Katika kila Watanzania 10, tisa wamewahi kwenda kwa waganga hasa matatizo yakiwaelemea. Je, dini ni pambo?

gearbox

Senior Member
Apr 20, 2024
187
489
Huu ndio ukweli mchungu watanzania wengi wamewahi kwenda kwa wataalam ila huwa ni siri ya kufa nayo kaburini, hakuna atayekubali kama ameenda au huwa anaenda kwa mganga

wahalifu hasa wa kusafirisha magendo, wizi, utapeli hawa karibu wote wanaenda kwa waganga

Wengi wakiumwa hospitali zikishindwa kutibu watahangaika sana makanisani misikitini na hospitali za ziada lakini mwishowe huamini ni ushirikina, ndipo safari kwa waganga zinapoanza

wafanyabiashara wengi biashara zikianza kuyumba wapo vulnerable kuamini kuna mkono wa mtu, pia mambo ya ulinzi wa kuzindika, kuvutia wateja, n.k. waganga wanatafutwa sana

wanawake wanaotaka malimbwata, kuroga wenzao, kupata waume, kutafuta watoto, n.k. wapo sana huko

wanasiasa kipindi cha ubunge huwa wanafanya kuwe na foleni huko

mtu akiibiwa ama kutaka kulipa kisasi huyoo kwa mganga

wakulima wengi ni wateja wa waganga
 
Point kuu ni Imani, watu wengi wamejengewa Imani Toka wadogo kuamini kwamba waganga wanatatua matatizo kwa 100% ndo watu Hawa hata akijikwaa mlangoni kwake kwa kuvaa ndara vibaya , kesho asubui kwa mganga kuangalia tego .

Kwa hitimisho tu, Ukitaka Mambo yako yote yaende Bila masharti , mtegemee Mungu kwa akili zako zote na sh. Zako maana yeye ndo uliyekupa mwili, roho na nafsi unayoendea kwa mganga.
 
Huu ndio ukweli mchungu watanzania wengi wamewahi kwenda kwa wataalam ila huwa ni siri ya kufa nayo kaburini, hakuna atayekubali kama ameenda au huwa anaenda kwa mganga

wahalifu hasa wa kusafirisha magendo, wizi, utapeli hawa karibu wote wanaenda kwa waganga

Wengi wakiumwa hospitali zikishindwa kutibu watahangaika sana makanisani misikitini na hospitali za ziada lakini mwishowe huamini ni ushirikina, ndipo safari kwa waganga zinapoanza

wafanyabiashara wengi biashara zikianza kuyumba wapo vulnerable kuamini kuna mkono wa mtu, pia mambo ya ulinzi wa kuzindika, kuvutia wateja, n.k. waganga wanatafutwa sana

wanawake wanaotaka malimbwata, kuroga wenzao, kupata waume, kutafuta watoto, n.k. wapo sana huko

wanasiasa kipindi cha ubunge huwa wanafanya kuwe na foleni huko

mtu akiibiwa ama kutaka kulipa kisasi huyoo kwa mganga

wakulima wengi ni wateja wa waganga
Dini hizi hazina maana kwetu na watu hawaziamini ila bası tu wanakuwa na hofu za kijinga na ndiyo maana unakuta wale wanaoendekeza hizi dini ni wafugaji wazuri tu wa majini
 
Waganha ndio walikua watoa tiba na. Utabaili kwa wazee wetu,dini za washezi wazungu na waarabu zimewaharibuni akili,pumbafu zenu.
 
Back
Top Bottom