake vinne vya mkono wa kulia vikiwa vimekunjwa ngumi na kubakiza kidole kimoja cha shahada kikiwa kimenyooka na kuegeshwa kwenye goti la mguu wa kulia, zinamtaka muumini wa dini hiyo kuamini kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wa Allah; kusimamisha swala, kutoa zakah, kufunga Ramadhani na kuhiji Makka.

Wachangiaji hao na wasambazaji hao wa picha hizo katika mwelekeo na mtazamo huo, kwa vyovyote vile, hawakuwa na nia njema kwa Lowassa, bali walikuwa na nia kama ya wale waliosambaza ujumbe kwenye vyombo mbalimbali vya habari mwaka 1995, wakisema John Malecela sasa alikuwa amebadili dini na kuitwa jina jipya la Jumanne Malecela.

Kasoro ndogo katika usambazaji wa picha zile na taarifa zilizoambatana na picha zile, wachangiaji na wasambazaji wa picha na taarifa zile, hawakututajia jina jipya la Lowassa, kwamba sasa ataitwa jina la El Sharrif Ngoyai Lowassa au Edwatalib Ngoyai Lowassa.

Hizo ndizo siasa za ndani ya wigo wa CCM, na hasa katika kipindi kama hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa makada wa CCM wanaousaka urais wa 2015 kwa udi na uvumba.

Anatajwa kuwa mbali sana katika mbio hizo, huku akitajwa kumiliki asilimia zaidi ya 80 ya wajumbe wote katika vikao vya uteuzi vya Chama Tawala hicho, Kamati Kuu (CC), Halmashauri Kuu (NEC) na Mkutano Mkuu.

Ingawa Lowassa mwenyewe hajawahi kuweka hadharani nia yake hiyo, lakini mwenye macho haambiwi tazama, anaweza kuona mapokezi anayopewa kila anapofanya ziara rasmi katika baadhi ya mikoa ambako amewekeza nguvu zake za kisiasa na kifedha, kwa mfano katika tukio hilo la hivi karibuni jijini Mwanza.

Katika tukio hilo, alipokelewa kama Rais au Mwenyekiti wa CCM. Viongozi wa CCM wa wilaya na mikoa, wakuu wa wilaya na mikoa; ya Mwanza na Shinyanga, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, walifunga ofisi na shughuli zao zote za kuwahudumia wananchi wa mikoa hiyo na kwenda kwenye mapokezi ya Lowassa.

Gazeti moja linalochapishwa kila siku hapa nchini, katika kuripoti mapokezi hayo ya Lowassa jijini Mwanza, chini ya kichwa cha habari kisema; Lowassa apata mapokezi makubwa, liliandika hivi: "Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, jana alilitikisa Jiji la Mwanza baada ya kuwasili jijini hapa.

"Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa jijini hapa, Lowassa alipokewa na mamia ya wananchi, viongozi wa Serikali, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wa madhehebu ya dini na mamia ya waendesha pikipiki.

Wakati akitokea Uwanja wa Ndege kuelekea katikati ya Jiji, mamia ya wananchi walijipanga barabarani kumpokea huku wakimshangilia." Ninavyofahamu, Lowassa (ambaye ni makosa kumwita Waziri Mkuu Mstaafu kwani hakuwahi kustaafu cheo hicho) ni mbunge tu wa Monduli. Ni Waziri Mkuu aliyeshindwa kuhimili changamoto za wadhifa huo na kujikuta akitangaza mwenyewe kuachia ngazi.

Ndani ya CCM, Lowassa si mjumbe wa NEC Taifa, bali ni mjumbe wa NEC anayewakilisha ki-wilaya kimoja tu cha ki-chama, Monduli. Ndani ya Bunge, Lowassa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje.

Kwa hiyo, kwa mwanachama yeyote wa CCM, kiongozi yeyote wa ngazi yoyote ya CCM, anaposhuhudia mtu mwenye nyadhifa hizo ndani ya chama na ndani ya Bunge akipokewa kwa namna vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti tukio hilo la mapokezi ya Mwanza, itambidi amwangalie Lowassa kwa jicho jingine kabisa.

Miongoni mwa maswali yanayoulizwa vijiweni; ni je; CCM ina uwezo wa kumzuia Lowassa asimrithi Jakaya Kikwete mwaka 2015?

Je; mamilioni hayo ya Shilingi anayoyamwaga Lowassa kwenye harambee zake kila kukicha anayatoa wapi? Kama anachangiwa na marafiki zake, kwa matarajio gani kutoka kwake? Ikitokea CCM ikimtosa wakati amekwishaingia gharama yote hiyo, yeye na wapambe wake hao anaowafadhili kila siku katika shughuli zao binafsi, watachukua mwelekeo na hatua zipi? Naogopa sana yale ya Jumanne Malecela wa mwaka 1995, yasije yakamkuta Edwatalib Ngoyai Lowassa mwaka 2015.

