GreatConqueror
Member
- Mar 27, 2009
- 75
- 5
Nimevutiwa na hoja ya Makamba kwamba safari hii kamati kuu ya CCM iliona ni vyema kupitisha mwanamke kwenye nafasi ya uspika sababu ni wakati wao na kwa kuwa tangu uhuru hatujawahi kuwa na spika wa kike.
Naona chama kama kinawathamini wanawake kingeanzia nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM kwani nayo haijawahi shikwa na mwanamke kuliko kukimbilia kwenye uspika ambao chama hakina uhakika wa kushinda moja kwa moja, ''charity begins at home''. Vinginevyo itakuwa siyo KUWAWEZESHA wanawake bali KUWAWEZA.
Hii statement inanikumbusha kauli aliyotoa Chiligati kuhusu kutoswa kwa Seleli kuwa aliachwa sababu hana mvuto, eti sababu alikuwa anatetea nafasi yake hakupaswa kupata idadi ndogo ya kura. Haijachkua muda tumegundua kuwa hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Kikwete naye hana mvuto. Toka ushindi wa 82% (2005) hadi kushindwa kwa 61% (2010) akiwa madarakani. Ama kweli nyani haoni kundule, na wanawake WAKIWEZWA, WANAWEZESHWA!
Mwanamke awe Katibu Mkuu CCM, naomba kutoa hoja!