Katika hili Magufuli uwe DIKTETA

Wandugu,

1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.

ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.

ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.

iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?

vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.


SHERIA INAYOTUONGOZA

11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.

Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) national framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) state-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.
MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.
SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.

Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.

Dr. Adelatus Kilangi
 
Hiyo kampuni ni ya kimataifa na uwa inadeclare inachokipata dunia nzima kuwa kiko genuine, na wana pata fedha za kuendesha biashara zao na pia soko la kuuza biashara zao kwa sababu ya uwazi wao, leo RAISI WA NCHI ANAPOTANGAZA KUWA HAO JAMAA NI WEZI TAYARI JAMAA WANAINGIA DOSARI KWENYE SOKO LAO NA PIA WANAHARIBU SIFA ZAO, SO WATAULIZWA NA WATASEMA KUWA WAO WAKO RIGHT, NA WATAKAO AMBIWA WATACHUNGUZA ILI KUJIRIDHISHA NA WAKIKUTA NI UONGO BASI TANZANIA NDIO IMEJIFUNGIA FURSA NA NDIO MWANZO WA KUWA NA VIKWAZO RASMI NA VILE AMBAVYO SIO RASMI

Ntawaeka uzi hapa kesho na ntakuquote
Mkuu tunazama KUFANIKISHA SOKO lao ama KUFANIKISHA nchi yetu? Nini cha muhimu hapa?
Ni WAZUNGU ama WATANZANIA?
 
Kumbe na wewe unaamini HITLER alikuwa DIKITETA!!!

Madhara ya UKOLONI ni makubwa sana.

Wauloze WAJEREMANI kama ADOLF alikuwa DIKITETA. Hayo ya kuambiwa na maadui zake changanya na ya kwako.

Ni kweli aliwaua wayahudi. Lakini hili lilikuwa DAI la wajeremani waliwachukia wageni matajiri nchini kwao na hasa WAYAHUDI. Sawa na DONALD anavyotimua wageni kwake huko. Kwangu huo siyo udikiteta.

Adolf aliwafanya wajeremani wawe taifa kubwa. Wote walimpenda.
HITLER alichukia WAGENI na alikuwa ni kama Mnyama.Hivyo ninachokizungumzia ni tofauti na hicho cha Hitler.
 
Halafu kuna watu nchi hiii wanajifanya,wazalendo wanaelewa au wanazijua sheria ila wamekosa busara,Jambo lolote likitokea wanakazana kuteka midia kwa mawazo yao,Badala ya kufanya utaratibu wa kuonana na Rais ili washauriane,wao kazi kulaumu TU,mbona wana nguvu sana kuomba kuonana na Rais wala hawawez kuzuiwa,kwangu Mimi staili ya maisha waliyoichagua ndiyo inayofanya kuwe na tofauti ya malengo baina ya pande hizi mbili.Hakuna wa kupona.
Kuna jambo nimekumbuka. Je SAUTI ya vyama vya UPINZANI iko wapi katika jambo hili la
Masuala ya UCHUMI wetu?
Ama mtazamo wao kuhusu taifa KUIBIWA mali ya Watanzania HALIWAHUSU?
 
Hiyo kampuni ni ya kimataifa na uwa inadeclare inachokipata dunia nzima kuwa kiko genuine, na wana pata fedha za kuendesha biashara zao na pia soko la kuuza biashara zao kwa sababu ya uwazi wao, leo RAISI WA NCHI ANAPOTANGAZA KUWA HAO JAMAA NI WEZI TAYARI JAMAA WANAINGIA DOSARI KWENYE SOKO LAO NA PIA WANAHARIBU SIFA ZAO, SO WATAULIZWA NA WATASEMA KUWA WAO WAKO RIGHT, NA WATAKAO AMBIWA WATACHUNGUZA ILI KUJIRIDHISHA NA WAKIKUTA NI UONGO BASI TANZANIA NDIO IMEJIFUNGIA FURSA NA NDIO MWANZO WA KUWA NA VIKWAZO RASMI NA VILE AMBAVYO SIO RASMI

Ntawaeka uzi hapa kesho na ntakuquote
Nangoja UZI wako uko wapi?
 
Nafikiri kwa mtazamo WANGU binafsi Tanzania hatuna tabia hiyo. Ama ni vipi mkuu?
Tabia hiyo tunayo kaka. Ukienda uchagani utaitea CHASAKA na ujaluoni utaitwa JA KURE.

Ni asili ya binadamu kubaguana. Haina namna ndivyo ilivyo kila mahali.
 
Tabia hiyo tunayo kaka. Ukienda uchagani utaitea CHASAKA na ujaluoni utaitwa JA KURE.

Ni asili ya binadamu kubaguana. Haina namna ndivyo ilivyo kila mahali.
Ninakubaliana nawe kuwa huenda ikawa ni matatizo ya mwanadamu.
Kujiona yeye ni bora, ama kabila lake ni bora kuliko lingine.
Tunamshukuru Mungu kuwa hapa kwetu Tanzania ni watu wachache sana kama wapo wenye tabia hizo.
 
