Katibu mkuu wa Wizara ya Afya lawamani (Blandina Nyoni)


Get your facts right

JF ndio iliipata hii ngoma kwanza halafu hawa akina kubenea wakaja kuinyanyua toka humu na wameshindwa ku acknowledge kuwa source ni JF
 
GT Nakumbuka tangu mjadala wa kwanza wa Blandina Nyoni wewe ulikuwa mtetezi wake. You are still a staunch ally of the woman.

Nyoni hawezi kuwa sahihi eti tu kwa sababu Beatrice ana makosa.

Please, please regain your JF reasoning!

Ya nini kuandikia mate wakati wino upo?

Lete post yoyote ile kuonyesha wapi nilikuwa namtetea huyu mama Blandina na ingekuwa vizuri ukaonyesha wapi i was an ally to her
 
Maliasili kafanya madudu mengi sana, huyu mama ni kimbelembele sana anaishi kwa majungu na kujipendekeza.hana kitu cha maana.
 
labda tungeanza kwa kumuuliza yeye huyo Beatrice ni wapi serikali imepitisha sheria ya uraia wa nchi mbili wakati wanae 4 wana passports mbili mbili

Nje ya topic, wewe mbona una pasi mbili vile vile...!!
 
Ujue amewahi kufanya kazi Wizara ya Afya kama Afisa mafunzo/utumishi hivyo basi anajua inside stories pia..siyo lazima asome JF kama sources of info Mkuu!

WoS

Memory yangu inafifia kidogo, naomba unikumbushe. Huyu Mama alikuwa Afisa mafunzo / utumishi miaka ipi? Mtu ambaye ninakumbuka kuwa alikuwa utumishi ni Mama Mollel, sasa hivi ni Katibu Mkuu (sikumbuki wa Wizara ipi)
 
passports mbili ninazo ya Tanzania na ya EAC travel document hapo tatizo liko wapi?

uraia wangu ni ule ule wa Kibongo...tatizo beatrice wanaye wana URAIA wa UK,USA na TANZANIA sasa huyu ni mtunga sheria atuambie inakuwaje wanae wawe na uraia wa nchi mbili mbili?
 
labda tungeanza kwa kumuuliza yeye huyo Beatrice ni wapi serikali imepitisha sheria ya uraia wa nchi mbili wakati wanae 4 wana passports mbili mbili

Nani nii baba ya hawa watoto,na ni raia wa inchi gani.And which passports do they hold?
 
Nani nii baba ya hawa watoto,na ni raia wa inchi gani.And which passports do they hold?

mmoja na ya Ireland, mwingine UK wawili USA bila kusahau kuwa wote hao wanazo za Tanzania pia

huyo ndio mbunge wetu ambaye yuko mstari wa mbele kutuambia madhambi ya wenzie
 
mmoja na ya Ireland, mwingine UK wawili USA bila kusahau kuwa wote hao wanazo za Tanzania pia

huyo ndio mbunge wetu ambaye yuko mstari wa mbele kutuambia madhambi ya wenzie

Na baba yao atakuwa William Shelukindo Mbungu wa Bumbuli ? au?
Kweykiti wa General Tyre (another big scandal) !!!
 
Hao watoto si watu wazima? Utamhukumuje mama yao kwa matatizo ya wanawe? Na hayo makosa yao unayodai yanahusiana vipi na hoja ya Mheshimiwa Mbunge?

Amandla.......
 
ni watoto wa kufikia wa beatrice
pili wazazi wao hawajui nini watoto wamefanya

ukiomba uraia wa nje hawakuambii wewe uukane uraia wa nchi yako kwa hiyo hawajafanya kosa lolote

wamechelewa kwenda kuukana uraia wa TZ

tafadhali naomba tumjadili beatrice mwenyewe na si watoto wake wa kufikia
 
Tanzania ya miaka hii ina mambo! Mie nadhani Beatrice kidogo kaenda nje ya mstari. Ilikuwa ni rahisi sana kwake kumfuata Mama Nyoni kiongozi/mwanamke mwenziwe na kumuuliza "mwenzangu kulikoni", akapata maelezo mazuri na ya kina kwa nini Nyoni alifanya uamuzi alioufanya hata kama ulikuwa umeshafanywa na Katibu Mkuu aliyekuwepo. Pengine anaweza kupata maelezo mazuri kabisa na ya kuridhisha. Lakini kama shambulia yenyewe ni kutaka umaarufu tu bungeni bila kutafuta ukweli ulivyo si jambo la busara sana.

