Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru inusuru CCM Songea Mjini, msije sema hamkuambiwa

skendo

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
212
101
Bashiru kama Katibu Mkuu wa CCM inapaswa hutumie vyombo vyako vyote vya usalama wa chama ili upewe taarifa sahihi ya mkoa wa Ruvuma.

Ishu ni kuwa kuna kata zaidi ya nne kamati ya Mkoa ilikwisha kuamua na mchakato wa kuwapa Madiwani watarajiwa barua za uteuzi ulikwisha fanyika mara ghafla mchakato ukasimamishwa kwa maelezo ya kuwa Bashiru umetoa maagizo ifanyike hivyo. Hatukatai inaweza kuwa sawa ila umetafuta kujua sifa za hao unaotaka wachaguliwe wewe? Umesikia namna wanavyolitumia jina lako katika huu mchakato?

1- Kata ya Ruhuwiko huyo Mgombea bwana Mahundi anayesema wewe ndiye umeagiza achaguliwe, ndiye yule aliyewai kushikwa Malawi kwa tuhuma za kuingia nchi ya watu bila kibali na nchi haikuwa na taarifa zake na kuzua sitofahamu na akawa ameitelekeza kata zaidi ya miezi 6 bila muwakilishi. Kama haitoshi huyu ndiye aliyeanzisha kikundi cha kusaidia walemavu na kuweka majina ya mke wake na mwanae pia watu wazima(wasio na ulemavu) na vikao vya nidhamu vya chama na madiwani walimwita akaomba msamaha.

2- Kata ya Subira huyu mgombea anayesema wewe ndiye chaguo lako kumbuka ndiye alikuwa Meya wa manispaa ya Songea na ndiye aliekuwa analeta ugomvi kila siku na Mkurugenzi na kupelekea migogoro ya manispaa kila siku na hata kufanya Manispaa ipate hati chafu.

Bashiru, hawa watu sasa kutokana na kurudishwa na wewe wamekuwa na kauli za kuwadharau viongozi wote wa kamati ya siasa ya Mkoa na kusema wao wanakujua wewe hawa wengine kwao si lolote maana wao wana watu ndani ya CCM Taifa.

Ushauri: Tumia vyombo vyako vya chama kujua ukweli usipuuze vitu kwa kuzani siasa wapinzani wataifurahisha Songea kwa uzembe unaoepukika kabisa na tabu mnao wabeba kauli zao ndio zimewavunja moyo kabisa wapiga kura sasa wana Songea wanataka kuona hicho kiburi unachowapa kama kitasaidia chama kwenye uchaguzi.

Nasisitiza, tuma vyombo vyako ujue ukweli wa mambo.
 
Shaibu kapigwa chini ila issue ni kuwa jamaa walipigwa chini na vikao vyote kuanzia Wilaya mpaka kamati ya Mkoa na kumbuka upande wa madiwani katiba ya chama inatoa mamlaka yote kwa viongozi wa Mkoa sasa viongozi wa Mkoa wameshafanya maamuzi jamaa wakapiga simu kwa Bashiru kwa mujibu wa maelezo yao na Bashiru akaamuru jamaa wapewe barua za uteuzi na za mwanzo zifutwe sasa jamaa saizi wanatamba kwamba wao hawa deal na mkoa wana deal na Taifa sasa hii imefanya wananchi waseme sawa tuone hao wa taifa kama ndio wapiga kura mabalozi wengi weshagoma kufanya kampeni na ndio maana tunasema ichunguzwe ukweli ujulikane ili haki ipatikane ila saizi viongozi wa Mkoa na Wilaya wanadharaulika kisa wao wana deal na Bashiru
 
Babeli ilianguka hivi hivi.

Koreshi Mkuu Tundu Lissu ameshatua huko full lugha gongana
 
Shaibu kapigwa chini ila issue ni kuwa jamaa walipigwa chini na vikao vyote kuanzia Wilaya mpaka kamati ya Mkoa na kumbuka upande wa madiwani katiba ya chama inatoa mamlaka yote kwa viongozi wa Mkoa sasa viongozi wa Mkoa wameshafanya maamuzi jamaa wakapiga simu kwa Bashiru kwa mujibu wa maelezo yao na Bashiru akaamuru jamaa wapewe barua za uteuzi na za mwanzo zifutwe sasa jamaa saizi wanatamba kwamba wao hawa deal na mkoa wana deal na Taifa sasa hii imefanya wananchi waseme sawa tuone hao wa taifa kama ndio wapiga kura mabalozi wengi weshagoma kufanya kampeni na ndio maana tunasema ichunguzwe ukweli ujulikane ili haki ipatikane ila saizi viongozi wa Mkoa na Wilaya wanadharaulika kisa wao wana deal na Bashiru
Ok tangu lini watu wa Songea wakaipinga ccm

Nyerere wakati wa kutafuta uhuru sehemu ya kwanza kwenda ni huko Peramiho songea vijijini kwa wamisionari wa kizungu wa kibenediktini ili wamuunge mkono na walimuunga mkono apiganie uhuru

