Katiba ya CCM ni ya kibaguzi

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,675
29,881
Viongozi wa dola kupitia CCM kuanzia Wabunge, Madiwani na Wenyeviti Mitaa, Vijiji na Vitongoji hawaruhusiwi kugombea nafasi yeyote ndani ya chama. Ingawa wanaingia kamati za siasa ndani ya ngazi maeneo yao. Katiba ya CCM imewawekea utaratibu wa mtu mmoja nafasi moja.

Lakini ukiangalia katiba hiyo hiyo inampa mamlaka mtu mwenye majukumu mengi sana tena yanayochosha na taabu nyingi kuwa ndiye mwenyekiti wa chama Taifa.

Hizi double standards zinaleta ukakasi kwenye uwiano na kutekeleza majukumu ya kazi. Mwenyekiti wa CCM Taifa ndiye msimamizi mkuu wa Ilani ya Uchaguzi na ndiye husimamia serikali kwenye kuitathmini utekelezaji wake.

Rais ambaye anakabidhiwa Ilani na kuinadi ili achaguliwe, ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani lakini ndiye huyo huyo anayeongoza vikao vya kupokea na kujadili utekelezaji wa Ilani.

Inaleta tafakuri jadidi sana kuhusu uwezo wa binadamu kujitathmini badala ya kutathiminiwa na wengine.
  1. Leo World Bank ndiyo wanaotathmini na kutoa takwimu za mwenendo wa uchumi wetu.
  2. CAG yupo kwa sheria iliyotungwa na Bunge kuweka bayana mwenendo wa transactions za serikali na yupo huru kukagua na siyp sehemu ya watendaji wa serikali
  3. Bunge hutunga sheria lakini mahakama ndiyo inayozitafsiri sheria na dola hutekeleza tafsiri za mahakama
Litakuwa jambo la hekima endapo CCM inataka kujiimarisha na kujikosoa pale ambapo nafasi za uongozi wa ndani ya chama zitatenganishwa na nafasi za uongozi wa dola.

Mwenyekiti wa CCM Taifa awe ni kiongozi ndani ya chama.na siyo mkuu wa nchi. Rais apewe nafasi ya kutekeleza ilani na chama kimfanyie tathmini kwa haki.
 
Viongozi wa dola kupitia CCM kuanzia Wabunge, Madiwani na Wenyeviti Mitaa, Vijiji na Vitongoji hawaruhusiwi kugombea nafasi yeyote ndani ya chama.
Ingawa wanaingia kamati za siasa ndani ya ngazi maeneo yao. Katiba ya CCM imewawekea utaratibu wa mtu mmoja nafasi moja.
Nia ni kwamba chama kizicontroo taasisi zote za Nchi zenye maguvu. !!!
 
Mwenyekiti akiwa ndiye Rais ina maana kubwa sana.
Katiba ya nchi imeweka bayana kwamba Rais hakuna wakati anakuwa siyo rais pale ambapo yupo madarakani.

Hivyo akiwa kwenye vikao ama utendaji wa nafasi yake ya Uenyekiti Taifa bado anaweza kutoa amri ambazo zinaleta effect chanya kwa CCM na effect hasi kwa Upinzani.

Balance of powers inakuwa in question mara zote. Ndo maana unakuta chaguzi za teuzi za wagombea wa CCM huwashirikisha mpaka watu wa Utawala Bora kinyume na teuzi za Upinzani. Ni kwa sababu Mkuu wa Chama ndiye Amiri Jeshi Mkuu na dola INAPASWA kumtii.

Tutenganishe kofia hizo as kuelejea kwenye njia ya kupata muafaka wa kisiasa Kitaifa.
 
CCM, nawaonea huruma sana wafuasi wake, ni kama tu Makerubi wa Mfalme Zumaridi
Neno kubwa hili.
Najua na nimedokezwa kuwa navuka mstari lakini ni vyema kuishi kwenye ukweli kwamba CCM isiyobadilika ni kansa kwa Taifa.

CCM ilipaswa kuimarisha siasa za vyama vingi badala yake inahakikisha inabomoa msingi huo ili kijiimarishe madarakani.

Ni kosa kubwa kisiasa
 
Hawa watu ndugu ni sikio la kufa wanaona ni ufahali vyombo vyetu vya ulinzi kujazana kwenye mavikao Yao ya chama
 
Mwenyekiti akiwa ndiye Rais ina maana kubwa sana.
Katiba ya nchi imeweka bayana kwamba Rais hakuna wakati anakuwa siyo rais pale ambapo yupo madarakani.

Hivyo akiwa kwenye vikao ama utendaji wa nafasi yake ya Uenyekiti Taifa bado anaweza kutoa amri ambazo zinaleta effect chanya kwa CCM na effect hasi kwa Upinzani.

Balance of powers inakuwa in question mara zote. Ndo maana unakuta chaguzi za teuzi za wagombea wa CCM huwashirikisha mpaka watu wa Utawala Bora kinyume na teuzi za Upinzani. Ni kwa sababu Mkuu wa Chama ndiye Amiri Jeshi Mkuu na dola INAPASWA kumtii.

