Katibu UVCCM azuia mkutano wa vijana uliokusudia kumpongeza Rais Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza Ramadhani Omary Amez

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Katibu UVCCM azuia mkutano wa vijana uliokusudia kumpongeza Rais

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza Ramadhani Omary amezuia mkutano wa chama hicho wenye lengo la kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongizwa na Mheshimiwa Rais Samua Suluhu Hassan ambapo akuweza kutoa sababu hasa za kuweza kuzuia mkutano huo.

Kwa mjibu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa vijana wa Chama hicho wilaya ya Nyamagana na mratibu wa mkutano huo, Boniphace Zephaniah, amesema wametii maelekezo ya katibu huyo na kueleza watayahoji kwa mamlaka yake ya uteuzi.

"Sisi tumetii maelekezo yake na mkutano wetu ulitarajia kufanyika leo lakini unezuiliwa bila sababu za msingi zaidi tutahoji kwa mamlaka yake ya uteuzi na lengo letu halikuwa na nia mbaya zaidi ya kumpongeza mheshimiwa Rais," amesema Zephaniah.

IMG-20230930-WA0282.jpg
IMG-20230930-WA0277.jpg
 
Walikuwa wampongeze Rais kwa lipi? UVCCM ya enzi hizi imeshapoteza dira, uwepo wao hauna maana tena kwenye jamii na tija yao kwenye chama haionekani zaidi ya kusaka teuzi.
 
Back
Top Bottom