Unaomba udikteta kwa Magufuli?.
Kulingana na ID ya jina lako hapa JF. unahitaji LUKUNDO bila upendo ni vigumu kunielewa.
UDIKTETA ninaouzungumzia kama ulisoma vizuri ni wa LUKUNDO si wa CHUKI. TUKUNDANE na tushikamane pamoja tuokoe nchi hii.
 
Kulingana na ID ya jina lako hapa JF. unahitaji LUKUNDO bila upendo ni vigumu kunielewa.
UDIKTETA ninaouzungumzia kama ulisoma vizuri ni wa LUKUNDO si wa CHUKI. TUKUNDANE na tushikamane pamoja tuokoe nchi hii.
Kama ana Lukundo alitakiwa awacharaze viboko kwanza CCM wenzake waliotufikisha mahali hapa kwani ni dhahiri kabisa pamoja na nia nzuri ya Magufuli ya kutaka kuiokoa nchi lakini tunakwenda kutumbukia kwenye mgogoro mwingine ambao unaweza ukawa na madhara makubwa zaidi kwetu.
 
Unaomba udikteta kwa Magufuli?.
Kulingana na ID ya jina lako hapa JF. unahitaji LUKUNDO bila upendo ni vigumu kunielewa.
UDIKTETA ninaouzungumzia kama ulisoma vizuri ni wa LUKUNDO si wa CHUKI. TUKUNDANE na tushikamane pamoja tuokoe nchi hii.
Si kweli kama vile wengine wanataka sisi tuamini hivyo. Katika MIKATABA ya KIMAKAMPUNI, nchi husika ikigundua kuwa kuna CHEATING/Udangayifu/ DISHONESTY upande wa the other party.

SHERIA za KIMATAIFA zinaruhusu kusimamisha mkataba na KUTATUA mgogoro ule. Wale wengine WAKIKUBALI na kusema
"TNAKUBALI MAKOSA YETU na TUTALIPA" Basi upatanisho hufanyika nao
hujirekebisha na KULIPA kulingana na nchi na kiasi kilichohusika.

. Wengi wangetaka tuamini kuwa kama mkataba ulipitishwa na rais MPYA akaingia madarakani AKAGUNDUA kulikuwa na UTAPELI basi
"ASILIGUSIE swala hilo hata kidogo maana tutakula hasara kubwa".
Nataka kusema HUO NI UONGO mkubwa unaosambazwa na wasioitakia nchi mema na wengine wanajifanya wanajua sheria na kumbe hamna lolote.
 
WAKIKUBALI na kusema
"TNAKUBALI MAKOSA YETU na TUTALIPA"
Hapa kuna watu wawili waliotufikisha hapa tulipo (1)kuna serekali ambayo iliidhinisha wizi kwa njia mikataba mibovu ambao kisheria nao ni wezi na kuna wawekezaji ambao wanaitwa kuwa ndio waliotuibia,Je kati ya hawa wote wawili ni yupi ambaye anatakiwa kukubali makosa yake na kutulipa?.
 
UDIKTETA ninaouzungumzia kama ulisoma vizuri ni wa LUKUNDO si wa CHUKI. TUKUNDANE
Swali nililouliza ni UNAOMBA UDIKTETA kwa magufuli?maana yake ni kwamba Magu ni dikteta wa moja kwa moja ambaye hapaswi kuombwa kuwa dikteta kwa kuwa ana udikteta wa aina zote ila udikteta wenyewe unategemea na mahali anapo utumia na aina ya udikteta anaoutumia na sijasema udikteta wa chuki.

Pia nimesema kuwa (LUKUNDO)upendo alionao anatakiwa auonyeshe kwanza kwa kuwacharaza viboko CCM wenzake ambao wametufikisha hapa tulipo,kwa kuwa huwezi ukamwadhibu mwizi aliyetuibia halafu ukamwacha yule aliye mfungulia mwizi mlango na kumruhusu atuibie na ukimwacha bila kumwadhibu inamaana kuwa humpendi.
 
Hapa kuna watu wawili waliotufikisha hapa tulipo (1)kuna serekali ambayo iliidhinisha wizi kwa njia mikataba mibovu ambao kisheria nao ni wezi na kuna wawekezaji ambao wanaitwa kuwa ndio waliotuibia,Je kati ya hawa wote wawili ni yupi ambaye anatakiwa kukubali makosa yake na kutulipa?.
JIBU ni rahisi. Katika serikali kuna WATU wengi. Mawaziri wa WIZARA hizo za MADINI katika kipindi chote WACHUNGUZWE na kuchukuliwa hatua bili kujali kuwa yeye ni wa CCM ama mjomba wa CCM. Maana Ufisadi hauna CHAMA.Then WAWEKEZAJI nao washughukikiwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom