Katiba ya Tanzania: Rostam anauachaje ubunge?

Rostam aliupata UBUNGE KIKATIBA. Haya unayoeleza hapa ni kifungu kipi kwenye KATIBA yetu? Au tuenende kiholela tu!
Wewe umetaka utaratibu ndio huo kama kuna mwingine unaoujua basi mimi siujui labda unifahamishe ila wabunge wote huwa wanafuta utaratibu niliouainisha na RA amefuata huo huo. Elewa katiba haiweki utaratibu au kanuni yenyewe inatoa mwelekeo mama tu.
 
Jaman baada ya hiyo ibara 71 (1) (g) kuna proviso. Inosomeka hivi;

"lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge
litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake"

Naomba kuwasilisha
Nilivyoielewa hii ni kuwa atalazimika kujiuzulu endapo ibara ya 71.1(a hadi g) itamkumba Mbunge husika au kama atafariki. Rostam hajakumbana na yote haya. Kaamua tu kwa hiari yake.
 
Wewe umetaka utaratibu ndio huo kama kuna mwingine unaoujua basi mimi siujui labda unifahamishe ila wabunge wote huwa wanafuta utaratibu niliouainisha na RA amefuata huo huo. Elewa katiba haiweki utaratibu au kanuni yenyewe inatoa mwelekeo mama tu.
Utaratibu unakuja baada ya mahitaji muhimu ya KIKATIBA kuzingatiwa na kukamilika. Rostamu arudishe kadi ya CCM kwanza. Mbona tupo wengi tusio na vyama.
 
Utaratibu unakuja baada ya mahitaji muhimu ya KIKATIBA kuzingatiwa na kukamilika. Rostamu arudishe kadi ya CCM kwanza. Mbona tupo wengi tusio na vyama.
Sijakuelewa kwenye bold arudishe kadi ndipo ajiuzulu ubunge au........
 
Sijakuelewa kwenye bold arudishe kadi ndipo ajiuzulu ubunge au........
Akisharudisha kadi ya CCM, ibara ya 71(1)(e) ya KATIBA yetu inamwondoa kwenye Ubunge mojakwamoja. Anakuwa sio mwanachama wa chama kilichompa tiketi ya kugombea ubunge.
 
Akisharudisha kadi ya CCM, ibara ya 71(1)(e) ya KATIBA yetu inamwondoa kwenye Ubunge mojakwamoja. Anakuwa sio mwanachama wa chama kilichompa tiketi ya kugombea ubunge.
Kwani kuwa na kadi ndio kuwa mbunge mbona Nape ana kadi na sio mbunge anyway wewe tega sikio leo au kesho jimbo litangazwe kuwa wazi kama una gutz ukachukue fomu ugombee mengine haya ni mapambo tu ya nyumba ambayo unaweza kuishi bila kuwa nayo.
 
WildCard

Wenzako wanagawana jimbo wewe unag'ang'ana na taratibu kalaghabaho hii ni bongo bana

Mwenzako Lipumba anapigiwa ndogondogo wakati wengine wakidai ni zamu ya wanawake utadhani tunacheza mdako.
 
we POLISI toa jina lako humu. Wenzio twaogopa hata kuchangia... Si unajua jinsi mlivyofundishwa na kukomaaa kutuliza ghasia kwa kulenga risasi za moto viunoni, tumboni, kifuani na kichwani. sasa usije ukasingizia maneno yangu yanaleta fujo hapa..... ohooooooooo....
 
Kwani kuwa na kadi ndio kuwa mbunge mbona Nape ana kadi na sio mbunge anyway wewe tega sikio leo au kesho jimbo litangazwe kuwa wazi kama una gutz ukachukue fomu ugombee mengine haya ni mapambo tu ya nyumba ambayo unaweza kuishi bila kuwa nayo.
Haujanielewa! Sio kila mwenye kadi ya chama cha siasa ni mbunge lakini ili ugombee ubunge ni lazima uteuliwe na chama chochote cha siasa chenye usajili wa kudumu pale kwa Tendwa. Hili ni sharti mojawapo la KATIBA yetu ya JMT. Ibara ya 71(1) inaeleza jinsi mtu anavyokoma kuwa mbunge. Rostam hajakidhi hitaji hili la KATIBA. Namsubiri Katibu wa Bunge atamjibu nini Rostam atakapopata barua yake ya kujiuzulu.
 
Mbunge yupo kwa mujibu wa KATIBA. Ni lazima aondoke kwa mujibu wa KATIBA pia. Kama ni mwizi angetangulia kufungwa kwanza au kufukuzwa kwenye CHAMA chake.
Nimekusoma mkuu ingawa huwezi eleweka kwa mfumo tulio nao kwa sasa sisi tunashangilia bira kujuwa ni mchezo gani tumechezewa huyu nimhalifu kufatana na buranketi nene tulilo funikwa na ccm hatuoni ikiwa chama chake kimekiri mapacha 3 ni mafisadi R A anajivua gamba tunampongeza hukojimbonikwake ni sawa walikuwa wananufaika na ufisadi wake bweha sehem akizalia watoto jilani hawezi thubutu kushika kuku anasafili kijiji cha 3 nk ndohao mapacha3 cdm ninawashuli waishinikize selikali apelekwe mahakamani kama walivo shinikiza wakaanza kujivuwa magamba
 
WildCard

Wenzako wanagawana jimbo wewe unag'ang'ana na taratibu kalaghabaho hii ni bongo bana

Mwenzako Lipumba anapigiwa ndogondogo wakati wengine wakidai ni zamu ya wanawake utadhani tunacheza mdako.
Quinine,
Hapa JF tupo kuelimishana zaidi. Nimeliangalia hili "game" la Rostam tangu jana nikawa nashangaa endapo wengi wetu tunaijua KATIBA au la. Na hiyo KATIBA mpya tunayodai itatusaidia kweli? Wapo walioapa kuilinda na kuihifadhi KATIBA hii. Wanasemaje juu ya hili pungufu kati ya mapungufu mengi tulionayo kwenye sheria hii mama ya nchi yetu.
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.