Tutenganishe kofia hizo as kuelejea kwenye njia ya kupata muafaka wa kisiasa Kitaifa.
Hofu kuu ni kupunguza udhibiti kwenye taasisi zenye maguvu !! Ukienda kwenye taasisi hizo na gwanda lako la mbogamboga unaonekana unastahili kupata umuhimu wa kipekee !! Something special !!
 
Neno kubwa hili.
Najua na nimedokezwa kuwa navuka mstari lakini ni vyema kuishi kwenye ukweli kwamba CCM isiyobadilika ni kansa kwa Taifa.

CCM ilipaswa kuimarisha siasa za vyama vingi badala yake inahakikisha inabomoa msingi huo ili kijiimarishe madarakani.

Ni kosa kubwa kisiasa
Kabisa kabisa !! Chama ambacho hakitaki kusikia mtu akikosoa chochote na wakikusikia unakosoa wanakuhesabu sio mwenzao na ni adui yao ni Hatari sana. !!
 
Usitupangie, Hizo ngonjera zako peleka pale ufipa kwa mwenye kigoda wa kudumu aliyegeuza chama Kama mradi wake binafsi wa kutafunia fedha
 
Naye atakuwa kaiga kutoka CCM
Mwenyekiti anasema vyama upinzani waanze kuonesha demokrasia kwao wakati yeye amesimama juu ya jukwaa lenye kila aina ya ukandamizi, ukatili na ubaguzi
 
Hofu kuu ni kupunguza udhibiti kwenye taasisi zenye maguvu !! Ukienda kwenye taasisi hizo na gwanda lako la mbogamboga unaonekana unastahili kupata umuhimu wa kipekee !! Something special !!
Umesema kweli kabisa.

Kwa mfano leo ikitokea mwanachama wa CCM akaenda kufanya vurugu jirani na kusanyiko la upinzani. Polisi wakija wanaanza moja kwa moja kuvunja kusanyiko lile na kuwakamata upinzani.

Haya yanawezekana kwa sababu Mkuu wa Cha.ndiye Dola Sponsor.
 
Viongozi wa dola kupitia CCM kuanzia Wabunge, Madiwani na Wenyeviti Mitaa, Vijiji na Vitongoji hawaruhusiwi kugombea nafasi yeyote ndani ya chama.
Ingawa wanaingia kamati za siasa ndani ya ngazi maeneo yao. Katiba ya CCM imewawekea utaratibu wa mtu mmoja nafasi moja.

Lakini ukiangalia katiba hiyo hiyo inampa mamlaka mtu mwenye majukumu mengi sana tena yanayochosha na taabu nyingi kuwa ndiye mwenyekiti wa chama Taifa.

Hizi double standards zinaleta ukakasi kwenye uwiano na kutekeleza majukumu ya kazi. Mwenyekiti wa CCM Taifa ndiye msimamizi mkuu wa Ilani ya Uchaguzi na ndiye husimamia serikali kwenye kuitathmini utekelezaji wake.

Rais ambaye anakabidhiwa Ilani na kuinadi ili achaguliwe, ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani lakini ndiye huyo huyo anayeongoza vikao vya kupokea na kujadili utekelezaji wa Ilani.

Inaleta tafakuri jadidi sana kuhusu uwezo wa binadamu kujitathmini badala ya kutathiminiwa na wengine.
  1. Leo World Bank ndiyo wanaotathmini na kutoa takwimu za mwenendo wa uchumi wetu.
  2. CAG yupo kwa sheria iliyotungwa na Bunge kuweka bayana mwenendo wa transactions za serikali na yupo huru kukagua na siyp sehemu ya watendaji wa serikali
  3. Bunge hutunga sheria lakini mahakama ndiyo inayozitafsiri sheria na dola hutekeleza tafsiri za mahakama
Litakuwa jambo la hekima endapo CCM inataka kujiimarisha na kujikosoa pale ambapo nafasi za uongozi wa ndani ya chama zitatenganishwa na nafasi za uongozi wa dola.

Mwenyekiti wa CCM Taifa awe ni kiongozi ndani ya chama.na siyo mkuu wa nchi. Rais apewe nafasi ya kutekeleza ilani na chama kimfanyie tathmini kwa haki.
Tanzania hali sio shwari. Ccm ndani kwa ndani wanalia .
Serikali inalia
Wananchi wanalia
Upinzani wanalia

Aliyepewa nchi na chama tawala haongei na hasikiki
Mtanikumbuka
 
Neno MRANIKUMBUKA ni legacy ambayo kwa sasa siyo hoja.

Tangu tumeingia siasa za vyama vingi niaorodheshee rais ambaye alisimama kuwa fair bila kuwabagua vyama vingine.

Inawezekana kabisa hata mimi leo nikachaguliwa kuwa mgombea wa CCM hivyo kutokana na mfumo fisi uliopo chamani lazima ninate na tempo yao.

Ni bora kukibadilisha kitoke madarakani kikajipange na kujifunza maana ya uzalendo kikiwa kwenye jukwaa la upinzani
 
Tanzania hali sio shwari. Ccm ndani kwa ndani wanalia .
Serikali inalia
Wananchi wanalia
Upinzani wanalia

Aliyepewa nchi na chama tawala haongei na hasikiki
Mtanikumbuka
“Karma “ Let them keep on harassing wazee faida yake wataipata mbele ya safari !! “Karma “
 
Back
Top Bottom