Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,638
109,000
Kuanzia Saa Tatu (3) Kamili pale Ofisi Ndogo Lumumba Mwamba na Kiboko ya Wapinzani wote Tanzania hasa CHADEMA na ACT Wazalendo Ndugu Paul Makonda (Katibu Mwenezi na Itikadi CCM Taifa) atakuwa anatambulishwa kuanza Kazi ya Kuwanyoosha na Kuwaadabisha Wapinzani wote nchini Tanzania.

Hakika mtamkoma....!!

====

Makonda atinga na bodaboda, umati wampokea Dar​

1698316793834.png

Na Tuzo Mapunda

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda amewasili Ofisi ndogo ya makao makuu ya chama hicho yaliyopo Lumumba akiwa kwenye Msafara wa bodaboda na kupokewa na umati wa wafuasi na viongozi wa chama na Serikali.

Makonda amewasili akiwa amepakizwa kwenye bodaboda kwa kile kilichodaiwa kuwa alishindwa kuja na gari yake kutokana na msongamano wa magari na umati wa watu uliojitokeza kwenye eneo la ofisi hiyo.

Makonda amewasili kwenye ofisi hizo nsaa 4:30 asubuhi na kuingia moja kwa moja kwenye ofisi za chama hicho kwenda kuwasalimia viongozi mbalimbali waliojitokeza kumlaki akiwemo Sophia Mjema aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi tisa.

Makonda aliyeteuliwa kwenye nafasi hiyo Oktoba 22 mwaka huu, baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa dakika 10 alitoka na kwenda kwenye ukumbi wa kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake kabla ya kuongea na vyombo vya habari.

Baada ya kuingia kwenye ukumbi huo, mkuu wa utawala wa chama hicho, Marko Mhanga alikuwa wa kwanza kuongea kwa kuwakaribisha viongozi na wanachama waliojitokeza kisha kutambulisha viongozi wa vitengo mbalimbali ndani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza utambulisho huo, Marko alimkaribisha Sophia Mjema kuendelea na shughuli ya kumkabidhi ofisi Makonda aliyefanya kazi serikali kwa awamu ya tano kwa kushika nafasi tofauti na mara ya mwisho akihudumu kwenye nafasi ya ukuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, Sophia amesema kitengo hicho ni moyo unaotegemewa na chama hicho kuhakikisha katika chaguzi zinazokuja kinapata ushindi wa kishindo.

"Nimehudumu kwenye nafasi hii kwa kipindi cha miezi tisa nilikabidhiwa kijiti na Shaka Hamdu Shaka na juzi Oktoba 22 Chama kilifanya uteuzi na leo nakukabidhi wewe, tunaimani kubwa utatimiza azma ya chama chetu," amesema.

Amesema anafahamu kwa kuwa wote kwa muda mrefu walikuwa huko serikalini lakini amekuja kukitumikia chama ambacho shabaha yake ni kuendelea kushika dola.

"Una timu kubwa ya kushirikiana nayo, nawaomba watumishi ninaowaacha mpeni ushirikiano dhabiti katika muendelezo wa kukijenga chama chetu," amesema.

Makonda baada ya kukabidhiwa vitendea kazi alitumia dakika nne kuzungumza akianza kwa kumshukuru mtangulizi wake Sophia huku akieleza ni miongoni mwa viongozi waliomfundisha kazi akiwa mtumishi serikali.

"Kwa bahati nzuri nimekuja kukitumikia chama na wewe unanikabidhi tena kijiti kijiti hiki asante sana, kikubwa nashukuru bado naendelea kwenye ulingo wa siasa kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kwenye nafasi nyingine," amesema.

"Sina maneno mengi nasema asante sana kwa kuwa mtumishi wa wengi, ni matumaini yangu mlango ambao Mungu ameufungua atanipa hekima, busara na uvumilivu na kukitumikia chama kwa uadilifu, uaminifu na mafanikio makubwa, ili nisimuabishe Mungu wala Rais aliyeniamini na kuniteua katika nafasi hii," amesema.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba watumishi wenzake wa chama hicho kumpatia ushirikiano kumuelekeza na kumshauri.

"Duniani kote watu wanaishi kwa taarifa na taarifa zinafanya maamuzi ukiwa na chanzo kibovu utafanya maamuzi mabovu, lakini ukiwa na chanzo kizuri utafanya maamuzi sahihi wakati wote," amesema.

Amesema ni matumaini yake atapatiwa ushauri mzuri utakaosaidia ujenzi wa chama hicho ili kiendelee kupata mashiko kwa wananchi.

Makonda amkumbusha Sophia kutowasahau wajane

Amemtakia Sophia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya, huku akimweleza kutokuwasahau wajane maana nao ni miongoni mwa kundi maalumu.