Nimewahi kwenda India kutibiwa na ninayo picha nzuri tu ya nini kinahitajika pale ili kuwasaidia wagonjwa. Anahitajika Daktari mzoefu wa tiba, mchapa kazi, mwadilifu, mkomavu na si mlevi! Ikiwezekana hata daktari bingwa pamoja na muuguzi mmoja mature wanastahili kwenda pale kusaidia wagonjwa.

Ni wagonjwa wengi sana wanaokwenda India kutibiwa hivi sasa, wanaopelekwa na Serikali na wanaojilipia wenyewe kutokana na unafuu wa tiba na umakini wa Madaktari kwenye hospitali nchini India.
Wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi (ukiacha wale wenye 'fedha' wanaokwenda kwa checkup hata ya mafua) ni wale ambao tiba zao kupitia mabingwa wote tulionao nchini zimeshindikana aidha kwa kukosa utaalam unaostahili ama kwa ukosefu wa vifaa - tukianzia kwa wagonjwa wanaomwagiwa tindikali machoni, wenye satarani, wenye matatizo/complications za moyo wakiwemo watoto wadogo wengi tu, na magonjwa mengine yote unayoweza kuyafikiria kichwani ambayo yanashindikana kutibiwa hapa nchini.

Sasa basi, wagonjwa wakishapitia hatua zote hadi kufikia kupata safari ya kwenda kutibiwa nje, (hapa tunazungumzia India) wanakwenda kwenye hospitali waliyopangiwa. Kwa mfano, kama wanakwenda kutibiwa hospitali iliyopo New Delhi, wakifika pale wanapokelewa na afisa wa Ubalozi wetu nchini India na kupelekwa hospitali - kazi ambayo akipatikana daktari huyo itabidi aifanye yeye. Mbali ya hilo, siku kadhaa kabla wagonjwa hao hawajasafiri anatakiwa kujua ni wagonjwa gani wanakwenda, wanaumwa nini na kama daktari anapaswa kabisa kuelewa kinaganaga na ikiwezekana kukariri kesi ya kila mgonjwa (inabidi awe amepelekewa taarifa za kutosha za kila mgonjwa na kuzielewa vyema).

Daktari kuelewa vizuri tatizo la kila mgonjwa ni muhimu sana ili kuweza kuwasaidia wagonjwa. Wapo wagonjwa wanaopata bahati ya kwenda kutibiwa nje lakini hawajui hata neno moja la Kiingereza kuweza kuelezea magonjwa yao kwa ufasaha hata kama inakuwepo ripoti inayotoka kwenye hospitali zetu huku (ambayo mara nyingi haina maelezo ya kina kuhusu tatizo la mgonjwa). Kwa hiyo inabidi mgonjwa mwenyewe ahojiwe na aeleze ugonjwa wake kwa madaktari bingwa. Halikadhalika, inapofikia hatua ya kwenda kwenye vipimo mbalimbali Kiingereza cha kujieleza kinahitajika katika kujibu maswali yanayoweza kuulizwa. Daktari wetu atawajibika sana kusaidia kwa hilo.

Nitatoa mfano hai. Tulisafiri na mama ambaye alikuwa na mtoto wa miaka mitano aliyekuwa na matatizo ya moyo na alihitaji operesheni. Kwa kawaida kwenye safari hizo huwa anakuwepo muuguzi ama daktari msindikizaji kutoka wizarani ama anateuliwa na wizara. Lakini, mama huyo alipofika hospitali alijikuta hana msaada wowote wa 'ukalimani' kwa sababu wakati huo, muuguzi msindikizaji hakujulikana yuko wapi. Naweza kumtetea kwamba asingeliweza kuwa kwa wagonjwa wote kwa wakati mmoja. Hata hivyo, kwa bahati mbaya hata angelikuwepo muuguzi huyo msindikizaji asingeliweza kufanya 'ukalimani' wa maana kwa sababu hata maneno ya Kiingereza ya kuagiza chakula chake mwenyewe ni tatizo! Pmoja na hayo hata kama lugha ingekuwa inapanda, sidhani kwamba alikuwa ametayarisha ripoti yoyote ya wagonjwa ili hata kama akiulizwa ghafla aweze kuwa na majibu sahihi ya papo kwa papo kuhusu mgonjwa/wagonjwa wake. Kwetu sisi tulimuona kama ni mtalii fulani tu aliyepanda ndege kwenda New Delhi kutembea na kufanya shopping!

