Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Sema ukianza kusakama watu kwa kigezo cha uchochezi huwezi jua mipaka yako na mwisho kujikuta unasakama sana watu wako na kuingilia uhuru wa habari ambao ni muhimu kwa taifa. Nchi zilizokomaa kwenye masuala ya uhuru yanaona njia bora ya kukabiliana na uchochezi ni kuukanusha na si kudeal nao kibabe. Pengine sisi hatuna resources au ukomavu wa kuelewa hilo.Benevolent Dictator mara nyingi huleta mabadiliko mazuri sana. Kuminya uhuru, inategemea ni uhuru wa aina gani wa habari.
Kama ni wauchochezi huo hauna msamaha ni lazima uminywe.
Lakini wa kuikosoa Serikali na kutoa njia mbadala sioni kama kuna tatizo.
Maana katiba yetu inaruhusu hilo.
Hata hivyo nimekuelewa mkuu.
Pia mi siamini kuwa kunaweza kuwa na benevolent dictator. Maana kwenye kufanya hivyo kuna watu anakuwa anawakandamiza japo wanaweza kuwa wachache. Pia anaweza kuwa anafanya maamuzi nje ya taratibu tulizojiwekea kitu ambacho ni kibaya. Udikteta ni kama uganga kwa wakristo, tunaamini hakuna uganga mzuri hata kama ulisaidia kukoponya au kukupa utajiri.