Katiba ya Tanzania: Rostam anauachaje ubunge?

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,506
2,409
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.
 
Hakuna pia katika katiba ambapo mtu analazimishwa kufanya kazi ya uwakilishi wa wananchi, ni makubaliano kati yake na wananchi anaowawakilisha, na iwapo wawakilishi anaowawakilisha watalazimisha awatumikie naye akiridhia hakuna wa kumzuia, kwani anaweza kuendelea kuwatumikia hata akiwa chama kingine (mfano mzuri ni Shibuda na Slaa).

Hili la Rostam kujiuzulu linawezekana kabisa, kwani wapo wabunge wengi waliomaliza muda wao na wakaamua hawaendelei tena kugombea ingawa wananchi wao bado walikuwa wanawahitaji.
 
Assume amkekufa, na endelea na mambo yako ya muhimu. Rostam kafanya kitu bora sana hata kama atakuwa amevunja katiba...yaani kupe anadondoka unahoji! Ulitaka anyonye damu ya ng'ombe huyu mkondefu mpaka ng'ombe adondoke au?
 
tz will remain to be tz unless we change our attitude. uzalendo+kujali maslahi ya taifa=chachu ya maendeleo
 
Hakuna pia katika katiba ambapo mtu analazimishwa kufanya kazi ya uwakilishi wa wananchi, ni makubaliano kati yake na wananchi anaowawakilisha, na iwapo wawakilishi anaowawakilisha watalazimisha awatumikie naye akiridhia hakuna wa kumzuia, kwani anaweza kuendelea kuwatumikia hata akiwa chama kingine (mfano mzuri ni Shibuna na Slaa).

Hili la Rostam kujiuzulu linawezekana kabisa, kwani wapo wabunge wengi waliomaliza muda wao na wakaamua hawaendelei tena kugombea ingawa wananchi wao bado walikuwa wanawahitaji.
Ibara ya 71(a) hadi (g) inatoa masharti ya mtu kukoma kuwa Mbunge. Hili la kujiuzulu kwa hiari yake halipo.
 
Assume amkekufa, na endelea na mambo yako ya muhimu. Rostam kafanya kitu bora sana hata kama atakuwa amevunja katiba...yaani kupe anadondoka unahoji! Ulitaka anyonye damu ya ng'ombe huyu mkondefu mpaka ng'ombe adondoke au?
Mbunge yupo kwa mujibu wa KATIBA. Ni lazima aondoke kwa mujibu wa KATIBA pia. Kama ni mwizi angetangulia kufungwa kwanza au kufukuzwa kwenye CHAMA chake.
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.

Kumbuka ya Fred Mpendazoe...
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.

Mkubwa na mimi nimesoma kwa kurudia rudia katiba sijaona sehemu inayosema mbunge awe fisadi.
Amejipima amegundua kuwa hatoshi vipimo vya uadilifu
 
Wana Magwanda Mpooooooo!
sema makamanda mpooo..
nasi tunaitika tupoooo...
hakuna kulala mpaka kieleweke.tuliwaambia toka mwanzo mkakataa.
oo wapinzani wapuuzweni,oo wapinzani hawana jipya.
bado ccm mpaka isambaratike kwa maovu waliyoifanyia nchi nii.
na wewe kwa akili yako unajiona kama magamba ndio waliofunga bao kumbe chadema tunahesabu point 3.
 
Mkubwa na mimi nimesoma kwa kurudia rudia katiba sijaona sehemu inayosema mbunge awe fisadi.
Mimi niko kwenye KATIBA yetu ya JMT. Hayo ya ufisadi sijui atabaki nani mle Bungeni tukianza kuwachambua mmoja baada ya mwingine!
 
Watanzania wenzangu,

Nimeisoma kwa kuirudia KATIBA yetu ya sasa ya JMT sijaona mahala popote panapompa Mbunge wa Bunge la Jamhuri yetu nafasi ya kuacha Ubunge kwa kujiuzulu kwa hiari yake kama alivyofanya Mh Rostam.