Daktari anayetakiwa India anahitajika afanye nini mbali ya kupokea wagonjwa?

1. Kama nilivyosema hapo juu awe anajua kinaganaga wagonjwa anaowapokea na kuwapeleka hospitali wana matatizo ya aina gani.

2. Wagonjwa husafiri mwendo mrefu kutoka Tanzania hadi India, awe amejitayarisha na ajue cha kufanya endapo mmojawapo anaweza kuzidiwa akishateremka kwenye ndege.

3. Wagonjwa wanapofika hospitali awe amekwishafanya utaratibu mzuri wa wagonjwa hao kuonana na mabingwa wa tiba zao na kueleza matatizo yao chini ya supervision yake huyo daktari ili pale mgonjwa anaposhindwa kujieleza kutokana na tatizo la lugha yeye awe pale kumsaidia mgonjwa. Kazi hiyo haiwezi kufanywa effectively na Afisa Ubalozi au msindikizaji wa mgonjwa muuguzi ama medical assistant ambao hawana utaalamu wa kutosha wa tiba zilizoshindikana nchini.

4. Daktari anayehitajika, anapaswa kuwa na rekodi sahihi kabisa ya wagonjwa wote kutoka Tanzania wanaolazwa kwenye hospitali zote za India. Anapaswa kufuatilia kwa karibu kabisa tiba inavyokwenda na matatizo yanayojitokeza ya kila mgonjwa. Ni kazi kubwa inayohitaji moyo wa kujitolea.

Kazi hiyo hivi sasa inafanywa na Afisa wa Ubalozi mzalendo ambaye anajitolea sana kwa kufanya kazi usiku na mchana kwenda uwanja wa ndege saa yoyote ya kuwasili kwa ndege inayoleta wagonjwa na kuwasindikiza wagonjwa wanaondoka urudi nyumbani. Pia, hupata muda wa kuwazungukia wagonjwa walio kwenye hospitali za New Delhi tangu siku ya jumatatu hadi jumapili bila kuchoka.

5. Daktari anapaswa kuwa mwadilifu, mwenye kuipenda kazi yake. Katika simulizi za wagonjwa inasemekana kuna muuguzi ama daktari mmoja ambaye alisindikiza wagonjwa kwenda kutibiwa. Baadhi ya wagonjwa wanaopelekwa na serikali wanatoka vijijini au mijini lakini wanakuwa hawajasafiri hata mara moja nje ya nchi. Mgonjwa mmoja alijikuta ameibiwa vijidola vyake vyote na muuguzi ambaye alimwambia alete akamnunulie vitu mjini akarudi na shati moja kwa dola zote mia tatu alizopewa na mgonjwa na kudai ndiyo bei ya shati!

Mwingine, alisindikiza wagonjwa na alipowafikisha kwenye hospitali husika alikuta kuna mgonjwa ambaye tiba ya kansa ilikuwa imeshindikana na alihitaji kurudishwa nyumbani ili asifie India. Wakati huo mgonjwa huyo alikuwa anajiweza kutembea kidogokidogo na mkongojo. Msindikizaji huyo muuguzi/daktari (jina linahifadhiwa) alikataa katakata kumsindikiza mgonjwa huyo kwa madai kwamba yeye ameleta wagonjwa na kwa utaratibu uliozoeleka anapaswa kukaa India kwa wiki moja na kapewa per diem ya siku hizo, kwa hiyo hawezi kumrudisha mgonjwa huyo labda aitwe muuguzi kutoka nyumbani aje amchukue mgonjwa huyo! Mgonjwa yule alikaa zaidi ya siku 10 akafariki akarudishwa nyumbani kwenye sanduku akisindikizwa na muuguzi aliyekataa kumrejesha akiwa hai maana hatimaye mgonjwa alizidiwa sana ikawa haiwezekani tena kumsafirisha akiwa hai!
To cut the long story short! Daktari anayehitajika kwa ajili ya wagonjwa wa India anatakiwa awe mtu ambaye amekomaa kitaaluma, kiakili na kimaadili. Awe Daktari anayeweza kushughulikia na hasa kuwasaidia wagonjwa kwa moyo.

