Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa John Mnyika aongea na Wanahabari

Katibu mkuu wa Chadema mh Mnyika amesema wataendelea kushinikiza uwepo wa Tume huru ya uchaguzi lakini siyo kwa kubweteka bali huku wakiendelea kudai haki zao nyingine.

Mnyika amesisitiza iwapo serikali ya CCM haitawapa haki yao kwenye sahani basi wataitafuta wenyewe kwa kutumia njia nyingine za kidemokrasia.

Source ITV habari

My take; Hizo njia nyingine za kiddemokrasia ndio zipi?

Maendeleo hayana vyama!
HEBU AANGALIE KWANZA KAMA HUKO CHADEMA KAMA KUN DEMOCRASIA KAMA MTU AKITAKA KUGOMBEA UENYEKITI TAIFA LAZIMA APOTEE CHADEMA NA ANACHOKITAKA HATOKIPATA ATABAKIKUWA MPINZANI TU MILELE
 
Jamaa naona wanataka kumuiga Raila Odinga, labda wasichokijua ni kwamba Raila Odinga ni tribal leader na hivyo Wajaluo wote na ndugu ya Wajaluo 100% wako nyuma yake, hivyo anapigania maslahi ya Wajaluo Kenya na ndo maana ana uwezo wa kuitisha na maandamano na kuisimamisha nchi, sasa chadema hata huko Uchagani tu wanagawana kura na CCM, sasa utamuingiza nani barabarani?
 
Cdm haigombanii kuwa chama kikuu cha upinzani, labda kama ACT ndio inagombea nafasi hiyo.
Hata ACT nia yao in kukamata dola. Lakini inaposhindikana ni faraja kubwa kuwa mpinzani mkuu. Inakupa leverage na kukutofautisha na vyama kama kina nccr anakoelekea chadema.
 
Mnyika awe mkali na tabia ya kushambuliana mitandaoni bila kuangalia uso wa mtu. Huwezi kuwa na jeshi imara huku askari hawaaminiani. Chadema uchaguzi umeisha lakini vinyongo havijaisha pande zote.

Majeraha ya 2015 hayajapona wanajenga migogoro mingine chama chenyewe bado kina changamoto nyingi. Hivi Mdee alikuwa na ulazima wa kumjibu Mwambe? Hakuna platform ya kusolve hayo nje ya Twitter?

Wako watu wengi wana majeraha ila wameamua kukaa kimya kwa busara kwanini msirudi chini mtafakari hayo majeraha na kuyaweka sawa? Hivi mnafikiri akina Selasini wana roho za chuma na yameisha?

Jeshi imara ni lenye nidhamu na ari ya vita kabla ya silaha bora. Mnahitaji mtaji wa watu kuwaunga mkono na kuwaamini. Mjitafakari kabla hamjatafakari namna ya kuwakomboa Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna vitu atakuja kuvijutia maishani siku zijazo Mnyika, ni pamoja na kukubali uteuzi huu wa ukatibu mkuu. Timing ni mbaya sana.
 
Back
Top Bottom