Faili lenye fomu za Jumanne Malecela kuomba vikao vimteue yeye kupeperusha bendera ya chama chake katika Uchaguzi Mkuu wa 1995 halikufikishwa hata kwenye vikao husika vya uteuzi. Inadaiwa kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliapa lisifike kwenye meza kuu, bali liishie kwenye meza ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CCM.


Source :Raia Mwema
MODS: asante kwa msaada tutani!!
 
Wanachanganya mambo hapo,hayo si mavazi rasmi ya kiislamu,uislam hauna vazi rasmi.

Nguo kwa mujibu wa uislam ni ile inayoficha uchi wa mwanaume na mwanamke akaweza kusitirika na aibu yake kikamlifu,
Hayo ni mavazi tuh ya waarabu, kama wangekuwa wameshapata exposure ya kufika nchi za kiarabu wasingezungumza hivyo hao waandishi wa Raia Mwema, kwani hata watu wa iman zingine mfano christians-arabs huvaa kanzu pia wanapoenda makanisani na hata katika shughuli zao za kila siku siku..
 
Tutaona na kusikia mengi ikichukuliwa kuwa kwa Tanzania siyo gharama kuwanunua waandishi wa habari na vyombo vyao vya habari.

Usije kushangaa hata huyu mwandishi wa habari wa Raia Mwema akawa ana upande katika sakata hili au ameisha nunuliwa kwa bei ya mnada wa nyanya sokoni na kujilazimisha kuandika makala kwa haraka haraka hata hakupata nafasi ya kufanya research kujua mila, desturi na taratibu za maeneo, makabila na dini ulimwenguni.

Tanzania kuna vioja ambavyo ni wachache wanafahamu vyanzo vyake.
 
Tuhakikishe Katiba Mpya inataka mgombea kuonyesha uadilifu wake siyo kwa miaka mitano tu ya nyuma bali maisha yote ya kisiasa na kikazi. Na hasa kwa wale wnaochangisha au kuchangia mapesa yanayotia shaka watueleze wameyatoa wapi na siyo tu kuwa amepewa na rafiki zake; awataje hao rafiki zake nao tuwapime uadilifu wao.
 
Sina shaka hata moja na uwezo wa sasa wa Mtanzania wa kawaida kupembua pumba na mchele. Ni kweli kwamba sehemu kubwa ya siasa ni propaganda lakini tutakuwa wagonjwa tena wasahaulifu waliopitiliza tutakapokubali kumpa uongozi wa nchi hii mtu huyu.
 
Alienda kuhiji Israel huyu na pia Nigeria kwa TB Joshua......sasa sijui anatafuta fursa ya kwenda Makkah.....
 
Hongera kwa kazi nzuri, nahisi utakuwa mwandishi wa habari wa Rais mtarajiwa wa nchi ya kufikirika lakini siyo Tanzania kwani huyo unayempigia debe hatapata urais wa Tanzania.
 
Najaribu kubashiri tu kwamba huyu mtu aliye andika haya anafahamiana na Membe na Sita.
 
Alienda kuhiji Israel huyu na pia Nigeria kwa TB Joshua......sasa sijui anatafuta fursa ya kwenda Makkah.....
Jana mchungaji wangu(Usharika sitaji) alonekana kukereka sana kwa tabia hii ya huyu jamaa kutapatapa.
Katika mahubiri alisema huyu jamaa atavalishwa vitu vingi ili aonekane mwema kwa kila mtu, lakini huko nyuma alimuasi Mungu kwa njia zake zisizofaa kiuongozi.
 
yanini kunilisha sumu za majizi ya CCM na wakati raisi wangu ajaye ninaye tayali nshamchagua? kikubwa na hoja ya msingi hapa ni kwamba hawa na chama chao hatuwataki tena 2 015 labda kwa baadae sana.

only Dr.Slaa fits to be my prosper future president rather than thinking of these assults,killers and lunatics from ccm
 
siku bado zipo haya ni mwanzo bado yatajitokeza mengi kuhusu wagombea urais.
 
Maelekezo ya CDM ni kwamba tule pesa saa hizi, hata wakati wa kampeni kura CDM, ndo makamanda ndani na nje ya CHAMA wanavyofanya, asubiri muziki wake 2015, atakufa kwa presha
 
Vilemba vina wenyewe maana hapo picha utadhani bibiharusi, du huu Uraisi tutaona mengi mbele.
 
Atavaa sana hijabu ila Urais hapati

Anatumia pesa nyingi sana kutaka kuingia Ikulu,atarudisha vipi hizo hela?au ndo ya mr Fastjet?
 
Mkuu ni Sheikh Abdalah Edward Ngoyai Lowasa. Jina la Abdalah alichagua mwenyewe huko Mwanza.
 
Kama mtu anafika kuvaa hijabu kwa ajili ya urais basi hiki cheo lazima kitakuwa kitamu mno!
 
Back
Top Bottom