Nisaidieni nipate mwanga zaidi.
Unataka kumlazimisha mtu kuwa mbunge labda sijakuelewa.............mtu halazimishwi na katiba kugombea cheo chochote au kuwa mbunge.

Unaweza kuacha ubunge kwa sababu zifuatazo....
kujiuzulu kwa hiari inategemea .........
unaweza kuacha ili utunze familia, uendeleze biashara zako, masuala ya kiafya, masomo nk.
kujiuzulu kwa lazima.........
umekiuka maadili ya ubunge
umekosa chama cha kukuwakilisha mfano chama kimepoteza usajili wa kudumu
umefukuzwa na chama kilichokudhamini ubunge (kwa katiba ya sasa lazima uwe mwanachama wa chama).

Utaratibu wa kuacha kuwa mbunge....
1. kwa vile unapokuwa mbunge moja kwa moja unakuwa mwajiriwa wa bunge kwa udhamini wa chama kwahiyo
wewe mwenyewe unaweza kuliandikia bunge kuhusu kujiuzulu kwako au
unaweza kuandika barua na kukikabidhi chama kiiwasilishe bungeni kwa niaba yako kama RA alivyofanya au

2. Unaweza kupeleka barua yako moja kwa moja Tume ya uchaguzi ya Taifa na NEC ikaiwasilisha bungeni.

Baada ya mawasiliano hayo NEC ina declare jimbo liko wazi.

Kwa taarifa yako Rostam hata kabla ya jana kutangaza kujiuzulu alikwisha peleka barua kwenye chama chake.
 
Rostam ataachia ubunge kwa mujibu wa katiba ya JMT kwani ni haki yake ya msingi kufanya hivyo,jambo la muhimu afuate taratibu zinazotakiwa kwa kuandikia barua viongozi wa bunge ili Jimbo hilo litangazwe kuwa huru,then ndani ya siku 90 kieleweke nani analichukua jimbo hilo.
 
Unataka kumlazimisha mtu kuwa mbunge labda sijakuelewa.............mtu halazimishwi na katiba kugombea cheo chochote au kuwa mbunge.

Unaweza kuacha ubunge kwa sababu zifuatazo....
kujiuzulu kwa hiari inategemea .........
unaweza kuacha ili utunze familia, uendeleze biashara zako, masuala ya kiafya, masomo nk.
kujiuzulu kwa lazima.........
umekiuka maadili ya ubunge
umekosa chama cha kukuwakilisha mfano chama kimepoteza usajili wa kudumu
umefukuzwa na chama kilichokudhamini ubunge (kwa katiba ya sasa lazima uwe mwanachama wa chama).

Utaratibu wa kuacha kuwa mbunge....
1. kwa vile unapokuwa mbunge moja kwa moja unakuwa mwajiriwa wa bunge kwa udhamini wa chama kwahiyo
wewe mwenyewe unaweza kuliandikia bunge kuhusu kujiuzulu kwako au
unaweza kuandika barua na kukikabidhi chama kiiwasilishe bungeni kwa niaba yako kama RA alivyofanya au

2. Unaweza kupeleka barua yako moja kwa moja Tume ya uchaguzi ya Taifa na NEC ikaiwasilisha bungeni.

Baada ya mawasiliano hayo NEC ina declare jimbo liko wazi.

Kwa taarifa yako Rostam hata kabla ya jana kutangaza kujiuzulu alikwisha peleka barua kwenye chama chake.
Rostam aliupata UBUNGE KIKATIBA. Haya unayoeleza hapa ni kifungu kipi kwenye KATIBA yetu? Au tuenende kiholela tu!
 
Jaman baada ya hiyo ibara 71 (1) (g) kuna proviso. Inosomeka hivi;

"lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge
litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake"

Naomba kuwasilisha
 
R.I.P RA Tunakuomba pia urudishe mali za watanzania ulizoiba na utuombe msamaha kwa mabaya yote uliyotutendea
 
Back
Top Bottom