Katiba Mpya (polls)

Je, unadhani katiba mpya ni muhimu kwa Tanzania ya sasa?

  • Hapana, Katiba mpya bado haina umuhimu, Iliyopo bado inakidhi mahitaji

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    3

Los técnicos

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
3,010
2,604
Tafiti ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku pengine ndiyo huchukua nafasi muhimu ya maamuzi katika maisha yetu.

Leo, binafsi ningependa kujua takwa/dai la katiba liko kwa kiwango kipi ndani ya mioyo yetu wadau wa jamiiforums.

Karibuni!

Piga kura yako, onesha hitaji lako
 
Naunga mkono uwepo wa Katiba mpya ya wananchi. Hii iliyopo ilitengenezwa kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya chama kimoja! Yaani ccm.

Huku Mwenyekiti wake, ambaye pia huwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, akipewa mamlaka makubwa ya kuwa Rais Mfalme.
 
Naunga mkono uwepo wa Katiba mpya ya wananchi. Hii iliyopo ilitengenezwa kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya chama kimoja! Yaani ccm.

Huku Mwenyekiti wake, ambaye pia huwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, katiba hiyo hoyo humpa mamlaka ya Rais Mfalme.
Hao Wananchi wanaijua vizuri katiba iliyopo? Au tunataka kutumia migongo ya watu wasioelewa katiba iliyopo? Vipi badae wakigundua wametumika?

Huu ni wakati muafaka ambao raia wanapaswa kuielewa katiba iliyopo ili inapodaiwa mpya wote tuwe kwenye msitari mmoja.

Nauona ugumu kwenye kudai katiba kwa sababu ni kundi dogo tu lenye uelewa na katiba iliyopo na kundi kubwa halifahamu chochote.

Tukisema tuishie kwenye tafiti za mitandaoni pia tutaishia kupata maoni ya kundi dogo tu lenye access ya mitandao na lile kundi kubwa lisilo na access maoni yao hatutayapata.

Kwa sasa tujikite kwenye kuijua vyema katiba iliyopo kwa sababu kama lingekuwa ni hitaji kubwa la Wananchi wakati wa kampeni Wananchi wangeomba kwa viongozi waliokuwa wananadi sera zao.
 
Wananchi siyo mbumbumbu kiasi hicho unachowaza! Ushahidi ni wakati wa Tume ya Katiba ya Jaji Warioba ilipozunguka Nchi nzima kukusanya maoni kwa wananchi!

Wananchi hawa hawa unao wachukulia kama wajinga na wasio na uelewa wowote ule, walitoa maoni yao kwa uwazi! Na ndipo ilipokuja kuzaliwa ile Rasimu ya Katiba, iliyo ishia mikononi mwa wanasiasa kutoka ccm na ukawa.
 
Kwanza naweza kusema hawakutoa maoni kuwa wanahitaji katiba mpya, Bali maoni kwakile kilichokuwemo kwenye rasimu.

Pili, utatakaje upate maoni ya kitu kipya wakati kilichopo wanakijua wachache tu. Hapa pia Wananchi waliburuzwa kwa sababu wengi hawana uelewa wa kutosha kwa katiba iliyopo
 
Hao Wananchi wanaijua vizuri katiba iliyopo? Au tunataka kutumia migongo ya watu wasioelewa katiba iliyopo? Vipi badae wakigundua wametumika?

Huu ni wakati muafaka ambao raia wanapaswa kuielewa katiba iliyopo ili inapodaiwa mpya wote tuwe kwenye msitari mmoja.

Nauona ugumu kwenye kudai katiba kwa sababu ni kundi dogo tu lenye uelewa na katiba iliyopo na kundi kubwa halifahamu chochote.

Tukisema tuishie kwenye tafiti za mitandaoni pia tutaishia kupata maoni ya kundi dogo tu lenye access ya mitandao na lile kundi kubwa lisilo na access maoni yao hatutayapata.

Kwa sasa tujikite kwenye kuijua vyema katiba iliyopo kwa sababu kama lingekuwa ni hitaji kubwa la Wananchi wakati wa kampeni Wananchi wangeomba kwa viongozi waliokuwa wananadi sera zao.
Binafsi si dhani kama hoja hii ya kwamba pengine ni hoja ya kundi dogo haina mashiko, kwa sababu hata ile ya kwanza haikutengenezwa na watanzania wote, kilikuwa kikundi kidogo zaidi ya hiki unachodhani leo. Na kibaya zaidi kilikuwa ni kikundi ambacho ni homogeneous, watu wenye itikadi moja ya kichama, bunge lenye itikadi moja ya kichama na hata serikali ya chama kimoja. Hivyo hoja yako haina mashiko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom