Katibu wa CUF afungwa miaka 30 jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu wa CUF afungwa miaka 30 jela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na Samson Chacha, Tarime; Tarehe: 12th May 2011

  KATIBU wa Wilaya wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Jeremia Mgunda (37), amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya ujambazi.

  Mgunda ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Sudi, Kata ya Mirare kupitia CUF na mkazi mwingine wa kijiji hicho, Julius Nyerere (43), walihukumiwa wamehukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tarime.

  Katika hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Yusto Ruboroga, wameamriwa kwenda jela miaka 30 na wakimaliza kifungo watamlipa Andrikus Rayar mali walizopora katika tukio la Januari 8, 2009, saa 5:50 usiku.

  Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Hussen Kiria, Mgunda na Nyerere wakiwa na wenzao, Januari 8, 2009 walimvamia Rayar na kufyatua risasi nne kutishia majirani waliotaka kutoa msaada na kisha kuijeruhi familia yake na kupora mali.

  Mali zilizodaiwa kuporwa katika unyang'anyi huo ni pamoja na Sh 680,200, magodoro mawili, mashuka, nguo za kuvaa, redio na viatu. Waliwajeruhi wanafamilia ya Rayar na kutoroka na mali hizo.

  Katika kesi hiyo ya unyang’anyi wa kutumia silaha, maganda manne ya risasi yaliletwa mahakamani hapo kama kielelezo. Upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne.

  Wakati washitakiwa walikuwa watatu, mahakama haikupata uthibitisho kwamba mmoja wao, Januari Sendi (41) alihusika hivyo Aliachiwa huru.

  Hata hivyo, Sendi anatumikia kifungo kingine katika gereza la Tarime.

  Awali, wakili wa washitakiwa hao, Kampuni ya Makowe Chambers ya Musoma, Makowe alidai wateja wake hawakukutwa kwenye tukio.

  Alidai kuwa, kulikuwa na chuki za kisiasa kati ya Rayar (mlalamikaji) na Mgunda kwa kuwa waligombea pamoja nafasi ya Uenyekiti wa Kijiji cha Sudi.

  Wakili Makowe alidai kuwa, mteja wake ameingizwa katika kesi hiyo kisiasa na kuiomba mahakama iangalie upande wa pili wa shilingi.

  Mwendesha Mashtaka, Kiria aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya unyang’anyi wa mali za watu na kufanya makosa wakijitetea kwa kisingizio cha siasa.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  HII NDIYO SURA HALISI YA VYAMA VYETU....HUKO HUKO DIWANI ALIKUTWA NA SMG....wa CHADEMA
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa nina hamu sana ya kuona thread inayohuyusu CUF. Nimechoshwa na thread za CCM na CHADEMA!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bila shaka sababu ni CDM
   
Loading...