Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa John Mnyika aongea na Wanahabari

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272

=====

Dar es Salaam. Katibu Mkuu mpya wa Chadema, John Mnyika ameanisha vipaumbele vitano vya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mnyika aliyeteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa katibu mkuu Desemba 20, 2019 kuchukua nafasi ya Dk Vicent Mashinji ameeleza hayo leo Jumapili Desemba 22, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema vipaumbele hivyo ni kudai tume huru ya uchaguzi, maandalizi ya wagombea kuelekea uchaguzi mkuu, ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuendeleza sera ya Chadema msingi na Chadema Digital.

Huku akiwashukuru wanachama waliopokea vyema uteuzi wake, mbunge huyo wa Kibamba amesema, “kazi kubwa ya chama cha siasa ni kushika dola, hili ndio lipo mbele yetu kwenye uchaguzi wa mwakani. Katika mkakati huu tumekuja na vipaumbele hivi vitano ambavyo vikitekelezwa kwa ufanisi Watanzania watarajie mabadiliko.”

Mnyika ametumia mkutano huo kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kueleza alipo ofisa wa kitengo cha elimu kwa umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti anayeshikiliwa na polisi.

Licha ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kusema kuwa polisi wanamshikilia ofisa huyo, hajasema anashikiliwa kituo gani jambo linalolalamikiwa na uongozi wa kituo hicho.

Chanzo: Mwananchi
 
Dah Mnyika bhana
FB_IMG_15770219469431104.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana yako kabila gani??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamjamuelewa Ndugu BB, maana yake kuuliza kama ni mchaga.

Sikujua kama BB ni she, anyway He/she anauliza kabila ya mnyika, akijua akiwa mchaga atadumu vizuri na atapata ushitikiano mzuri, atakuwa anatekeleza agenda za ASSOCIATION inavyitakiwa.

Anywa Mnyika ni Mpare ni second Cousin ya Mchaga after Mmeru

Mkuu Ni uwongo Ni msukuma
 
Sio kweli huyu anaukabila sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom