Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,461
- 829,851
Mauaji mengine Tabata..mtoa taarifa anasema marehemu kajinyonga, lakini walinda sheria wamegoma hiyo sababu.. Ushahidi ni mwingi sana wa kumtia hatiani lakini kama kawa marehemu hana haki... Huyu si wa kwanza na hatakuwa wa mwisho
Mauaji haya ni mfululizo wa vifo vinavyohusiana na mapenzi.. Bado hatujapoa na kifo cha katibu.. Sio kata lakini na sio tawala! Katibu wa kiroho. Huyu kifo chake kimeacha maswali mengi kuliko majibu! Eti kaamua kujinyonga kisa penzi la mke wa mwajiri wake
Yaani mwizi kajisahau mpaka kajiona ana haki ya kuandika ujumbe mrefu mfano wa barua ya mahaba enzi zetu akililia penzi la wizi tena la mke wa boss? Hivi inaingia akilini kweli hii? Ndio maana nikasema katibu katibua ama katibuliwa!
Ujumbe ni mawasiliano ya wawili nani kavujisha mitandaoni? Mtajwa mtuhumiwa yuko kimya kabisa lakini si vema hapa kumhukumu kwa hili.. Mume ndio kakurupuka.. Haraka haraka hata kabla ya mazishi keshakimbilia mitandaoni na kutangaza msamaha kwa mkewe! Amekuwa na haraka kuliko upesi je analenga kuficha nini?
Aliyekufa ni mwajiriwa wake kwa cheo cha katibu lakini kukiwa na hizo habari za kuchepuka na mkewe halali wa ndoa..! Tuupe muda wakati ya sirini yanaweza kuwa bayana!
Tuliuanza mwaka tukizisoma hizi habari tangu January.. Ni wastani wa vifo viwili mpaka vitatu kwa mwezi, vingine vimevuma sana mitandaoni na vingine havikuvuma sana
Kuna waliua wake/wapenzi
Kuna walioua wake na watoto na wao wenyewe
Kuna waliouliwa wakigombea bibi
Kuna waliouana wakigombea bibi
Kuna waliotaka kuua wote wakafakiniwa mmoja au wote na wao kutoroka na kukamatwa ama kutoroka kusikojulikana
Hizi ni taarifa za,matukio ya vifo, bado zile za walioachwa
Waliojeruhiwa
Waliopata ulemavu wa kudumu nk.. Taarifa kuhusu talaka pia zinatisha sana!
Swami last kujiuliza tunakwenda wapi? Mamlaka na washika dau wako kimya kabisa... Ngoja mmoja wao liwatokee ndio watajitokeza kupaza sauti zao.. Na kwa mwendo huu December mbali
Jamii imeweka ufa na wanajamii..hakuna yoyote aliyeko tayari kwa yeyote walau kwa ushauri wa kujengana, kuonyana kufundishana, kuelekezana na kutiana moyo.. Hakuna nani wa kumshauri nani.. Wakushauri nao wanahitaji kushauriwa.. Wakushauriwa ama hawaamini katika ushauri ama hawazingatii ushauri
Mahusiano ya mwendokasi.. Simu janja ni ziraili wa kifo cha mwili na roho.. Ngoja wauane huko juu na huko mjengoni ndio tutasikia matamko na tume..kwasasa tuendelee kusubiri zamu ya mwingine.. Sijui atakuwa nani..!
December imeshafungua lango.. Katibu katibua ama katibuliwa?