Katiba Ya Zanzibar Imekiukwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Ya Zanzibar Imekiukwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tatanyengo, Jul 26, 2012.

 1. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Katiba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya mwaka 1984 (Toleo la 2010) katika Kifungu cha 19 (1) inasema:

  Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani na wa uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa kubadilisha dini au imani yake.

  Kifungu kidogo cha (2) kinasema: Bila kuathiri sheria zinazohusika na kazi ya kutangaza dini na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiyari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

  Kama hivyo ndivyo:
  1. Kwa nini Waumini wa dini nyingine (wasio waislamu) huko Zanzibar kwanini wanalazimishwa kuwa na mfungo wa Ramadhan kinyume na imani zao?

  2. Kwanini kiongozi wa serikali (SMZ) ahimize kwamba wale wote wataokwenda kinyume na matakwa ya mfungo atachukuliwa hatua za "KISHERIA?"
   
 2. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Umeamini sasa kama serikali ina dini ?
   
 3. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 950
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  CDM na kanisa ni vigumu kuvitenganisha kama muislam na mckiti hilo swali kampe waziri wako mkuu pinda naona jibu analo hapa hutopata jibu mambo ya z'bar wachie wazanzibar wenyewe kama una njaa katafute kitimoto ule au kama unaumwa nenda kaombewe kwa mchungaji fulani pale kati
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,892
  Trophy Points: 280
  sitasema chochote juu ya hili,
  nahisi mchango wangu utasababisha uvunjifu wa amani.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kufunga wakati huu wa ramadhani ni sehemu ya ibada kwa muumini wa dini ya kislam. Nijuavyo au ninavyoamini ibada ni juu mtu na mungu wake. Lazima itoke rohoni kwake maana mbele ya mungu hakuna unafiki. Unaweza ku-pretend kufanya jambo mbele ya binadamu mwenzako lakini sio mbele ya mungu.

  Tukirudi kwenye ibada ya kufunga, muumini anatakiwa aoneshe kushinda vishawishi kwa kutokula siku nzima. Lazima itoke rohoni na sio kwa kulazimisha. Sasa hii ya kulazimisha watu inatoka wapi? Kama mtu hakufunga kula (ibada) kinakuhusu nini maana ni juu yake na mungu wake?
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Huo ndio Uislamu dini ya amani iliyotoka kwa Mungu, kila kitu ni JIHAD tu hakuna willingness ya mioyo ya watu.Ni mwendo wa amri amri kama vile uko Jeshini. Sijui ni Mungu gani anayeaangalia matendo ya kulazimisha au kulazimishwa na si utayari wa muhusika kutoka moyoni. Mimi kwa haya yanayofanywa na waislamu pamoja na viongozi wao naamini kutoka moyoni kwamba huyu Mungu wanayemtumikia ni Mungu wa pekee sana tofauti na Mungu wa Imani zingine.
   
 7. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Leo UKWELI umejidhihirisha CHADEMA wanasimamia MASLAHI ya nani!
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  watu wengine kama hoja huna ni bora ukalale mapema kuliko kuleta mambo ya kashata na kahawa kwenye jukwaa la watu makini. Mleta hoja kaongelea point na zaidi ameonyesha ni kwa namna gani katiba ya Zanzibar imevunjwa. Wewe kwa uelewa wako mdogo wa hata kushindwa kutambua mada inayojadiliwa unaibuka na mambo ya CHADEMA. Kwa uelewa wako CHADEMA wanahusika vipi hapa wakati hata katika maandalizi ya hiyo Katiba ya Zanzibar hawakushirikishwa.

  Ushauri: Siyo makosa kushughulisha akili yako, kwani kufanya hivyo utapanua uelewa wako. Pia siyo vichwa vyote vyenye nywele zina akili (chanzo: Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT Bungeni wiki jana).
   
 9. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe usiwe na akili kama mbuni. Hoja imetolewa na mbunge mchungaji wa CHADEMA, hivyo CHADEMA imedhihirisha inatetea maslahi ya kundi gani!
   