Ccm na Songea ni kama meno na Fizi vinafanya kazi pamoja

Huo Mkoa wa Ruvuma plus Dodoma ni kambi za ccm

Ccm hata ikiweka jiwe linashinda huko

Historia ya Mwalimu Nyerere na mkoa wa Ruvuma ni mkubwa sana

Hata vita vya Idd Amini kambi za huko Ruvuma za kijeshi ndizo zilizoenda Bukoba huko na silaha nzito kwenda kuweka mambo sawa

Mkuu mambo mengine yana historia yake,Mwalimu Nyerere aliwaamini wangoni kama watu jasiri na watu wazalendo mpaka leo huko songea ccm haina upinzani kabisa

Wangoni na ccm wana historia ndefu tangu enzi za Mwalimu Nyerere

Mwalimu vikao vingi vya maamuzi na ziara alizifanya huko Songea

Leo hii hakuna mwanaccm anayefikiria eti wangoni watawasaliti

Kumbuka wangoni hii nchi sio yao walitokea Afrika kusini huko hivyo wanaogopa kurudishwa kwao,wanafuata sheria na kanuni za chama

Wewe nani,Wangoni ndio wazalendo Tanzania tangu enzi za Nyerere
 
Tatizo huko ni full uchawi na unafiki, wacha mtoane ngeu. na wewe utakuwa ni mhanga! we ni sanga One au charles? Aisee
 
Haaaaa! Mzee hii issue ipo hot haijawai tokea mabalozi kugoma kupiga kampeni kwa huu mkoa ila sasa kwa mara ya kwanza mda ndio mwamuzi wacha tuone
 
Shaibu kapigwa chini ila issue ni kuwa jamaa walipigwa chini na vikao vyote kuanzia Wilaya mpaka kamati ya Mkoa na kumbuka upande wa madiwani katiba ya chama inatoa mamlaka yote kwa viongozi wa Mkoa sasa viongozi wa Mkoa wameshafanya maamuzi jamaa wakapiga simu kwa Bashiru kwa mujibu wa maelezo yao na Bashiru akaamuru jamaa wapewe barua za uteuzi na za mwanzo zifutwe sasa jamaa saizi wanatamba kwamba wao hawa deal na mkoa wana deal na Taifa sasa hii imefanya wananchi waseme sawa tuone hao wa taifa kama ndio wapiga kura mabalozi wengi weshagoma kufanya kampeni na ndio maana tunasema ichunguzwe ukweli ujulikane ili haki ipatikane ila saizi viongozi wa Mkoa na Wilaya wanadharaulika kisa wao wana deal na Bashiru
Mtajiju.
 
Ok tangu lini watu wa Songea wakaipinga ccm

Nyerere wakati wa kutafuta uhuru sehemu ya kwanza kwenda ni huko Peramiho songea vijijini kwa wamisionari wa kizungu wa kibenediktini ili wamuunge mkono na walimuunga mkono apiganie uhuru

Ccm na Songea ni kama meno na Fizi vinafanya kazi pamoja

Huo Mkoa wa Ruvuma plus Dodoma ni kambi za ccm

Ccm hata ikiweka jiwe linashinda huko

Historia ya Mwalimu Nyerere na mkoa wa Ruvuma ni mkubwa sana

Hata vita vya Idd Amini kambi za huko Ruvuma za kijeshi ndizo zilizoenda Bukoba huko na silaha nzito kwenda kuweka mambo sawa

Mkuu mambo mengine yana historia yake,Mwalimu Nyerere aliwaamini wangoni kama watu jasiri na watu wazalendo mpaka leo huko songea ccm haina upinzani kabisa

Wangoni na ccm wana historia ndefu tangu enzi za Mwalimu Nyerere

Mwalimu vikao vingi vya maamuzi na ziara alizifanya huko Songea

Leo hii hakuna mwanaccm anayefikiria eti wangoni watawasaliti

Kumbuka wangoni hii nchi sio yao walitokea Afrika kusini huko hivyo wanaogopa kurudishwa kwao,wanafuata sheria na kanuni za chama

Wewe nani,Wangoni ndio wazalendo Tanzania tangu enzi za Nyerere

Unashauri A. C. T wasipeleke mgombea huko watakuwa wanajisumbua.?
 
Masikini ccm, hatimae inaendeshwa kama sole proprietorship. hivi wenye hiki chama wameenda wapi aisee?
 
Tatizo la Songea Mjini nasikia ni Dr Ndumbaro. Ni mchonganishi, mmbea, na anatimu yake ya madiwani ( anabagua)
 
Inaweza kua kweli Ndumbaru ila uwez kua na diwani ambaye katumia nafasi yake kuanzisha kikundi cha walemavu hewa na pesa kala yeye na mkewe na kakili makosa kamati inamtoa Bashiru anamrudisha alafu unataka wananchi wampokee na anasema kabisa mkoa hauniwezi mi na deal na Taifa......
 
Songea ashinde mpinzani? Sidhani
Kumbuka kata ya Lizabon waliwai dharau na ikaenda Cdm na this time inaenda tena cdm maana Ruhuwiko na Lizabon chaguo la wananchi limetolewa na ili kuondoa utata Bashiru achunguze ukweli ili ajue ni fitina au ukweli
 
Back
Top Bottom