kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,428
- 7,216
Ukienda Marekani ukaanza kusifu ujamaa wa Karl Marx na sera za kupinga ubepari watakuvumilia kwa muda tu wakiona unaanza kupata ushawishi watahakikisha unapotea. Ubepari na ubeberu ndio sera iliyoletea nchi yao maendeleo na kua tajiri kuliko nchi zote duniani.
Vivyo hivyo kwa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani. Ukienda Uchina na Urusi kuna kauli hazivumiliki. China ukitaka kuleta sera za Marekani na za mabepari wa magharibi watakuzuia. Saudi arabia ukitaka kutangaza injili ya Yesu watakudhibiti mara moja.
Leo hivi kuna mtu anakuja Tanzania na anatoa kauli za kejeli na dharau dhidi ya mfumo wetu wa kujali utu na usawa na kupigania ukombozi wa raia kiuchumi. Mtu huyo sio mwingine ni Antipas Tundu Lissu. Lissu hadi sasa ametoa kauli nyingi dhidi ya mfumo wetu wa uongozi unaoegemea maendeleo kwa wananchi kwa usawa.
Hivi punde baada ya kurudi kutoka Ubelgiji alikokua anafundwa kuhujumu uhuru wa nchi yetu; Lissu amedharau na kukejeli mafanikio ya ujenzi wa miundombinu inayojengwa nchini. Eti hata wakoloni walijenga miundombinu barabara reli na bandari.
Huko ubeleji hata kama hawakumwambia msomi wa kiwango chake angejiuliza kama wabeleji walijenga reli gati mto Congo na barabara kwa ajili ya uchumi wa Congo au Ubelgiji. Huyu anajifanya hajui Wakongo zaidi million 10 waliuliwa kwa kushindwa kukamilisha kwa muda kazi zao tu za kitumwa kwenye mashamba ya mpira na ujenzi wa miundombinu ya kikoloni.
Tukirudi hapa Tanzania, reli barabara zilizojengwa na Wajerumani utalinganishaje na reli tunayojenga wenyewe kwa uchumi wetu kama nchi huru, utakua mtu mwehu. Kama Lissu aliyejaa jazba na kisasi ndio utaweza sema miundombinu ya ukoloni ina maana sawa na hii anajenga John Pombe Magufuli.