 10. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,160
  Likes Received: 675
  Trophy Points: 280
  Aisee, wacha kutaja kitimoto. Mauzo ya kitimoto yamepungua sana katika kipindi hiki cha mfungo. Yatarejea tena katika hali yake ya awali wakati wakati mfungo umeisha maana walaji waliofunga wataingia tena sokoni. Si kitimoto tu, hata sigara zimeathiriwa na huu mfungo.
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  kilaza
   
 12. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,160
  Likes Received: 675
  Trophy Points: 280
  Point. mungu dikteta ni wa kuogopwa sana.
   
 13. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,160
  Likes Received: 675
  Trophy Points: 280
  Hapa hakuna kufunga, ukweli ni kwamba kilichotokea ni mabadiliko ya ratiba ya kula. Badala ya kula mchana mnakula usiku.
   
 14. M

  MLETAHOJA Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona unakuwa mwoga kujielekeza kwenye hoja iliyoletwa. Kwani hoja anayoileta unaipa majibu ya jumla jumla kwamba haijibiki hapa jamvini. Unawakilisha akili za watu gani hao unaowasemea? Hoja ipi iliyo ngumu kwako unayohitaji Pinda akusaidie kuijibu? Kwamba katiba imekiukwa unahitaji elimu gani kujua hilo? Zanzibar si nchi ya Kiislamu hilo lipo kwenye katiba si ya muungano tu bali hata ile ya zanzibar. Njia bora ya kuifanya Zanzibar iwe ya kiislamu ni kupitia kura ya maoni au kwa kujitenga na muungano si kabla ya hapo. Hilo likipitishwa kikatiba nani atakuwa na ugomvi nalo. Kuwaona wanaokula nguruwe kuwa ni watu duni na kuwatukuza wanakula ngamia ni ufinyu katika kuchambua mambo. Huu udini wenu utawafikisha pabaya.
   
 15. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mbona mwapanda magari mazuri,
  yaundwayo na wala nguruwe namba moja Duniani??
  Kama kuto kula nguruwe ni welevu?
  Kwa nini mpande Mabenzi yenye unajisi?
  kwa nini mpande BMW zenye unajisi?
  Maengineer wa kijerumani,
  Main menu yao kuu nyama ya PIG,
  ngozi ya viti vya benzi,
  yalainishwa kwa mafuta ya pig,
  kapeti la benzi nalo pia,
  lote manyoya ya pig,
  Rangi za kumeremeta?
  lainishwa kwa mafuta ya pig,
  Meli zenu asilia za mbao,
  mwatamani za wala nguruwe,
  mwaagiza meli za wala nguruwe,
  boti za mwendo kasi na michezo,
  Wanja losheni lipustiki,
  zote mafuta ya pig,
  Plastic za compoter rangi pia,
  zimejaa mafuta ya pig,
  Nawapa hakika chungu,
  bila mafuta ya pigi ujima wenu daima.

  Mchele mwaagiza asia,
  wao ni wala nguruwe pia!
  Umelimwa kwenye vijaluba rutuba,
  mavi ya pigi watu mbolea safi,
  Kama kuto kula nguruwe ni akili,
  ninyi mngetawala dunia,
  magari hewani mngeunda,
  dunia za mbali vyombo peleka,
  wala nguruwe wamewatangulia,
  kunajisi mwezi kwa mshikaki wa pig,
  mwezi mtautawazaje? udhu kuutia?
  Ujima mahoka mwasumbuka,
  zama enzi pitwa wakti,
  Elimu kanuni peleleza,
  kwa upana kilindi bahari,
  ujuzi gandishwa wakti bakia nyuma,
  Ukale shikiria gandamiza sheria.
   
 16. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,892
  Trophy Points: 280
  Aisee mirungi imeshuka bei gafla.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 17. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Haya madini tumeletewa na marafiki/washikaji zetu Waarabu na Wazungu. Si rahisi kupata rafiki aliyetimilika kwa mambo yote, lakini unapochagua rafiki jaribu basi kuangalia angalau mwenye akili na maendeleo. Sasa Mwarabu na Mzungu nani zaidi? Ukifuata akili ndogo utegemea kuwa na akili finyu. Poleni
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  inamaana hapo anafanya kulazimisha na anamaanisha Zanziba inaendeshwa kwa misingi ya kiislamu siyo!
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  pia katiba imewekwa kama kivuli tu na inatumika pale inapokuwa na maslahi kwa serikali
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ww ni miongoni mwa wale wanaokunywa pombe leo wanakuja kulewa siku tatu baadae!
   
Loading...