Nimekusoma mkuu, hapo umenena kweli. Lakini vile vile kwenye vifungu vya katiba hakuna sehemu ilikotajwa kwamba iwapo mbunge atajiuzulu kwa hiari yake mwenyewe ni kosa kikatiba, nahisi walioverlook kwa kuamini kwamba mtu huwezi kuuacha ubunge kwa hiari yake mwenyewe.
 
Hakuna pia katika katiba ambapo mtu analazimishwa kufanya kazi ya uwakilishi wa wananchi, ni makubaliano kati yake na wananchi anaowawakilisha, na iwapo wawakilishi anaowawakilisha watalazimisha awatumikie naye akiridhia hakuna wa kumzuia, kwani anaweza kuendelea kuwatumikia hata akiwa chama kingine (mfano mzuri ni Shibuda na Slaa).

Hili la Rostam kujiuzulu linawezekana kabisa, kwani wapo wabunge wengi waliomaliza muda wao na wakaamua hawaendelei tena kugombea ingawa wananchi wao bado walikuwa wanawahitaji.
Je wananchi wana uwezo wa kumkataa mbunge asiwatumikie? Wanaweza kumshinikiza mbunge ajiuzulu? tusaidiane hapa kwa sababu ameacha wakati wananchi "wanampenda". Je wananchi wanaweza au wana haki ya kumkataa mbunge wakati bado yeye anaupenda ubunge?
 
Nimekusoma mkuu, hapo umenena kweli. Lakini vile vile kwenye vifungu vya katiba hakuna sehemu ilikotajwa kwamba iwapo mbunge atajiuzulu kwa hiari yake mwenyewe ni kosa kikatiba, nahisi walioverlook kwa kuamini kwamba mtu huwezi kuuacha ubunge kwa hiari yake mwenyewe.
Utanukuu ibara ipi ya KATIBA kulitangaza jimbo la Igunga liko wazi. Nakubaliana nawe kuwa watungaji wa KATIBA waliamini mtu hawezi kujiuzulu Ubunge kwa kuwa siasa za nchi hii ni uwekezaji. Mtu anaupata ubunge kwa gharama kubwa. Ni lazima zirudi. Rostam arudishe kadi ya CCM.
 
Haujanielewa! Sio kila mwenye kadi ya chama cha siasa ni mbunge lakini ili ugombee ubunge ni lazima uteuliwe na chama chochote cha siasa chenye usajili wa kudumu pale kwa Tendwa. Hili ni sharti mojawapo la KATIBA yetu ya JMT. Ibara ya 71(1) inaeleza jinsi mtu anavyokoma kuwa mbunge. Rostam hajakidhi hitaji hili la KATIBA. Namsubiri Katibu wa Bunge atamjibu nini Rostam atakapopata barua yake ya kujiuzulu.

Wilcard you are right,as long as Rostam Aziz anaendelea kubaki na kadi yake ya CCM hajapoteza sifa ya kuwa Mbunge kama katiba inavyosema,ni mpaka pale chama chake kitakapoamua otherwise.Mimi naona huu ni mchezo wa kuigiza tusubiri tuone hii filme inavyoendelea.
 
Je wananchi wana uwezo wa kumkataa mbunge asiwatumikie? Wanaweza kumshinikiza mbunge ajiuzulu? tusaidiane hapa kwa sababu ameacha wakati wananchi "wanampenda". Je wananchi wanaweza au wana haki ya kumkataa mbunge wakati bado yeye anaupenda ubunge?
Wananchi kazi yao inamalizika wakishapiga kura tu. Baada ya hapo Mbunge ni wa chama kilichomteua kugombea. Ndicho pekee kinaweza kumwondoa hata bila kuwauliza waliomchagua au hata spika.
 
Ndugu nakushauri uzirai kama wale maskini wa roho na nafsi, usitupotezee pumzi, mtu yeyote mwenye haki ya kuchaguliwa an haki pia ya kuwajibika, huyo kawajibika!
 
Ndugu nakushauri uzirai kama wale maskini wa roho na nafsi, usitupotezee pumzi, mtu yeyote mwenye haki ya kuchaguliwa an haki pia ya kuwajibika, huyo kawajibika!
Katiba iseme hivo wazi. Mimi ni mmoja wa wanaochukia wafanyabiashara wa aina Rostam kuwa wanasiasa wetu. Tulifika mahala wafanyabiashara hawa wakatuchagulia Rais. Vurugu yote hii ndani ya CCM na serikali imesababishwa na hawa wafanyabiashara. Mwalimu alikuwa na sababu nzuri tu za kuwakataa hawa. Alipoondoka madarakani tukampuuza. Cha moto tunakiona sasa.
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.
Mkuu isome Katiba ya JMT kwa umakini na utaona kwamba tamko lake linamfanya kutokuwa mbunge wa jimbo lake; soma Ibara ya 71(1)(g) paragraph ya pili inasema nanukuu" Lakini iwapo mbunge hatakoma kuwa mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake" RA ametimiza hapo kwenye red color.
 
Back
Top Bottom