Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akamatwa na Polisi

Hapo wanasubiri reaction yetu wananchi, wakiona moto umekuwa mkubwa watasema wanamshikilia na ‘upelelezi’ unaendelea.
Hapa ndipo vyombo vyetu vya usalama hunichosha, unamshikilia vipi mtu pasi na kuwa na hati ya mashtaka dhidi yake?

Na hata upelelezi huo ukikamilika kila uchwao yanaibuka mashtaka mapya, BS.
Kuna watu hawalali ili wewe ulale. Mambo mengine mnajitakia kabisa.
Eti vyombo vya usalama vinakuchosha!!!!!
 
Kuna watu hawalali ili wewe ulale. Mambo mengine mnajitakia kabisa.
Eti vyombo vya usalama vinakuchosha!!!!!

Ni kweli tunajitakia kuwekwa kwenye mifuko ya plastiki na kutupwa coco beach, kupigwa risasi , kubambikiziwa kesi zisizo kichwa wala miguu, kuteswa magerezani nk

Mzigo wa mwenzako kwako ni ganda la usufi. Mpira ukigeuka usije kuita maji ni mma
 
Jeshi la Polisi nchini linaendelea kumshikilia mhadhiri na katibu wa Jumuiya ya uamsho Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda kwa kile kinachoelezwa ni kutoa maoni ya taasisi yao juu ya masuala mtambuka yanayoendelea nchini.

Mpaka sasa bado hajapelekwa mahakamani na kuna madai kuwa hajaonana na mtu yeyote wa familia yake au wakili wake.

Sababu kuu iliyoelezwa juu ya kushikwa kwake ni waraka unaolenga kuwaamsha Waislam na kutaka haki itendeke katika Taifa,suala ambalo ni jukumu lake kwa nafasi ya uongozi wa kiroho na vile vile kwa Utanzania wake.

Kushikiliwa kwake bado kunazua maswali mengi ikilinganishwa na namna wanavyotendewa viongozi wa madhehebu mengine ya kidini pale wanapotoa waraka wenye kuhimiza hisia za utengano wa kitaifa tofauti na ushauri wa Ponda.

Miongoni mwa waliowahi kutoa kauli za ukakasi kwa mustakabali wa Taifa ni pamoja na Askofu Gwajima ambaye Mara kadhaa alisikika akiapa kuutokomeza Uislam na kugeuza misikiti kuwa makanisa.

Kama hiyo haitoshi, Gwajima akaamua kuhamasisha makundi ya kikabila huku alitimia mwamvuli wa dini na uaskofu wake kujifanya mtetezi wa moja ya makabila nchini.

Yote hayo hatukuwahi kusikia rabsha zikimkabili kama ambavyo anafanyiwa Sheikh Ponda.

Na hapo ndipo maswali yanapojitokeza: Je, ni Uislamu wake umemponza au waraka?
 
Kakamatwa au kahojiwa?

Hakuwa chini ya ilinzi. Mbona haraka sana kukimbilia kwenye kushambulia ukristo. Inawezekana kuna wakrsto wachache wanawachukia vile vile sisi wakristo kuna waislsmu wachache wanaweza wakawa wanatuchukia. Hatuweshi shambulia au kujenga vita au kuweka chuki kwa waislamu wote. Na nyinyi siyo sahihi kuwachukia wakristo wrote. Tumetoka mbali. Keaho yetu muumba pekee ndiyo anayeijua. Tupendane.
 
Katibu mkuu wa shura ya maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa ponda akamatwa na polisi hivi punde

Amekamatwa akiwa anatoka Msikitini sala ya Alasiri saa kumi na Moja maeneo ya Ilala. Alivyotoka Msikitini anataka kuingia kwenye gari yake ndo Wakamkamata.

Kwa sasa wapo wanasheria wanafuatilia dhamana yake japo inadaiwa wanamhamisha hamisha.

Bado hajajulikana kapelekwa kituo gani.
View attachment 1504199
=======

UPDATES :
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP- Lazaro Mambosasa, ameiambia JamiiForums kwamba ni kweli Polisi wanaye Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

"Tunaye sisi Polisi, tumemkamata kwa Mahojiano ya Uchochezi walioutoa kwenye kitu walichokiita Waraka. Tunamhoji kutokana na ule Waraka, Yeye kakubali kwamba ni wake na Taasisi yake lakini Viongozi wote wa Taasisi wameukana kupitia Vituo mbalimbali vya radio na TV. Hivyo tunazidi kumshikilia. Amesema Mambosasa.

Hivi Karibuni, Shura ya Maimamu Tanzania, ilitoa Waraka kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020

Zaidi, Soma;

Uchaguzi 2020 - Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

CUF: Tunatoa pongezi za dhati kwa Waraka uliotolewa na Shura ya Maimamu. Unachora taswira halisi ya hali ilivyo nchini tangu uhuru

Shura ya maimamu yakana kutoa waraka wa uchaguzi, yampongeza Rais Magufuli kwa kuitokomeza Corona

Sheikh Ponda ajeruhiwa vibaya baada ya kupigwa Risasi mjini Morogoro
mzee baba anatujengea BAKWATA msikiti bab kubwa bana... hatutaki kingine chochote!
 
Hakuwa chini ya ilinzi. Mbona haraka sana kukimbilia kwenye kushambulia ukristo. Inawezekana kuna wakrsto wachache wanawachukia bile vile sisi wakristo kuna waislsmu wachache wanaweza wakawa wanatuchukia. Hatuweshi shambulia au kujenga vita suuwachuki waislamu wote

Soma tena waraka unasema nini, hayo maneno yako ni kweli
 
Mzigo wa mwenzako kwako wewe ni ganda la usufi

Zawadi yako hii

Kama alivyo na anachoongea kinafanana na yeye na mwingine mwenye fikra kama zake anafanana naye. Ukikosa unyenyekevu na hekima roho mtakatifu utakuwa mpumbavu mpaka kifo.

Hyo inaeleweka kwa yeyote asiyemwamini Roho mtakatifu.
 
Kama alivyo na anachoongea kinafanana na yeye na mwingine mwenye fikra kama zake anafanana naye. Ukikosa unyenyekevu na hekima roho mtakatifu utakuwa mpumbavu mpaka kifo.

Hyo inaeleweka kwa yeyote asiyemwamini Roho mtakatifu.

Roho mtakatifu wa kanisa lipi anaaminika zaidi?
 
Roho mtakatifu wa kanisa lipi anaaminika zaidi?
Mimi naamin Roho mtakatifu yupo mmoja tu, sasa cjajua wew unamzungumzia yupi? Au unamzungumzia roho mtaka bifu? Maana huyo yupo kwa wenzetu hawa wanaotoka jangwani(mitendeni)
 
Mimi naamin Roho mtakatifu yupo mmoja tu, sasa cjajua wew unamzungumzia yupi? Au unamzungumzia roho mtaka bifu? Maana huyo yupo kwa wenzetu hawa wanaotoka jangwani(mitendeni)

Unataka kuniambia roho mtakatifu wa kanisa la Roman Catholic anayowaongoza ni sawa na anayowaongoza walokole ??

Na Roho mtakatifu anyewaongoza Mashahidi wa Yehova ndiye huyo huyo anayewaongoza Wa Lutheran ??

Mbona wote wanaamini vitu tofauti ??
 
Back
Top Bottom