Katibu Mtendaji MCT: Vyombo vya Habari bado vinaendelea kupokea vitisho vya kiutawala

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, licha mabadiliko ya sheria kadhaa zinzogusa tasinia ya habari nchini lakini amedai kuwa bado zipo changamoto za kisheria ambazo ni kikwazo kwa vyombo vya habari.

"Pamoja na mabadiliko tunayoyaona ya sheria kadhaa, bado zipo changamoto za kisheria na zile zisizo za kisheria ambazo zinakwaza uhuru wa vyombo vya habari."
photo_2023-09-13_17-04-05.jpg

Kajubi Mukajanga
Ambapo amedai kuwa "Vyombo vya habari bado vinaendelea kupokea vitisho vya kiutawala , changamoto za kiuchumi na kibiashara na nyinginezo."

Ayasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa mawakili 20 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Arusha, Dodoma na Ruvuma yaliyoanza September 12, 2023 Mjini Songea, Mkoa wa Ruvuma.

Mukajanga alisema kuwa vyombo vya habari kama mmoja wakala muhimu katika kukuza na kutetea haki ya kujieleza bado vinaendelea kukutana na changamoto nyingi zinazokwamisha utendaji wao.

Aidha katika wasilisho lake kuhusu sheria mahsusi za kusimamia uhuru wa kujieleza na jinsi zinavyohusu uhuru wa kiraia Wakili Fulgence Massawe amesema kua bado pamoja na marekebisho yanayoendelea kufanyika kwa ujumla wake sheria hizo zimesababisha uwepo mambo kadhaa ambayo yanafanya mazingira ya haki ya kujieleza na hata uhuru wa habari na vyombo vya habari kuwa magumu.

Ambapo alitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa watu kukamatwa kutoka na kutekeleza haki yao ya kujieleza, kupekua na kukamata mali, faini mbalimbali, kuharibiwa vifaa, kuchunguzwa ama kufuatiliwa mawasiliano binafsi.

Pamoja na hayo ametaja mambo mengine kuwa pamoja na watu kubambikiwa mashtaka/makosa ya jinai, kuzimwa kwa mawasiliano ya intanent, hofu ya kushtakiwa, kudhibitiwa katika maudhui katika vyombo vya habari ama mitandaoni.

“Lakini hivi mnajua wapo watu ambao imebidi waende kuishi uhamishoni baada ya vitisho walivyokua wanavipokea kutokana na habari ama matamshi waliyokua wanayafanya,” alisema Wakili Massawe wakati wa uwasilishaji wake.

Kufuatia kauli hizo kuhusu changamoto kwenye vyombo vya habari hususani kuhusu vitisho na kuthibitiwa kwa baadhi ya maudhui, zimetolewa ikiwa kumekuwepo na madai kutoka kwa baadhi ya watu kuwa Serikali kupitia watendaji wake wamekuwa wakiingilia vyombo vya habari kwa kutaka baadhi ya maudhui ya habari mbalimbali zinazogusa mamlaka zisiweze kuripotiwa, hata hivyo Serikali imekuwa ikikana kuhusika kwenye madai hayo.
 
Back
Top Bottom