Youngblood
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 19,295
- 56,242
Kiranga hii pointi yake tangu jana imenifikirisha sana, uliyosema yote hapa ni ukweli mtupu.
Juzi kati nilienda kijijini huko nyanda za juu kusini nimekuta watu wanafanya mambo ya kijinga wasomi na ambao sio wasomi, watu wengi bado wana imani potofu sana, kwakweli inasikitisha sana.
Nina mifano kadhaa ambayo nimeishuhudia mwenyewe.
1. Kuna dogo ameungua na moto wakaenda kwa mganga akawaambia amemwagiwa maji ya moto na mizimu, kama sio kurumbana sana dogo angekufa na kile kidonda mana waligoma kumpeleka hospitali anapakwa mavi ya ngombe ndo dawa.
2. Kuna jirani yetu alikuwa ana kansa ya shingo ya kizazi, hii nina uhakika nayo kabisa mana mtu wangu wa karibu kabisa aliugua ugongwa kama huu wa jirani akapona, ila hawa majirani walimuacha huyo mgonjwa tangu 2022 januari, amefariki December mwaka 2023 kwa upungufu wa damu, ndugu waligoma kumpeleka hospitali wanadai umerogwa na mke mwenzake.
3 Kuna mshkaji wangu mamake mdogo alipata shida wakati wa kujifungua, ikapelekea kupata fistula, bado yupo nyumbani kila siku kwa waganga anadai amelogwa.
Ujinga wa watanzania ni kweli upo kama utamaduni au tuseme ni kama dini (imani) hata utumie nguvu nyingi kiasi gani kuwaelewesha watakuona wewe ndo umepotea.
Watu wanatorosha wagonjwa hospitali wanapeleka kwa waganga wa kienyeji.
Kwa kweli tuna safari ndefu sana.
Credit Kiranga