Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,731
- 29,986
Viongozi wa dola kupitia CCM kuanzia Wabunge, Madiwani na Wenyeviti Mitaa, Vijiji na Vitongoji hawaruhusiwi kugombea nafasi yeyote ndani ya chama. Ingawa wanaingia kamati za siasa ndani ya ngazi maeneo yao. Katiba ya CCM imewawekea utaratibu wa mtu mmoja nafasi moja.
Lakini ukiangalia katiba hiyo hiyo inampa mamlaka mtu mwenye majukumu mengi sana tena yanayochosha na taabu nyingi kuwa ndiye mwenyekiti wa chama Taifa.
Hizi double standards zinaleta ukakasi kwenye uwiano na kutekeleza majukumu ya kazi. Mwenyekiti wa CCM Taifa ndiye msimamizi mkuu wa Ilani ya Uchaguzi na ndiye husimamia serikali kwenye kuitathmini utekelezaji wake.
Rais ambaye anakabidhiwa Ilani na kuinadi ili achaguliwe, ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani lakini ndiye huyo huyo anayeongoza vikao vya kupokea na kujadili utekelezaji wa Ilani.
Inaleta tafakuri jadidi sana kuhusu uwezo wa binadamu kujitathmini badala ya kutathiminiwa na wengine.
Mwenyekiti wa CCM Taifa awe ni kiongozi ndani ya chama.na siyo mkuu wa nchi. Rais apewe nafasi ya kutekeleza ilani na chama kimfanyie tathmini kwa haki.

- Leo World Bank ndiyo wanaotathmini na kutoa takwimu za mwenendo wa uchumi wetu.
- CAG yupo kwa sheria iliyotungwa na Bunge kuweka bayana mwenendo wa transactions za serikali na yupo huru kukagua na siyp sehemu ya watendaji wa serikali
- Bunge hutunga sheria lakini mahakama ndiyo inayozitafsiri sheria na dola hutekeleza tafsiri za mahakama