"Wewe mwenyewe umekuwa shahidi tumewapigania nilipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na sasa wewe umepata nafasi hiyo utakuwa kiungo muhimu na mimi nitakuwa na kukumbusha ujane kama sehemu ya kundi maalumu," amesema.

Baada ya mazungumzo hayo viongozi hao waliondoka kwenye ukumbi huo kuelekea kwenye ofisi za CCM, mkoa ambako sherehe za kumkaribisha kiongozi huyo zilikuwa zimeandaliwa.
 
Mh. Makonda Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi, kiongozi mwenye nyota ya pekee inayong'ara nchini anatarajiwa kupokelewa Leo kwenye ofisi ya CCM, Lumumba, Dar Es Salaam.

Siku ya Leo tarehe 26 Oktoba 2023

Kila la kheri Mheshimiwa, kutoka kwa mwana JF Mimi. Natumaini siku moja nitakutana nawe uso kwa uso kwa mara ya kwanza.

Makonda Oyeeee

Kazi iendelee...
 
Kuanzia Saa Tatu (3) Kamili pale Ofisi Ndogo Lumumba Mwamba na Kiboko ya Wapinzani wote Tanzania hasa CHADEMA na ACT Wazalendo Ndugu Paul Makonda (Katibu Mwenezi na Itikadi CCM Taifa) atakuwa anatambulishwa kuanza Kazi ya Kuwanyoosha na Kuwaadabisha Wapinzani wote nchini Tanzania.

Hakika mtamkoma....!!
Ndio Atatatua shida ya ajira kwa Wahitimu? amekuja kutatua tatizo la upungufu wa Dolla?

Post zako zimejaa ujinga mtupu
 
Laiti ungejua adui mkubwa wa Makonda ni wapambe wa mama na wala sio wapinzani usingesema hayo. Kwa kuteuliwa Makonda;
Hivi Kinana ana furaha?
Hivi JK ana furaha?
Hivi Nape ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi January ana furaha?
Hivi Makamba senior ana furaha?
Hivi Philip Mpango ana furaha?
Hivi Majaliwa ana furaha?
Hivi Ridhwani ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi Abdallah Bulembo ana furaha?
Hivi Bashe ana furaha?
Hivi Sofia Mjema ana furaha?
Hivi mzee Warioba amefurahi?
Hivi Askofu Gwajima amefurahi?
 
Kuanzia Saa Tatu (3) Kamili pale Ofisi Ndogo Lumumba Mwamba na Kiboko ya Wapinzani wote Tanzania hasa CHADEMA na ACT Wazalendo Ndugu Paul Makonda (Katibu Mwenezi na Itikadi CCM Taifa) atakuwa anatambulishwa kuanza Kazi ya Kuwanyoosha na Kuwaadabisha Wapinzani wote nchini Tanzania.

Hakika mtamkoma....!!
Huyo nyamitako tunamuona boya tu.Nilidhani kipaumbele ni kuondoa kero kwa watanzania kama vile mgao wa umeme nk. lakini kama ni kuonyesha ubabe kwa Chadema basi ajihesabu ameshashindwa kabla ya kuanza. Kama alishindwa Magu aliyekuwa CIC atakuwa huyo MC wa chama chakavu.
 
Ni kawaida sana vyama pinzani kufuatiliana katika kila jambo Ili kuweka mikakati ya kudhibitiana

Wanachadema wanasubiri kwa hamu Hotuba ya Mwenezi mpya wa CCM Komredi Makonda

Wasiwasi wa Wapinzani ni endapo Makonda atafufua ile sera bora kabisa ya Kuunga Juhudi iliyoasisiwa na Komredi Polepole

Inasemekana Watema Madini makini bado wapo Chadema na leo Makonda huenda akasindikizwa Lumumba na baadhi ya Wabunge waliounga Juhudi wakiwemo Covid-19

Mungu Ibariki Chadema 😀

Tutakuwa mubashara Channel ten 😂
 
Ni kawaida sana vyama pinzani kufuatiliana katika kila jambo Ili kuweka mikakati ya kudhibitiana

Wanachadema wanasubiri kwa hamu Hotuba ya Mwenezi mpya wa CCM Komredi Makonda

Wasiwasi wa Wapinzani ni endapo Makonda atafufua ile sera bora kabisa ya Kuunga Juhudi iliyoasisiwa na Komredi Polepole

Inasemekana Watema Madini makini bado wapo Chadema na leo Makonda huenda akasindikizwa Lumumba na baadhi ya Wabunge waliounga Juhudi wakiwemo Covid-19

Mungu Ibariki Chadema

Tutakuwa mubashara Channel ten
Yaani watu waache shughuli zao wakafuatilie hutuba ya zero brain?
 
Back
Top Bottom