Sina tatizo na uamuzi wa Mama Nyoni wa kupeleka Daktari Mstaafu ambaye bila shaka anao uzoefu wa kutosha sana na anaweza kuwasaidia zaidi wagonjwa kuliko hao vijana hata kama wana taaluma hiyo lakini si waadili, ni walevi, hawawezi kuhudumia wagonjwa ipasavyo n.k.

Mh. B. Shelukindo angejaribu zaidi kumsaidia Mama Nyoni kupeleleza na kufichua matatizo wanayopata wagonjwa wanaopitishwa kwenda India lakini wanaonyanyaswa na kuombwa rushwa pamoja na matatizo wanayoyapata wagonjwa wakifika India badala ya kumlaumu kwa kufuta uteuzi wa Daktari ambaye lazima kuna sababu ya msingi ya mama Nyoni kusitisha uteuzi wake ama kumteua Mstaafu ambaye hata hatujaona dosari yake kiutendaji. Kama sikosei, Serikali inaruhusu Wastaafu ambao fani zao zinahitajika wapewe kazi ama waendelee na kazi zao. Bora Mstaafu aende India ili tusiwe na upungufu wa madaktari kwa kumchomoa mmoja ambaye anahitajika zaidi nyumbani!
 
Boramaisha,

..Mbune hajakwenda nje ya mstari. yuko sahihi kuhoji maamuzi ya serikali akiwa Bungeni.

..sidhani kama suala hili linapaswa kuwa siri kati ya kina mama/dada wawili -- beatrice na blandina.

..hivi hata kama Daktari aliyeteuliwa mwanzo hakuwa na sifa, ina maana hatuna Madaktari ambao bado wako kwenye utumishi wa serikali wenye sifa za kuwa Medical Attache ktk ubalozi wetu wa India?

NB:

..suala hili linazua maswali mengi kuliko majibu.

..je, utaalamu wa huyo Daktari mstaafu unahitajika huko India tu, hapa Tanzania hauhitajiki?

..je, huyo Daktari mstaafu ndiye pekee mwenye maadili na utu wa kuwasaidia wagonjwa huko India, na wenzake walioko ktk utumishi hawana sifa hizo?
 
Mkuu BoraMaisha.

Umeeleza mengi ya muhimu lakini bottom line ni kuwa inabidi tufunguwe wadi ya wagonjwa wetu India! Huyo Daktari mmoja ataweza kuwahudumia hao wagonjwa wote uliowatolea mifano? Pili, huyo Daktari atakaa New Delhi wakati wagonjwa wanapelekwa miji tofauti nchini humo. Hizo per diem za huyo Daktari akiwa anafuatilia masuala ya mgonjwa Chennai si zitatosha kujenga kadispensari Matombo?

Maamuzi haya ni mfano hai wa tunavyopenda majibu mepesi kwa maswali magumu. Badala ya kuborosha huduma za tiba nchini tunamtengenezea mtu ulaji nchini India!

Amandla.........
 
Kama vile haitoshi, mama Nyoni huyuhuyu ni/alikuwa Mwenyekiti/Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini NSSF. Hivyo, anahusika kwa namna moja ama nyingine na madudu mengi ndani ya NSSF - Shirika la "umma" lililojikita katika kunufaisha wajanja wachache kwa kutumia pesa za wanachama wake ambao wengi ni walalahoi!
 
Hao watoto si watu wazima? Utamhukumuje mama yao kwa matatizo ya wanawe? Na hayo makosa yao unayodai yanahusiana vipi na hoja ya Mheshimiwa Mbunge?

Amandla.......

Mama mwenyewe wa kufikia na anakaribiana umri na hao "watoto" watu wazima wenye uwezo kuamua.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…