Katiba ya Tanzania: Rostam anauachaje ubunge?

Ibara ya 71(a) hadi (g) inatoa masharti ya mtu kukoma kuwa Mbunge. Hili la kujiuzulu kwa hiari yake halipo.

Ngoja lifike bungeni, wamkubalie au wamkatalie kwani mpaka sasa katangaza tu, bunge halijapokea hayo rasmi, kwa mujibu wa spika leo asubuhi bungeni.
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.

Ukiisoma vizuri utakuta pia hakuna mahali panapomkataza kujiuzulu.
 
Mkuu isome Katiba ya JMT kwa umakini na utaona kwamba tamko lake linamfanya kutokuwa mbunge wa jimbo lake; soma Ibara ya 71(1)(g) paragraph ya pili inasema nanukuu" Lakini iwapo mbunge hatakoma kuwa mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake" RA ametimiza hapo kwenye red color.

bora useme maana watu wanasoma sheria au katiba kama wimbo,kila neno lina maana yake ktk katiba. Sijui hawa neno linalogusa KUJIUZURU wanadhani lipo kujaza nafasi iliyo wazi au wanaelewaje!
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.

Wildcard, ni kweli kuna udhaifu kwenye katiba kwa maana ya kutoonesha waziwazi kabisa ni vipi mbunge anaweza kujiuzuru. Article 71 (c) na (g), zinaashiria tu.

Wildcard, nadhani tumekuwa (me included:biggrin1:!) wavivu tu wa kusoma katiba yetu. Actually, ibara ya 149 (1) inamaliza kabisa mjadala huu pasipo kuacha shaka yoyote:

149.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, Naibu Waziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa madaraka ya kazi yake, aweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiliwa sahihi kwa mkono wake, kwa kufuata masharti yafuatayo:
(a) iwapo mtu huyo aliteuliwa au alichaguliwa na mtu mmoja, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu atawasilisha
kwa mtu huyo aliyemteua au aliyemchagua, au iwapo aliteuliwa au alichaguliwa na kikao cha watu, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye
kikao hicho;
(b) iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika;
(c) iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu wa Spika wa Bunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye Bunge; na
(d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.
Shame on us!
 
Duu! Kweli hakuana kinachoshindikana Duniani? Kweli Rais wa Magamba (RA) kaachia ngazi!
Labda sasa Rais wakuachaguliwa (JK) ataingia kazini aongoze nchi bila ubia na mtu.

Tunasubiri kwa hamu apeleke barua kwa Dr.Thomas Kashilila (katibu wa Bunge), itangazwe jimbo la INGUNGA liwazi. Songombingo za uchaguzi mdogo zianze. Nadhani atapeleka barua mwisho wa mwezi ili akombe mshahara wa July 2011.
 
http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

pp 56

Kifungu cha 70 kinachozungumzia kukoma ubunge kinamalizia hivi.

lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.
 
Hakuna pia katika katiba ambapo mtu analazimishwa kufanya kazi ya uwakilishi wa wananchi, ni makubaliano kati yake na wananchi anaowawakilisha, na iwapo wawakilishi anaowawakilisha watalazimisha awatumikie naye akiridhia hakuna wa kumzuia, kwani anaweza kuendelea kuwatumikia hata akiwa chama kingine (mfano mzuri ni Shibuda na Slaa).

Hili la Rostam kujiuzulu linawezekana kabisa, kwani wapo wabunge wengi waliomaliza muda wao na wakaamua hawaendelei tena kugombea ingawa wananchi wao bado walikuwa wanawahitaji.


Mpendazoe
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.

Ungehangaika kutafuta vufungu kwenye katiba kama Rostam angeshinikizwa kuachia ubunge kwa lazima, hapo katiba ingeshika mkondo wake. Lakini Rostam ametumia demokrasi na kwa hiari yake amepima shughuli zake za kibishara na malumbano yanayoendelea kwamba yanaathiri biashara zake yuko sahihi na ametumia haki ya kisheria kikatiba kuachia ubunge. Ulizeni bungeni mahudhuria yake yakoje? Na kama hali hiyo ingeendelea asubiri kuadhibiwa wakati anaona maisha yake bora kujikita kwenye biashara zake badala ya kushinda analumbana ni watoto wadogo akina Nape?
 
Mbunge asipohudhuria vikao vya bunge mara tatu mfululizo; then speaker ana declare vacant kwa tume. hilo ni gamba hivyo sidhani kama litaandika barua kujitoa kwenda kwa tume (sijui kama ni utaratibu) maana limeondoka bila kupenda
 
Watanzania wenzangu,Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam. Nisaidieni nipate mwanga zaidi.
Vitu vingine havihitaji sana mambo ya katiba kuvi-judge.Yaani kama hujisikii kuongoza watu kwa nafasi ambayo hukulazimishwa kuichukua, basi haihitaji sana katiba kukufanya uache hiyo kazi,Kwa hiyo ni sawa tu, wacha jamaa aende zake
 
kwa mujibu katiba ibaraya71...kamabado ana kadi na mwanachama...basi bado ni mbunge
 
kwa mujibu katiba ibaraya71...kamabado ana kadi na mwanachama...basi bado ni mbunge

Wapi wamesema hivyo? Una direct quote? Ibara ya 71 inaisha kwa kutoa nafasi ya mbunge kujiuzulu (soma juu hapo nimetoa katika katiba)
 
Ungehangaika kutafuta vufungu kwenye katiba kama Rostam angeshinikizwa kuachia ubunge kwa lazima, hapo katiba ingeshika mkondo wake. Lakini Rostam ametumia demokrasi na kwa hiari yake amepima shughuli zake za kibishara na malumbano yanayoendelea kwamba yanaathiri biashara zake yuko sahihi na ametumia haki ya kisheria kikatiba kuachia ubunge. Ulizeni bungeni mahudhuria yake yakoje? Na kama hali hiyo ingeendelea asubiri kuadhibiwa wakati anaona maisha yake bora kujikita kwenye biashara zake badala ya kushinda analumbana ni watoto wadogo akina Nape?

Whether Rostam kashurutishwa au hajashurutishwa, swala liko valid, kwamba katiba yetu inaruhusu mbunge kujiuzulu?

Au hata kama mbunge anaumwa na anaona hawezi kufanya kazi za kibunge kwa mujibu wa katiba hawezi kujiuzulu (kwani amekuwa Papa?)

Jibu lishatolewa na ibara ya 71,

...lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu
au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.

http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

ibara ya 71, pp 56
 
Rostam aliupata UBUNGE KIKATIBA. Haya unayoeleza hapa ni kifungu kipi kwenye KATIBA yetu? Au tuenende kiholela tu!
Hata kama aliupata ubunge kikatiba hakuna mahali kwenye katiba inayosema mbunge hapaswi kujiuzulu kwa utashi wake. Kutumikia taifa ni hiari si kifungo.
 
Back
Top Bottom