Katika amri 10 za Mungu sidhani kama hizi 3 aliziweka yeye bali ni viherehere vyetu tu sisi Wakristo

Walimu wa uongo utawajua tu, kwa taarifa yako ukae ukijua kuwa tupo wengi tunaziamini hizo amri na ni kwa neema ya YESU tunafanya hivyo pia ni kwa neema hiyo hiyo tutaokolewa. BARIKIWA KWA KUBADILISHWA NA BWANA.
Kumbe unazini, unatamani, unaiba na unasema uongo kwa sababu kuna neema????

Hapo naona neema ni kubwa kuliko amri.
 
Nimekaa na kutafakari sana kuhusu hizi amri kumi ( 10 ) za Mungu juu yetu sisi Wakristo na kugundua ya kwamba zile saba ( 7 ) kweli Mwenyezi Mungu aliziweka ila hizi tatu ( 3 ) lazima tu zitakuwa zimewekwa na Sisi Wakristo kwa kiherehere chetu na roho mbaya zetu tu zilizotukuka.

Nakataa kata kata kwamba Mwenyezi Mungu aliweka hizi amri tatu zifuatazo :

  1. Usiseme Uwongo
  2. Usizini
  3. Usitamani Mwanamke / Mwanaume asiye Mke / Mume wako
Hivi jamani tuacheni Unafiki na Uwoga kuna Binadamu au Mkristo aliyetukuka kweli anaweza kuishi bila......
  1. Kusema Uwongo?
  2. Bila Kuzini kwa kisingizio tu cha kutegemea Mbunye / Mkuyenge huo huo 24/7?
  3. Kutamani Demu / Mke wa Mshikaji au Buzi / Mume wa Mtu?
Mimi kuanzia leo hii naamini kuwa amri za Mwenyezi Mungu ni saba ( 7 ) tu na hizi tatu ( 3 ) tumezitunga tu Sisi Binadamu / Wakristo hivyo nawashaurini pia Wakristo wenzangu wote popote pale mlipo kuwa acheni kudanganyika na Watu wabaya waliomsingizia Mungu kuwa amezuia kusema Uwongo, Kuzini na Kutotamani Mpenzi wa Mwenzako.

Ipo haja kwa Wakristo wenzangu kujifunza Kutafakari haya Maandiko vizuri na siyo kukubali tu kudanganywa na Watu wa hovyo hovyo ambao hawaruhusu Watu wenye akili kubwa kuhoji mambo ya msingi kama haya.

Haya mnaojua dini na maandiko yake Kindakindaki karibuni mtiririke na mserereke Kiroho zaidi.
mbona maandiko yanaonyesha wazi kabisa kuwa amri zote kazitoa Mungu au umeamua tu kuandika soma kitabu cha kutoka mlango wa 19 wote na wa 20 wote utadhibitisha nani mtoa amri na pia soma kumbukumbu la Torati 5:1-22 iko wazi kuwa Mungua ndio aliyezitoa amri zote kabisaa ubarikiwe unapoendelea kujifunza
 
kitabu chenu mmezoe kupachika na kupachua kwani hata trump ana bible yake
 
Unaongea vitu vy kipuuz san we unaichkulia dunia kma kizibo cha soda?! Akli zako unahis zimelingana na za kila mtu
Bola ukojoe ukalale
 
Uongo huleta kifo .
Kuzini huleta kifo .
Kutamani huleta kifo .

Mshahara Wa dhambi ni kifo .

Kwann sasa Mungu asiwaonye watoto wake ?? .

Sikatai kufa ,,ila kuna kufa kwa kujitakia .
 
Taahira limeandika tena mataputapu... Kwanza kujiita mkristo wakati ni paganism na kichaa si sawa. Ukipingana na mamlaka na wewe umo ndani utaondolewa tu kama Magu alivyomng'oa Nape
 
Hizo ni amri zinazoboresha mahusiano ya MTU na MTU au MTU na jamii, kutokuzitii kunaleta majanga mengi na mifarakano baina ya watu. Amri ni njema na safi, zinatueleza tabia ya Mungu ilivyo.
 
Back
Top Bottom